Tafuta

2025.05.15 Papa Leone XIII alichapisha Waraka wa Rerum Novarum 15 Mei 1891. 2025.05.15 Papa Leone XIII alichapisha Waraka wa Rerum Novarum 15 Mei 1891. 

Kumbukizi ya Waraka wa Rerum Novarum ya Papa Leo XIII:Waraka muhimu wa kijamii

Imepita miaka 134 tangu kuchapishwa kwa Hati ya “Rerum Novarum,”hati ya Papa Leo XIII iliyochapishwa tarehe 15 Mei 1891.Hati hiyo ifuatiwa hata nyingine.Muda mfupi baada ya uchaguzi,Papa Prevost alisisitiza kuwa:“Kanisa,kwa kuchota urithi wa Mafundisho ya kijamii,limealikwa kujibu mapinduzi mengine ya viwanda na zaidi changamoto za maendeleo ya Akili Nunde.”

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Papa Leone XIII, na Waraka wake wa  Rerum Novarum aliouchapisha kunako tarehe 15 Mei 1891 alikabiliana na masuala ya kijamii katika muktadha wa mapinduzi makubwa ya kwanza ya viwanda; na leo hii Kanisa litoa fursa kwa wote urithi wa mafundisho jamii ya Kanisa ili kuweza kujibu mapinduzi mengine ya viwanda kaìsi ya kuongezeka kwa Akili Nunde, ambayo inapelekea changamoto mpya kwa ajili ya ulinzi na utetezi wa hadhi ya binadamu, haki na  kazi.  Baba Mtakatifu Leo XIV mnamo tarehe 10 Mei 2025 akikutana na Baraza la Makardinali, alielezea kwa ufasaha, uchaguzi wake wa jina la Leone XIV. Njia aliyoelekeza kwa namna hiyo,  ni ile ya Mafundisho jamii ya Kanisa, na kuendelea hata katika nyakati hizi zinazotawaliwa na kuyumba kwa uchumi na changamoto nyingine mpya.

Papa Leo XIV akizungumza na Makardinali
Papa Leo XIV akizungumza na Makardinali   (@Vatican Media)

Kwa mtazamo wa sasa wa Hati ya Rerum Novarumu ya kipindi cha mwisho wa karne ya 19, ulimwenguni na Kanisa, ni moja ya misingi ambayo ni kiungo cha kijamii.  Kusoma kwa upya waraka huu wa Papa Pecci,(Papa Leo XIII) uliolenga hali ya umati wa watu wanaofanya kazi, na kuweka tafakari hizo katika muktadha wa sasa, mtu anaweza kutayarisha aina ya “Rerum digitalium",Rerumu ya kidijitali yaani kwa usomaji upya wa mambo ya kidijitali: katika njia iliyofuatiliwa na Papa Leo XIII, mtu anaweza kiukweli kuzingatia suala la kazi na haki za wafanyakazi kwa kuzingatia mabadiliko makubwa yanayoletwa na teknolojia mpya. Waraka wa Papa Pecci, ambamo ujumbe wa Kikristo unakutana na usasa, ni andiko ambalo pia linazungumza na wanaume na wanawake wa siku hizi kwa maisha ya ulimwengu ujao.

Papa Leo na Makardinali
Papa Leo na Makardinali   (@Vatican Media)

Kwa njia hiyo Waraka wa Rerum Novarum ulitangazwa hasa miaka 134 iliyopita,  lakini  pia ni ujumbe wake unaovuka miongo na kizingiti cha milenia ya tatu. “Haiwezekani kuelewa na kutathmini mambo ya wakati ipasavyo, ikiwa roho haigusi kwenye maisha mengine, ambayo ni ya milele, na ambayo bila hiyo dhana ya kweli ya wema wa maadili itatoweka, hakika uumbaji wote unakuwa fumbo lisiloweza kuelezeka. Asili yenyewe inayotuelekeza, kwa hiyo, katika Ukristo ni fundisho ambalo msingi mzima wa dini umeegemea kama msingi wake mkuu: yaani, kwamba maisha ya kweli ya mwanadamu ni yale ya ulimwengu ujao.” Maneno haya yaliyoelekezwa na Papa Leo XIII kwa wanaume wa mwishoni mwa karne ya kumi na tisa yanasikika hata katika enzi hii ya kidijitali kwamba: "uwe na wingi wa mali na bidhaa nyingine za kidunia au kama umenyimwa, hii haijalishi chochote kwa furaha ya milele; lakini hhi iwe ni kwa matumizi mazuri au mabaya ya bidhaa hizo, ndiyo muhimu zaidi,” aliandika Papa Leo XIII.

