Tafuta

2024.09.16 Mkutano wa uwakilishi wa Sinodi ijayo ya Oktoba 2024 kwa waandishi wa habari 2024.09.16 Mkutano wa uwakilishi wa Sinodi ijayo ya Oktoba 2024 kwa waandishi wa habari  (Vatican Media)

Viongozi wa Sinodi watoa maelezo ya Mkutano Mkuu wa Oktoba

Makardinali Grech na Hollerich,pamoja na Padre Costa na Monsinyo Battocchio,walieleza kwa undani zaidi juu ya Mkutano Mkuu wa Oktoba wa Sinodi katika mkutano wa uwakilishi uliofanyika mjini Vatican una ambao ulisimamiwa na Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano.Papa ataongoza toba yenye ushuhuda kutoka kwa waathiriwa wa dhuluma,vita,na kutojali uhamiaji.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Sinodi ni wakati wa maombi, “sio kusanyiko,” bali “kusanyiko la Kanisa linaloomba,” wakati wa kusikiliza Neno la Mungu na Roho, na fursa ya kuomba msamaha kutoka kwa Mungu kwa ajili ya dhambi za Kanisa. Kardinali Mario Grech, Katibu Mkuu wa Sekretarieti Kuu ya Sinodi akiwasilisha kikao cha pili cha Mkutano Mkuu wa XVI wa kawaida wa Sinodi ya Maaskofu kitakachofanyika mjini Roma kuanzia tarehe 2 hadi 27 Oktoba  2024 wakati wa mkutano na waandishi wa habari, Jumatatu,tarehe 16 Septemba. Alikumbuka kwamba Papa Francisko, katika ufunguzi wa njia ya sinodi tarehe 9 Oktoba 2021, alisisitiza kwamba "mhusika mkuu wa Sinodi ni Roho Mtakatifu."

Uwakilishi wa Sinodi ijayo Okotba 2024
Uwakilishi wa Sinodi ijayo Okotba 2024

Dk.Paolo Ruffini, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la  Mawasiliano na Rais wa Tume ya Habari ya Sinodi, aliwasilisha michango iliyoonesha mkutano wa sinodi katika Ofisi ya Waandishi wa Habari. Kwa upande wake alikumbuka kwamba, kulingana na kifungu cha 24 cha Kanuni za Sinodi "kila mmoja wa washiriki anatakiwa kudumisha usiri", hii "kulinda utambuzi wa bure wa kila mtu", na "kupumzika" kutoka katika haraka haraka  ambazo sisi sote tumezamishwa ndani yake na kutoka katika mazoea ya nyuma na mbele. Ni njia ambayo, Dk. Ruffini alisema, akikumbuka maneno ya Papa mwaka 2023, kuwa "inaweza kusaidia ulimwengu, sio tu Kanisa, katika nyanja nyingi na juu ya maswala mengi"."  Mbinu ni kuajiachia, kusikiliza na kuelewana. Kupitia kiunga cha video, Sheila Pires, katibu wa Tume ya Habari, alielezea vifaa kwa waandishi wa habari na kuorodhesha baadhi ya matukio kwenye kalenda. Kuhusu mawasiliano, kikao cha pili kitakuwa na mdundo tofauti na wa kwanza: vikao vichache, na utulivu mwingi wa kutafakari, maombi na utambuzi.

Mafungo ya Kiroho na Mkesha wa Toba

Kardinali Grech alieleza kwamba, sawa na kikao cha kwanza, kikao hiki cha pili na cha mwisho cha Sinodi ya Sinodi kitatanguliwa na siku mbili za mafungo ya kiroho kuanzia tarehe 30 Septemba na Oktoba 1 mjini Vatican, kikiongozwa na tafakari kutoka kwa Padre  Mdominikani, Timothy Radcliffe na Mama Benediktini Sr  Ignazia Angelini. Wataongoza sala wakati wa Sinodi, pamoja na Padre wa Camaldoli Matteo Ferrari, ambao watawajibika kwa liturujia; na watawa wa Camaldoli. Mapya ya mwaka huu itakuwa mkesha wa toba baada ya mafungo, yatakayofanyika jioni ya Jumanne, tarehe 1 Oktoba 2024 kwenye Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, na kuongozwa na Papa Francisko.

