Tafuta

2025.05.14: Maonesho ya Kimataifa ya Vitabu 2025, Torino,Italia. 2025.05.14: Maonesho ya Kimataifa ya Vitabu 2025, Torino,Italia. 

Maonesho ya Vitabu ya Torino,mikutano ya Nyumba ya Uchapishaji ya Vatican!

Jukumu la Wakristo katika ulimwengu wa leo,changamoto ya matumaini na kazi ambayo haijachapishwa ya Padre Giussani,kumbukumbu ya Papa Benedikto XVI.

Vatican News

Mwaka huu 2025, Nyumba ya Uchapishaji wa Vitabu ya Vatican (LEV) inashiriki katika matukio matatu katika Ukumbi wa Kimataifa wa Vitabu huko Torino nchini Italia kwa tukio linalooanza kuanzia Alhamisi tarehe 15 hadi 19 Mei 2025.  Kwa mujibu wa Lorenzo Fazzini, mhusika mkuu wa wahariri wa Duka la uchapishaji wa Vitabu la Vatican(LEV), alifafanua kuwa “umuhimu wa kukabiliana na majadiliano ya kujenga kati ya waamini na wasioamini,  mada hii iligusiwa mara nyingi na Hayati Papa Francisko, kama ilivyoelezwa katika mikutano yetu na Sandro Veronesi, Kardinali De Kesel, Matteo Lancini na Massimo Camisasca.” Kwa kuongezea: “Mada zilizopendekezwa zinashughulikiwa na watu mashuhuri wa kimataifa ambao wanapanua mtazamo wetu, na ndiyo mwaliko wa kutafakari, kwa matumaini na mtazamo wa mbele, kuhusu Jukumu la wakristo katika mazingira ya kimataifa ya mivutano na migawanyiko.”

Maonesho ya kimataifa ya vitabu huko Torino Italia
Maonesho ya kimataifa ya vitabu huko Torino Italia   (ANSA)

Tukio hilo linalofanyika huko mjini Lingotto, ambapo LEV ipo katika maonyesho ya kimataifa katika kibanda cha 2 stendi ya L05, pia itakuwa fursa ya kuwasilisha matoleo yake mapya ya wahariri kwa umma, ikiwa ni pamoja na maandiko ya hivi karibuni ya Papa Francisko, kitabu cha mahubiri cha Benedikto XVI na kitabu ambacho hakijachapishwa na Padre Luigi Giussani, mwalimu na mwanzilishi wa Harakati za kikanisa ya “Comunione e Liberazione” yaani, “Umoja na Ukombozi.”

Tukio la kwanza linafanyka Alhamisi, tarehe 15 Mei 2025 saa 9:15 alasiri katika (Uwanja wa Oval – Ukumbi wa urujuani) kuhusu mada “Je, inawezekana kuwa na matumaini? Mafundisho ya Padre Giussani na wakati wetu" katika fursa ya kitabu cha kukutana kinachohusu Matumaini kilichohaririwa na Davide Prosperi, chapsho la kwanza kuhusu kuhani mwalimu aliyewafutia maelfu ya vijana. Wazungumzaji watajumuisha Paola Bergamini, mwandishi wa habari wa Tracce ya kila mwezi, Askofu Massimo Camisasca,mstaafu wa Reggio Emilia-Guastalla, na Matteo Lancini, mwanasaikolojia na rais wa Mfuko wa Minotauro huko Milan.

Ufunguzi wa Monyesho kimataifa ya vitabu
Ufunguzi wa Monyesho kimataifa ya vitabu   (ANSA)

Ijumaa, tarehe 16 Mei 2025 saa 11:15 jioni kutakuwa na mkutano muhimu wa kutafakari juu ya mustakabali wa Kanisa katika enzi ya kisasa. Kardinali Jozef De Kesel, Askofu mkuu mstaafu wa Malines-Brussels, mwandishi wa kitabu "Cristiani in un mondo che non lo è più", yaani Wakristo katika ulimwengu usio kuwa ulimwengu" na mwandishi Sandro Veronesi, watajadili mada: "Kama Wakristo katika ulimwengu ambao sio (tena) wa Kikristo". Mkutano huo utasimamiwa na Alessandro Zaccuri, mwandishi wa habari wa Italia na mwandishi wa riwaya.

Jumamosi, Mei 17, saa 7:45 machana (Banda 1 – katika ukumbi wa Ambra), mwimbaji-mtunzi wa nyimbo Giovanni Lindo Ferretti, Padre Federico Lombardi, Msemaji mkuu wa zamani wa karibu na Papa Benedikto XVI, pia Msemaji wa Ofisi ya Vyombo vya Habari Vatican na rais wa sasa wa Mfuko wa Vatican wa Joseph Ratzinger-Benedikto XVI na Dk. Andrea Tornielli, Mwariri Mkuu wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano, katika fursa ya uchapishaji wa Hati “ Bwana anatushika mikono kinachokusanya mahubiri yaliyotolewa na Papa Benedikto XVI wakati wa upapa wake na Papa Mstaafu.

Maonesho ya Kimataifa ya vitabu huko Lingoto, Torino
Maonesho ya Kimataifa ya vitabu huko Lingoto, Torino   (ANSA)
Vitabu Torino katika Manyesho ya kimataifa
15 Mei 2025, 11:37