Tafuta

2025.02.27 Sala mbele ya Sanamu ya Mtakatatifu wa Armenia Gregory wa Narek, mwalimu wa Kanisa iliyoko kwenye Bustani za Vatican. 2025.02.27 Sala mbele ya Sanamu ya Mtakatatifu wa Armenia Gregory wa Narek, mwalimu wa Kanisa iliyoko kwenye Bustani za Vatican. 

Sala kwa Mtakatifu Gregori wa Narek kwa ajili ya uponyaji wa Papa Francisko

Katika tukio la sikukuu ya kiliturujia ya mtawa wa Armenia aliyetangazwa kuwa Mwalimu wa Kanisa na Papa Francisko,ilifanyika sala kwa ajili ya afya ya Papa mbele ya sanamu ya Mtakatifu huyo iliyoko katika bustani ya Vatican:"Uondoe uchungu na uponye magonjwa ya watu wako na mtumishi wako Papa Francisko,Bwana Mungu wetu na uwajalie wote afya kamilifu kwa njia ya Msalaba wako wa ushindi,ambao umeharibu udhaifu wa wanadamu."

Vatican News

Ewe Mtakatifu Gregori wa Narek, mwombee mrithi wa Mtakatifu Petro, Baba Mtakatifu Francisko. Umpe nguvu, afya na uponyaji, ili aweze kuendeleza utume wake na huduma yake ya kujitolea kwa watu wa Mungu. Ni katika sala iliyoinuliwa chini ya sanamu ya Mtakatifu Gregory wa Narek, mtawa wa Armenia na wa ibada ya kina, Mwalimu wa Kanisa la Ulimwengu, kwa dakika maalum kwa ajili ya kumuombea Baba Mtakatifu Francisko ili apone iliyofanyika tarehe 27 Februari 2025, saa 9.00 asili katika bustani ya Vatican.

Ni katika fursa siku ya sikukuu ya kiliturujia ya Mtakatifu huyo ambaye Papa aliamua kuadhimishwa kila ifikapo tarehe 27 Februari ya kila mwaka. Ubalozi wa Armenia unaowakilisha nchi hiyo mjini Vatican, ukiongozwa na Balozi Boris Sahakyan, ulitaka kuweka wakfu siku hiyo pamoja na mkuu wa Chuo cha Kipapa cha Kiarmenia, Monsinyo Khachig Kouyoumadjian kwa maadhimisho ya kumuombea Papa Francisko aliyelazwa hospitalini tangu tarehe 14 Februari 2025 katika Hospitiali ya Gemelli Roma. Na aliyekuwepo katika sherehe hiyo, miongoni mwa wengine ni Sr  Arousiag Sagionia, mkuu wa Shirika la Masista wa Kiarmenia wa Moyo Safi wa Bikira Maria.

Sala kwa Mtakatifu wa Armenia
Sala kwa Mtakatifu wa Armenia

Kitabu cha Maombolezo cha Gregory wa Narek kina muktadha wa kibiblia kwa Waarmenia. Kila familia ya Waarmenia, pamoja na Biblia Takatifu, kama  lishe ya kiroho ya watu, ambao hupokea daima upatanisho kwa ajili ya dhambi na uponyaji kwa wagonjwa. Na ni kwa nia hiyo kwamba sala kwa maombezi ya Mtakatifu wa Armenia kuomba maombezi yake kwa ajili ya uponyaji wa Baba Mtakatifu Francisko.

Sala

Kwa njia hiyo kundi hilo lililokusanyika mbele ya sanamu hiyo na kusali:  “Uondoe uchungu na uponye magonjwa ya watu wako na mtumishi wako Papa Francisko, Bwana Mungu wetu, na uwajalie wote afya kamilifu kwa njia ya Msalaba wako wa ushindi, ambao kwa huo umeharibu udhaifu wa wanadamu na kulaani adui wa maisha yetu na imani yetu. Wewe ndiwe uhai wetu na nguvu zetu, Mungu wa rehema na huruma, ambaye peke yake ndiye awezaye kusamehe dhambi na kutuondolea magonjwa na udhaifu. Unajua mahitaji ya wahitaji wako. Mpaji wa vitu kulingana na hitaji la kila mtu. Uwajalie rehema zako kwa wingi viumbe wako, ambao kwa njia yao Utatu Mtakatifu unatukuzwa na kupendwa daima, sasa na milele na milele. Amina".

Kubariki
28 Februari 2025, 12:08