Kardinai Grech akiwakilisha kwa waandishi wa habari juu ya Sinodi Ijayo
Kardinai Grech akiwakilisha kwa waandishi wa habari juu ya Sinodi Ijayo

Toba hiyo imeandaliwa na Sekretarieti Kuu ya Sinodi na Jimbo la Roma kwa ushirikiano na Umoja wa Mama Wakuu wa mashirika (USG) ambayo itatangazwa na Vyombo vya Habari vya Vatican na kuwa wazi kwa wote, hasa vijana, “kwa sababu ujumbe wa Kanisa umekabidhiwa kwao,” Kardinali Hollerich alisema alisisitiza kwamba “vijana wanateseka kwa sababu ya dhambi zetu na dhambi ndani ya Kanisa.” Sherehe hiyo itaakisi ushuhuda kutoka kwa watu watatu ambao wamepitia dhambi za unyanyasaji, vita, na kutojali kwa mzozo unaokua wa uhamiaji.

Maungamo kutambua mateso

Kisha kutakuwa na maungamo ya dhambi ili “kujitambua kuwa sehemu ya wale ambao, kwa kutotenda au kutenda, wanawajibika kwa mateso na madhara yanayovumiliwa na wasio na hatia na wasio na ulinzi,” Kardinali Grech alisisitiza. Hasa, dhambi dhidi ya amani, uumbaji, watu wa kiasili, wahamiaji, wanawake, familia, vijana; dhambi ya kutumia mafundisho kama jiwe dhidi ya wengine, dhambi dhidi ya umaskini na sinodi (kama vile kushindwa kusikiliza, au dhambi kuathiri ushirika au ushiriki wa wote) itaungamwa. Papa atahitimisha kwa kuomba msamaha kwa Mungu na wanadamu wote kwa niaba ya waamini wote.

Sala ya Kiekumene

Ibada ya maombi ya kiekumene pia itafanyika jioni ya tarehe 11 Oktoba jijini  Vatican kwenye Uwanja wa Mashahidi wa kwanza, ambapo mapokeo yanashikilia kuwa Mtakatifu Petro aliuawa. Tarehe hii ni kumbukumbu ya miaka 62 tangu kufunguliwa kwa Mtaguso mkuu wa Pili wa Vatican. Hatimaye, tarehe 21 Oktoba, kutakuwa na siku nyingine ya mapumziko ya kiroho katika matayarisho ya utambuzi wa rasimu ya hati ya mwisho. Kama Kardinali Grech alivyosema, kutakuwa na “mbadiliko kati ya sala ya kibinafsi, mazungumzo, na ushirika wa kindugu katika kusikilizana na upendo.”

Vikao vinne vilivyo wazi kwa wote

Kipengele kingine kipya kitakuwa vikao vinne vya kitheolojia-kichungaji, ambavyo vitakuwa wazi kwa wote, wakiwemo waandishi wa habari walioidhinishwa. Vikao viwili vitafanyika tarehe 9 Oktoba 2024, moja juu ya “Watu wa Mungu, fundisho la utume ” katika Ukumbi wa Nyumba mama ya  Kijesuit  na lingine juu ya “Wajibu na Mamlaka ya Askofu katika Kanisa la Sinodi” katika  Taasisi ya Augustino. Mikutano miwili iliyosalia itafanyika Oktoba 16. Mada zitakuwa "Mahusiano ya Kuheshimiana kati ya Kanisa la Mtaa na la Ulimwengu Wote" katika Ukumbi wa Nyumba Mama  ya Kijesuit na "Zoezi la Ukuu na Sinodi ya Maaskofu" katika Taasisi ya Baba wa Kanisa Augustinianum. Mabaraza haya yatahusisha wataalimungu, waamini watakatifu, maaskofu, na wengineo, pamoja na fursa ya mazungumzo. Mkutano huo pia utapatikana mtandaoni.

Idadi ya washiriki wa sinodi

Kardinali Hollerich alieleza kwamba idadi ya washiriki katika kikao hiki cha pili ni sawa na ile ya kwanza, yenye wajumbe 368 waliopiga kura, wakiwemo maaskofu 272 na wasio maaskofu 96. Kumekuwa na mabadiliko 26, hasa mbadala. Kuna waalikwa maalum 8, wakati idadi ya wajumbe ndugu imeongezeka kutoka 12 hadi 16, ikionesha shauku inayokua ya Makanisa dada katika safari ya kisinodi. Pia alithibitisha kuwepo kwa maaskofu wawili kutoka China.

Kikao kuhusu Sinodi Ijyao Oktoba 2024
16 September 2024, 17:05