Vatican na Azerbaigjan kutia saini ya makubaliano juu ya mazungumzo ya kidini
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Safari ndefu, iliyosimikwa katika Mtaguso wa Pili wa Vatican, iliyoashiriwa kwa miaka mingi na mazungumzo na kuheshimiana, iliyofikia kilele cha Makubaliano ya Nchi Mbili kunako 2011 na sasa iliyoboreshwa na Mkataba zaidi wa Maelewano juu ya mazungumzo ya kidini. Katika salamu zake kwa viongozi wa Kiazabajani waliohudhuria sherehe za Jumatatu tartehe 28 Julai 2025, mjini Vatican, Kardinali George Koovakad, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Majadiliano ya kidini alitoa muhtasari wa njia inayofuatwa na Vatican na Jamhuri ya Azabajani katika kutia saini hati kuhusu "eneo muhimu" kama vile mazungumzo kati ya imani tofauti. Kwa upande wa Kardinali, hati hiyo inawakilisha "ishara wazi ya hamu ya pamoja ya kuendelea kufanya kazi pamoja kwa ajili ya malezi muhimu ya kila mtu, kama waamini na kama raia."
Vatican na Azerbaijan zimeimarisha uhusiano
Zaidi ya hayo, Kardinali Koovakad alisema, “ miongo ya hivi karibuni, Vatican na Jamhuri ya Azerbaijan zimeonesha nia ya pamoja ya kuendeleza na kuimarisha uhusiano wao kwa mfululizo wa hatua zilizohimizwa na alikumbuka Mtakatifu Yohane Paulo II kunako mwaka 2002 na Papa Francisko Oktoba 2016, bila kusahau ziara ya 2008 nchini Azerbaijan ambayo Kardinali Bertone alikuwa msemaji wa Baba Mtakatifu Benedikito XVI. Mkataba uliotiwa saini tarehe 28 Julai 2025 unatokana na makubaliano ya nchi mbili ya Aprili 2011 kati ya Vatican na Jamhuri ya Azerbaijan. Mwakilishi wa wa Vatican alibainisha kwamba, pamoja na kuimarisha mahusiano baina ya nchi hizo mbili na kuliwezesha Kanisa kutekeleza utume wake katika Jamhuri ya Caucasia, limekuwa “chombo chenye thamani kubwa cha kukuza kanuni ya uhuru wa kidini, kinachofumbatwa katika Katiba ya Azerbaijan yenyewe.
Heshima kwa Jumuiya ya kidini walio wachache
Maandishi, yanabainisha zaidi, ambayo yanaonesha "heshima kwa jumuiya ya kidini ya wachache na jinsi Wakristo na Waislamu wanaweza kuishi pamoja kwa maelewano." Kardinali Koovakad alisisitiza umuhimu wa Papa Francisko katika miaka ya hivi karibuni juu ya mazungumzo ya kidini, ambayo yanaeleweka kama kichocheo cha "utamaduni wa amani," kwa roho ya Waraka wa Udugu wa Kibinadamu, na hata kabla ya hapo, kwenye Mtaguso wa II wa Vatican kwenye Tamko la Nostra Aetate juu ya Uhuru wa Kidini, ambalo litaadhimisha miaka 60 Oktoba ijayo. Tangu 1965, Kardinali anabainisha, "maeneo mapya ya kujitolea kwa pamoja yameibuka, kama vile hamu ya kutunza na kulinda mazingira na haja ya matumizi ya kimaadili ya akili ya bandia.