Tafuta

Askofu Mkuu Gallagher,Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa azungumza katika (UNGA80) 22-30 Septemba 2025. Askofu Mkuu Gallagher,Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa azungumza katika (UNGA80) 22-30 Septemba 2025.  (ANSA)

Ask.Mkuu Gallagher:Aina zote za ukatili dhidi ya wanawake na wasichana lazima zipigwe vita

Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Mataifa wakati wa Hotuba yake kwenye Juma la Umoja wa Mataifa(UNGA80)katika kuadhimisha miaka 30 baada ya Tamko la Beijing alisema kuwa:"licha ya maendeleo makubwa yaliyotokea kwa miaka hii,ubaguzi katika ajira na vikwazo vya upatikanaji wa elimu na huduma za afya bado viko juu."

Na Sr. Christine Masivo, CPS , - Vatican.

Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa  Vatican wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa, akizungumza Jumatatu, tarehe 22 Septemba 2025, kwenye Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani, wakati wa Mkutano wa Ngazi  za Juu kwenye mkutadha wa Juma la  Baraza la Umoja wa Mataifa(UNGA80), ikiwa pia ni sehemu ya  kuadhimisha miaka 30 ya Mkutano wa Nne wa Dunia wa Wanawake, uliofanyika Beijing Septemba 1995 alisema kuwa:  “Mataifa lazima yajitolee kulinda heshima na utu; suluhisho  za uwongo kama vile utoji mimba lazima zikataliwe. Nchi lazima zitimize ahadi zao ili kuhakikisha usawa wa wanawake na heshima kwa utu wao waliopewa na Mungu.”

Licha ya mafanikio makubwa, utu wa mwanamke bado unakandamizwa

Askofu Mkuu Gallagher alisema kwamba“ licha ya mafanikio makubwa yaliyopatikana kuhusu masuala muhimu na ya dharura kuhusu utu wa wanawake na kufurahia kikamilifu haki zao za kimsingi za binadamu, leo hii kwa kiasi  fulani bado hayajatatuliwa katika  tamko la Beijing na Jukwaa la Utekelezaji, ikiwa ni pamoja na viwango vya juu vya umaskini uliokithiri, vikwazo vya kupata au hata kuwatenga wanawake katika elimu bora, na mishahara ya chini katika wafanyakazi."  Kwa njia hiyo alieleza kwamba masharti haya yote yanazuia mafanikio kamili ya utu sawa wa wanawake na uwezo wao wa kutambua uwezo wao katika nyanja zote za maisha.”

Mwakilishi wa Vatican alisema: Tofauti katika huduma za afya zinaendelea kuathiri wanawake. Ingawa viwango vya vifo vya uzazi vimepungua sana tangu 1990, maendeleo yamekwama katika miaka ya hivi karibuni. Upatikanaji wa huduma ya kabla ya kujifungua na wakunga wenye ujuzi, pamoja na mifumo ya huduma za afya na miundombinu lazima kuongezeka, huku suluhisho za uwongo kama vile utoaji mimba kukataliwa. Kwa hakika, kulinda haki ya kuishi ni muhimu, kwani ndio msingi wa haki nyingine zote za kimsingi. Usawa kwa wanawake hauwezi kufikiwa isipokuwa "heshima ya kila mtu, haswa aliye dhaifu na aliye hatarini zaidi, kutoka kwa watoto ambao hawajazaliwa hadi wazee  inaheshimiwa.

Aina yoyote ya ukatili haikubaliki

Vatican  pia inaelezea hofu kubwa juu ya kuenea kwa "unyanyasaji dhidi ya wanawake na wasichana, dharau kwa utu wao na dhuluma kubwa, iwe nyumbani, wakati wa migogoro, au wakati wa biashara haramu. Unyanyasaji huu pia unazidishwa na teknolojia. Lakini vurugu, pia inajumuisha mazoea ya kuchagua ngono kabla ya kuzaa na mauaji ya watoto wachanga. Vitendo hivi, vimelaaniwa katika tamko la  Beijing na Jukwa la Utekelezaji, linaendelea kusababisha vifo vya mamilioni ya wasichana waliopotea kila mwaka. Aina yoyote ya ukatili dhidi ya wanawake na wasichana haikubaliki na lazima ipigwe vita,” alisisitiza Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Mataifa.

Katibu wa Vatican wa mahusiano na chi alisema: Kwa kusikitisha, teknolojia pia inatumiwa kuzidisha aina fulani za unyanyasaji na jeuri. Hata hivyo, unyanyasaji hauishii tu katika unyonyaji na usafirishaji haramu wa kingono bali pia ni pamoja na desturi za uteuzi wa ngono kabla ya kuzaa na mauaji ya watoto wachanga. Vitendo hivi, vilivyolaaniwa katika Azimio la Beijing na Jukwaa la Utekelezaji, vinaendelea kusababisha matokeo ya vifo vya mamilioni ya "wasichana waliopotea" kila mwaka. Aina yoyote ya ukatili dhidi ya wanawake na wasichana haikubaliki na lazima ipigwe vita.

Ukosefu wa usawa wa kiafya

Kwa mujibu wa Mwakilishi wa Vatican alisisitiza kwamba “mbali na unyanyasaji wa kimwili, wanawake bado ni waathirika wa kukosekana kwa usawa wa huduma za afya. Upungufu uliothibitishwa wa viwango vya vifo vya uzazi haujalinganishwa na maendeleo makubwa katika eneo hili. Upatikanaji wa huduma ya kabla ya kujifungua na wafanyakazi wa afya waliohitimu, pamoja na mifumo ya afya na miundombinu, lazima iongezwe, wakati ufumbuzi wa uongo kama vile uavyaji mimba lazima kukataliwa. Ulinzi wa haki ya kuishi ni muhimu, kwani ndio msingi wa haki zingine zote za kimsingi." Kwa kuhitimisha, Askfofu Mkuu Gallagher alikikubali kwamba masuala muhimu yaliyotolewa na Beijing kwa ajili ya wanawake yamepuuzwa, na kuelezea  matumaini yake kwamba jumuiya ya kimataifa haitazingatia masuala ya mgawanyiko ambayo si lazima kuwa na manufaa kwa wanawake."

Askofu Mkuu Gallagher alisema: Wasiwasi wa kimsingi wa Tamko  la Beijing na Jukwaa la Utekelezaji, ambalo linashughulikia mahitaji ya wanawake katika umaskini, mikakati ya maendeleo, kusoma na kuandika na elimu, kukomesha unyanyasaji dhidi ya wanawake na wasichana, utamaduni wa amani, na upatikanaji wa ajira, ardhi, mitaji na teknolojia, bado limepuuzwa. Ni matumaini ya Baraza Kuu kwamba badala ya kuzingatia masuala ya mgawanyiko ambayo si lazima yawe na manufaa kwa wanawake, Mataifa yanatimiza ahadi zao ili kuhakikisha usawa kwa wanawake, na kuheshimu utu wao waliopewa na Mungu. 

Gallagher na Mongela
24 Septemba 2025, 16:35