Tafuta

Hadhi ya Binadamu tuliyopewa na Mungu Hadhi ya Binadamu tuliyopewa na Mungu  (©Africa Studio - stock.adobe.com)

Tarehe 8 Aprili itachapishwa Hati juu ya "hadhi ya binadamu isiyo na mwisho"

Tamko la“Dignitas Infinita”litachapishwa Jumatatu Aprili 8 na kuwasilishwa siku hiyo hiyo katika Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican na Kardinali Fernandez,Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa,katibu wake Monsinyo Armando Matteo na Profesa Paola Scarcella.

Vatican News

“Dignitas Infinita,”yaani “Hadhi isiyo na mwisho,” ndicho kichwa cha tamko kuhusu mada ya Hadhi ya  binadamu iliyohaririwa na Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa  litakalochapishwa mnamo tarehe 8 Aprili 2024. Hati hiyo itawasilishwa siku hiyo hiyo, saa 6.00 mchana kamili, katika mkutano kwenye Chumba cha Waandishi wa Habari cha Vatican, na Kadinali Víctor Manuel Fernández, na Monsinyo Armando Matteo, Mwenyekiti na katibu wa  Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa, na Profesa Paola Scarcella wa Chuo Kikuu cha Tor Vergata na Chuo Kikuu cha Lumsa cha Roma, anayehusika na Katekesi ya watu wenye ulemavu katika Jumuiya ya Mtakatifu Egidio.

Mkutano wa waandhishi utaoneshwa moja kwa moja au(Mbashara)katika lugha asilia kwenye chaneli ya YouTube ya Vatican News, kwa kuunganisha kwenye tovuti(sito.) Na itawezekana kupata njia za kutafsiriwa kwa wakati mmoja na kusikiliza mkutano wa waandishi wa habari kwa lugha ya Kiitaliano, Kiingereza na Kihispania.

Tangu Novemba 2023, Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa, inayoongozwa na Kardinali Fernandez, imetoa hati kadhaa kwa kujibu maswali kutoka kwa maaskofu au makadinali juu ya mada tofauti kama vile: Watu wasio na jinsia tofauti wanaweza kupokea Ubatizo(rej.la possibilità per le persone transessuali di ricevere il Battesimo,) na pia watoto wa watu wa jinsia moja ikiwa alizaliwa kutoka katika tumbo la kukodi; umarufuku(rej.divieto )kwa wakatoliki kujiandikisha kwenye vikundi vya Freemasons; marufuku kuweka majivu ya wafu ndani ya nyumba(rej.collocazione delle ceneri):kuhamasisha mama wasio na mme ili kujongea katika Sakramenti(rej.incoraggiamento alle madri single).

Na tarehe 18 Desemba 2023 pia Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa, lilichapisha hati ya(Fiducia Supplicans,)yaani imani katika kuomba, ambayo ilifungua uwezekano wa kubariki watu wawili wasio wa kawaida(mashoga),lakini nje ya ibada yoyote na  isyo na aina ya kuiga harusi.

02 April 2024, 17:00