Jubilei ya Makanisa ya Mshariki katika Kanisa Kuu la Mt.Petro na Liturujia ya Ethiopia
Vatican News
Sherehe muhimu sana katika fursa ya Jubilei ya Makanisa ya Mashariki ambapo Jumatatu tarehe 12 Mei 2025: Ibada ya Kimungu ya utamaduni ya Ibada ya Ethiopia ilishuhudiwa katika Kanisa la Kwaya ya Basilika ya Mtakatifu Petro ikiwa na Kanisa la Ethiopia na Kanisa la Eritrea. Ibada hiyo iliongozwa na Askofu Mkuu wa Addis Ababa, Kardinali Berhaneyesus Demerew Souraphiel, kwa kusaidiana na Askofu Mkuu wa Asmara, Menghesteab Tesfamariam.
Mwanzoni, mwa ibada hiyo, Kardinali Claudio Gugerotti, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Makanisa ya Mashariki alitoa salamu zake hapo na kuwashukuru wale waliofika katika hija ya maadhimisho ya Jubilei ya Matumaini 2025. Kardinali alifikisha ukaribisho na ukaribu wa Papa Leo XIV, na kusema kuwa "ambaye hakika atatuongoza katika njia ya wokovu," huku akikumbuka kusindikizwa kwa miaka hii na Papa Francisko, pia hata kukumbatiwa na Kanisa la Roma, ambalo ni Kanisa la mashahidi.
Kardinali Gugerotti, alisema kuwa Kanisa lao ni Kanisa tukufu ambalo mizizi yake ya Kikristo ilisitawi katika muktadha maalum, ulioangaziwa pia na mateso. "Ni kweli kwamba katika historia yao bado kuna nyakati za mateso makubwa, kutokana na vita, migawanyiko, kutokana na kiburi, lakini Kanisa hilo halina cha kudai isipokuwa haki ya kutenda mema." Kwa kusisitiza zaidi alisema kuwa "Mkristo hawezi kuishi bila upendo - hivyo basi aliotoa ombi la "kuweza kuitekeleza Ethiopia na Eritrea." Jubilei hii ni ishara ya matumaini, kwa sababu mahali ambapo mtu anasali, kama walivyofanya hapo, kuna Bwana na Mungu yupo, na maisha hustawi. Makanisa ya Kikatoliki ya Ethiopia na Eritrea yameundwa kisheria kama Makanisa makuu juu ya Shiria kamili ambayo ni ya utamaduni wa Aleksandria na yanafanana na liturujia ya ghe'ez kwa pamoja.
Mjini Roma kukiwa na, mapadre wa baadaye wa Kanisa la Ethiopia na Kanisa la Eritrea wanafunzwa katika Chuo cha Kipapa cha Ethiopia. Hali ya kiroho ya Makanisa haya ina mizizi ya kina kibiblia, kuanzia historia ya malkia wa Sheba, aliyevutwa na hekima ya Mfalme Sulemani, iliyosimuliwa katika Kitabu cha Wafalme (1 Wafalme 10) na Mambo ya Nyakati (2 Mambo ya Nyakati 9), na ya mwanawe Menelik, ambaye alikuja kuwa mrithi wa kiti cha Axum, hadi tukio la shemasi Filipo lililosimuliwa na kitabu cha Matendo ya Mitume, kuhusiana na mkutano na afisa wa Malkia Candace.