Vatican:Biashara isiyo ya haki inakuza umaskini,lazima ikomeshwe!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Tarehe 6 Agosti 2025 lilifanyika Kongamano la Tatu la Kimataifa la la Nchi Zinazoendelea,Nchi sizizofungwa na Bandari na Nchi Zinazoendelea za Visiwa Vidogo, lililofanyika huko Awaza, Turkmenistan. Katika tukio hilo pamoja na wengine walioshiriki alikuwa ni mwakilishi wa Vatican, Monsinyo Arnaud du Cheyron de Beaumont ambaye alitoa hotuba yake. Akianza alisema kuwa: “Mkutano huu unaipa jumuiya ya kimataifa fursa ya kuthibitisha uungaji mkono wake kwa la Nchi Zinazoendelea,Nchi sizizofungwa na Bandari na Nchi Zinazoendelea za Visiwa Vidogo (LLDC) na kuzipa msaada wa muda mrefu unaoonekana unaokuza maendeleo fungamani ya binadamu. Kupitishwa kwa Mpango wa Utendaji wa Awaza ni hatua muhimu katika suala hili, lakini utekelezaji wake lazima udumishwe na kuungwa mkono na utashi madhubuti wa kisiasa.”
Nchi maskini kuendelea kuathirika na mabadiliko ya Tabianchi
Kwa njia hiyo Mwakilishi wa Vatican alisisitiza kuwa Nchi Zinazoendelea,Nchi sizizofungwa na Bandari na Nchi Zinazoendelea za Visiwa Vidogo (LLDC) ingawa ni tofauti katika mazingira yao ya kijiografia, kiutamaduni na kiuchumi, zinakabiliwa na changamoto sawa za kimfumo, ikiwa ni pamoja na mizigo ya madeni isiyo endelevu, gharama kubwa za usafiri na kuathirika kwa mabadiliko ya tabianchi na majanga kutoka nje.” Hata hivyo, kwa kukazia zaidi “ umaskini unasalia kuwa changamoto kubwa na ya dharura kwa LLDCs. Kwa njia hiyo katika LLDC nyingi, umaskini umeenea na una sura nyingi. Sio tu kwamba inazuia matarajio ya kiuchumi ya la Nchi Zinazoendelea,Nchi sizizofungwa na Bandari na Nchi Zinazoendelea za Visiwa Vidogo(LLDC), lakini pia unadhoofisha utu aliopewa na Mungu kwa kila mwanadamu kwa kuwanyima mamilioni ya mahitaji yao ya kimsingi.” Umaskini umekithiri hasa katika maeneo ya vijijini, ambako watu mara nyingi wanakosa huduma muhimu na fursa. Umaskini unatokana na aina mbalimbali za kunyimwa utamaduni na kunyimwa haki za kitamaduni. Elimu na maendeleo ya watu binafsi lazima iwe jambo kuu la hatua zote za kijamii.
Sheria ya Biashara
Mwakilishi wa Vatican aliendela: "Umaskini hauepukiki; ni matokeo ya miundo isiyo ya haki na uchaguzi wa sera, na kwa hiyo inaweza na ni lazima kushindwa. Kizuizi kimoja cha kimfumo cha kutokomeza umaskini kwa la Nchi Zinazoendelea,Nchi sizizofungwa na Bandari na Nchi Zinazoendelea za Visiwa Vidogo(LLDC ) nyingi ni biashara isiyo ya haki. "Biashara ya kimataifa - ikiwa ina mwelekeo mzuri - inakuza maendeleo na inaweza kuunda uwezekano mpya wa ajira na kutoa rasilimali muhimu." Hata hivyo, ili hili lifanyike, biashara lazima iundwe na matakwa ya haki na mshikamano. Biashara lazima ianzishwe juu ya kanuni ya hatima ya ulimwengu ya bidhaa, ambayo ni, "kwa kila mtu na kwa watu wote hali zinazohitajika kwa maendeleo kamili, ili kila mtu aweze kuchangia kufanya kuwa Ulimwengu wa kibinadamu zaidi." Nchi zilizoadhibiwa na sheria zisizo za haki za biashara ya kimataifa mara nyingi zinakabiliwa na uhaba wa mtaji, ambao mara kwa mara unachangiwa na mzigo wa deni la nje. Katika hali kama hizi, unyonyaji mkubwa na wa kupindukia wa mazingira ni karibu hauwezi kuepukika, na husababisha njaa na umaskini.
Vatican kuendeleza huduma ya upatanisho
Zaidi ya hayo, alisema "kukuza maendeleo hakutakuwa na ufanisi ikiwa biashara itapunguzwa kwa ubadilishanaji wa bidhaa. Ni muhimu kuhimiza nchi zinazoendelea kujitawala kisayansi na kiteknolojia kwa kukuza ubadilishanaji wa maarifa ya kisayansi na kiteknolojia na uhamishaji wa teknolojia. Binadamu lazima abakie katikati ya mikakati yote ya maendeleo. Biashara na ukuaji wa uchumi sio mwisho wao wenyewe bali ni njia za kukuza maendeleo fungamani ya binadamu ya kila mtu na maendeleo ya manufaa kwa wote. Kama vile Papa Leo wa XIV alivyothibitisha kwamba: “Vatican itaendelea katika huduma ya mapatano kati ya watu siku zote na haitachoka kamwe kushirikiana kwa ajili ya manufaa ya familia yote ya mataifa, kwa heshima ya kipekee kwa wanadamu wanaoteseka zaidi […] na pia kanda za mbali ambazo haiwezi kuinuka kutoka kwenye shida yao kwa sababu ya kutojali kwa wale ambao zoezi la mshikamano usioshindwa unapaswa kuwa nembo ya maisha yao.”