Tafuta

Askofu Osório Afonso Citora wa Jimbo Katoliki la Quelimane, Msumbiji Askofu Osório Afonso Citora wa Jimbo Katoliki la Quelimane, Msumbiji 

Askofu Osório Citora Afonso, I.M.C Jimbo Katoliki Quelimane, Msumbiji

Baba Mtakatifu Leo XIV amemteuwa Askofu msaidizi Osório Citora Afonso, kutoka Shirika la Wamisionari wa Consolata, I.M.C., wa Jimbo kuu la Maputo, Msumbiji, kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Quelimane nchini Msumbiji. Kabla ya uteuzi huu Askofu Osório Citora Afonso, I.M.C. alikuwa ni Askofu msaidizi wa Jimbo kuu la Maputo, Msumbiji. Itakumbukwa kwamba, Askofu Osório Citora Afonso, I.M.C., alizaliwa tarehe 6 Mei 1972, Jimbo kuu la Nampula.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV amemteuwa Askofu msaidizi Osório Citora Afonso, kutoka Shirika la Wamisionari wa Consolata, I.M.C., wa Jimbo kuu la Maputo, Msumbiji, kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Quelimane nchini Msumbiji. Kabla ya uteuzi huu Askofu Osório Citora Afonso, I.M.C. alikuwa ni Askofu msaidizi wa Jimbo kuu la Maputo, Msumbiji. Itakumbukwa kwamba, Askofu Osório Citora Afonso, I.M.C., alizaliwa tarehe 6 Mei 1972, Jimbo kuu la Nampula.

Askofu Osorio Citora Afonso wa Jimbo Katoliki Quelimane, Msumbiji
Askofu Osorio Citora Afonso wa Jimbo Katoliki Quelimane, Msumbiji

Baada ya masomo na majiundo yake ya Kipadre na Kitawa, tarehe 17 Juni 2001 akaweka nadhiri zake za daima na baadaye, tarehe 3 Novemba 2003 akapewa Daraja takatifu ya Upadre. Kunako mwaka 2017 akateuliwa kuwa ni Afisa katika Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu. Tarehe 21 Septemba 2023, Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo kuu la Maputo, Msumbiji na kuwekwa wakfu kuwa Askofu tarehe 28 Januari 2024. Na ilipofika tarehe 25 Julai 2025, Baba Mtakatifu Leo XIV akamteuwa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Quelimane nchini Msumbiji.

Uteuzi Msumbiji
25 Julai 2025, 16:04