Papa Leo akienda kukutana na makardinali
Papa Leo akienda kukutana na makardinali   (@Vatican Media)

Mapokeo ya Waraka wa kijamii, katika kipindi cha  sasa, kwa hiyo yanaanza  na Rerum Novarum ya Papa Leo XIII, kushuhudia wasiwasi wa Papa wa sasa, katika mazingira tofauti ya kihistoria, kwa masuala ya kijamii na kiuchumi. Waraka huo ulichapishwa  mnamo 1891 unafungua kipindi cha   usasa wa mafundisho ya kijamii ya Kanisa. Hati ya Papa Leo XIII iliingizwa katika muktadha ambao kazi ilichukuliwa kama bidhaa. Ulimwengu wa kazi ulibadilika sana, lakini haki za wafanyakazi bado zinahitaji kulindwa. Miongoni mwa hatari zinazohusiana na teknolojia mpya, na hasa na akili Nunde,  kuna hata zile za aina mpya za utumwa na unyonyaji mamboleo. Kando ya vivuli, pia kuna taa nyingi zinazohusishwa na fursa ambazo enzi hii ya dijitali inaweza kutoa kwa familia nzima ya wanadamu na hasa, kwa vizazi vipya. Waraka wa Rerum Novarum unasisitiza sababu ya ubaguzi kuwa: ni matumizi mazuri au mabaya ya bidhaa. Kigezo hiki ni sawa kwa mbinu ya kufuatwa leo hii katika matumizi ya teknolojia ya kidijitali. Papa Leo XIII pia aliandika kwamba watu wote wanaunganishwa na kifungo cha Udugu Mtakatifu.

Kuishi udugu kunamaanisha kuelewa kwamba "bidhaa za asili na neema ni urithi wa kawaida wa wanadamu. Ikiwa wote ni watoto, wao pia ni warithi: Warithi wa Mungu na warithi pamoja na Yesu Kristo (Rm 8:17). Hii ndiyo kanuni bora za haki na wajibu Iliyomozo katika Injili zote,"alisisitiza Papa Leo XIII. Ni wazo lile lile lililooneshwa na Hayati Papa Francisko katika Waraka wa la Fratelli tutti (yaami Wote ni Ndugu au lile la Udugu wa kibinadamu la huko Abu dhabi. Kama Papa Leo XIV alivyosema alipokutana na Makardinali tarehe 10 Mei 2025, kuwa “Injili lazima itusukume kutafuta kwa moyo wa kweli ukweli, haki, amani na udugu.” Katika waraka wa Rerum Novarum, Papa Leo XIII aliakisi mazingira magumu ya kazi ya wafanyakazi wa viwandani. “Si haki wala si kibinadamu, kudai kutoka kwa mwanadamu kazi nyingi kiasi kwamba akili yake inakuwa kiziwi na uchovu mwingi na mwili wake unadhoofika. Kama asili yake, kwa hivyo shughuli ya mwanadamu ina mipaka na imezingirwa ndani ya mipaka iliyowekwa vizuri, ambayo hawezi kwenda. Zoezi na utumie kuboresha, kwa masharti, hata hivyo, kwamba mara kwa mara inasimamishwa ili kutoa nafasi ya kupumzika. Kwa hiyo, kazi haipaswi kurefushwa zaidi ya mipaka inayoruhusiwa na nguvu za mtu.”

Papa Leo XIV
Papa Leo XIV   (@Vatican Media)

Suala jingine lililopo katika waraka wa 1891 ni lile la elimu katika kuweka akiba. “Mfanyakazi anapopokea mshahara wa kutosha kujitunza yeye na familia yake katika starehe fulani, ikiwa ana hekima, kwa kawaida atafikiria kuweka akiba.” Hizi ni tafakari za sasa zinazopaswa kusomwa tena hata katika wakati wetu, mara nyingi huwekwa alama na mipaka ambayo si mara zote hufafanuliwa vizuri kati ya shughuli za kazi na nafasi ya maisha ya kibinafsi. Hata kaulimbiu ya kuweka akiba, inayoonekana kama chombo chenye uwezo wa kusaidia familia, ni ya sasa sana, na si ya kandoni kwa sababu ni suala la kutoa thamani sahihi ya mshahara, na ambayo leo hii inazidi kushambuliwa na matumizi yasiyo na mipaka.

