Tafuta

Nembo ya Jubilei  2025 . Nembo ya Jubilei 2025 . 

Jubilei 2025:PUM inafanya mafunzo ya tafakari na sala kwa njia ya mtandao!

Katika mwaka uliowekwa wakfu kwa ajili ya Sala katika maandalizi ya kuelekea Jubilei ya 2025,Umoja wa Mashirika ya Kipapa ya Kimisionari (PUM)imeandaa mafunzo kwa njia ya Mtandao kuhusu sala na tafakari kuanzia tarehe 7,17,28 Septemba na 8 Oktoba 2024.Unaweza kujiandikisha.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

“Safari ya wanafunzi wamisionari,” ndiyo kauli mbiu inayoongoza ratiba ya mikutano 4 kwa njia ya mtandao kwa lugha ya Kiingereza kuhusu sala, iliyoandaliwa na kuhamasishwa na Umoja wa Mashirika ya Kimisionari ya Kipapa (PUM)kwa ajili ya maandalizi ya Jubilei ya  2025. Mkutano wa kwanza ulifanyaika tarehe 7 Septemba, kuanzia saa 11.00 jioni  hadi saa 1.30 usiku masaa ya Roma ambapo mikutano itakuwa inafanyika muda huo kama  ilivyopangwa.

Katika mwaka wa sala kwa njia hiyo PUM inatoa, miongoni mwa mengine, pendekezo hilo la mafunzo ya kimisionari ambalo linaanza kutokana na mwaliko Papa Francisko, ambaye aliandika katika Ujumbe wa Siku ya Kimisionari Duniani mwaka huu 2024 kuwa: “Kwa mtazamo huo, katika mwaka uliowekwa wakfu kwa sala kwa ajili ya maandalizi ya Jubilei ya 2025, ningependa kuwaalika watu wote pia na zaidi ya yote kuzidisha ushiriki wa Misa na maombi kwa ajili ya utume wa uinjilishaji wa Kanisa.” Kwa njia hiyo waliongeza kuwa “Yeye, kwa kutii neno la Mwokozi, haachi kuinua sala ya Baba Yetu kwa Mungu katika kila adhimisho la Ekaristi na liturujia kwa wito wa Ufalme wako ufike.”

Kwa njia hiyo Jumamosi tarehe 7  2024  mada ya mkutano ilikuwa ni: “njia ya Yesu ya kusali” wakati  Jumanne tarehe 17 Septemba mada itakuwa zamu ya “Sala ya Baba Yetu - Sala ya kimisionari.”  Jumamosi 28 Septemba  mada itazungumzwa juu ya “Sala” ya wanafunzi wa Kristo,” wakati tukio la mwisho  la Jumanne tarehe 8 Oktoba 2024 na la mwisho  itakuwa na mada kuhusu:  “Ekaristi chanzo na kilele cha Utume na Sala.” Mpango huo utaratibiwa na Padre Dinh Anh Nhue Nguyen OFMConv, Katibu mkuu wa PUM, ambaye atashirikiana na Padre Tadeusz J. Nowak OMI, Katibu mkuu wa Shirika la Kipapa la Kueneza Imani.

Siku ya Jumamosi tarehe 7 Septemba 2024, Padre Nguyen alitambulisha mada, kisha alitoa nafasi kwa ajili ya hotuba ya Padre Nowak. Ushiriki huko huru hata kama inapendekezwa  kwamba ni bora kujiandikisha kwa ajili ya maadalizi mema kwa kutumia barua pepe ifuatayo:pum@ppoomm.va.

 

09 September 2024, 16:14