Mada kuu ya Waraka wa Rerum Novarum ni ile ya kuanzishwa kwa utaratibu wa kijamii wa haki. Katika sehemu ya mwisho, njia ya kuchukua imeoneshwa, ile ya upendo. "Kila mtu afanye sehemu yake na sio kuchelewesha, kwa sababu kuchelewa kunaweza kufanya iwe ngumu zaidi kuponya uovu ambao tayari ni mbaya. Acha serikali zifanye kazi kwa sheria nzuri na hatua za busara; waache mabepari na wakubwa daima wazingatie wajibu wao; waache wafanya kazi, ambao wana nia ya moja kwa moja, wafanye, ndani ya mipaka ya haki, wanachoweza. Kwa upande wa Kanisa, halitawahi na kwa njia yoyote kuruhusu kazi yake kukosa. Wokovu unaotakiwa lazima hasa uwe tunda la kumiminiwa kwa upendo; tunamaanisha upendo wa Kikristo unaojumuisha Injili nzima,” aliandika Papa Leo XIII.  Njia ya upendo ni njia kuu hata katika milenia ya tatu. Katika enzi ya kidijitali, pamoja na mantiki ya kasi za kidijitali, kipengele cha binadamu kinasalia kuwa muhimu ili kuruhusu familia ya binadamu kutopuuza pumzi ya mshikamano.

Papa Leo XIV
Papa Leo XIV   (@Vatican Media)

Kanisa hata hivyo haliachi kutoa sauti yake kwenye kujipyaisha kwa mfano wa enzi ya kisasa, na linahimiza kila mtu kufanya kila awezalo ili kuthibitisha ustaarabu wa kweli unaolenga kutafuta maendeleo fungamani na kuunga mkono wa binadamu. Msingi wa Fundisho la kijamii la Kanisa unaohusishwa kwa karibu na Waraka wa Rerum Novarum wa Papa Leo XIII ni barua ya Hati ya ‘Quadragesimo Anno ya Papa Pio XI’, iliyotangazwa mnamo tarehe 15  Mei 1931, katika ukumbusho wa miaka  40 ya Waraka wa Rerum Novarum, ambayo inafaa katika muktadha wa kihistoria ulioakisiwa sana na mzozo mkubwa wa Wall Street wa 1929 ambao ulitikisa ulimwengu wa viwanda na sio Amerika tu bali kwingineko. Katika hati hiyo, maandishi ya Papa Leo XIII yanafafanuliwa kama "magna carta" ya utaratibu wa kijamii.

Papa Pio XI aliakisi kwanza kipindi cha Rerum Novarum: "kuelekea mwisho wa karne ya 19, mfumo mpya wa kiuchumi ulioletwa mapema na ongezeko jipya la tasnia, aliandika Papa huku akitafakari juu ya matukio ambayo kwa kiasi fulani yalihusikana yanahusika na wakati wetu ambapo ilifika mahali ambapo jamii karibu katika mataifa yote ilionekana kugawanywa sana katika tabaka mbili: mmoja, mdogo kwa idadi, aliyefurahia karibu starehe zote na mwingine, akijumuisha umati mkubwa wa wafanyakazi waliokandamizwa na uhaba wa uharibifu. Maandishi ya Papa Ratti yanaonya dhidi ya kile kinachofafanuliwa kuwa ubeberu wa kimataifa wa pesa na yanaeleza uharibifu wa mfumo ambao fedha hutawala uchumi na uchumi halisi. Hali inayofanana sana na ile tunayoishi leo hii katika ulimemwengu wote.

Papa Leo XIV
Papa Leo XIV   (@Vatican Media)

Katika kumbukumbu ya miaka 50 ya “Rerum Novarum”, Papa Pio XII katika ujumbe wake wa Radio kwa ajili ya Pentekoste 1941, katika wakati uliogubikwa na mchezo wa kutisha wa vita, kama ilivyo hata leo hii, kati ya mambo mengine Papa alisisitiza kwamba kutoka katika barua ya Waraka wa Papa Leo XIII ilichipuka “chanzo cha roho ya kijamii yenye nguvu, ya dhati, isiyopendezwa. Chanzo ambacho, ikiwa leo hii kinaweza kufunikwa na maporomoko ya matukio tofauti na yenye nguvu zaidi, kesho, mara magofu ya kimbunga hiki yameondolewa, wakati kazi ya kujenga upya utaratibu mpya wa kijamii, unaosihiwa kuwa unastahili Mungu na mwanadamu, itaanza, itaingiza msukumo mpya wa nguvu na wimbi jipya la kustawi na kukua katika maua yote ya utamaduni wa mwanadamu. Waraka wa Rerum Novarum, uliowakaribia watu, ambao uliwakumbatia kwa heshima na upendo - aliongeza Pius XII - ulipenya mioyo na akili za wafanyakazi na kuingiza hisia za Kikristo na heshima ya raia." Katika ujumbe wake wa Radio wa mwaka 1942, katika mkesha wa Noeli Papa Pio XII pia alisisitiza kwamba Kanisa halisiti kutafakari matokeo ya vitendo yanayotokana na uadilifu wa kazi.

Papa Leo XIV kwa salamu Malkia
Papa Leo XIV kwa salamu Malkia   (@Vatican Media)
15 Mei 2025, 15:13