Tafuta

2025.09.25 Mazishi ya Askofu Mkuu Novatus Rugambwa. 2025.09.25 Mazishi ya Askofu Mkuu Novatus Rugambwa.   (@VATICAN MEDIA)

Kard,Parolin,Ask.Mkuu Rugambwa alikuwa mwadilifu na ukweli alioutangaza

Alikabiliana kwa imani yake na mfano wa upendo katika ugonjwa,kwa kufanya hata katika fursa hii kujibakidhi kwa mapenzi yake na kwa ujenzo wa watu wa Mungu,hasa kwa wale wote ambao kwa imani walimuuguza na kumfuatilia hadi mwisho wa maisha yake hapa duniani.Alikuwa mwadilifu wa maisha na ushuhuda wa mamlaka na uaminifu wa ukweli ambao aliutangaza na kuuishi.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Alhamisi tarehe 25 Septemba 2025, Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican, aliongoza ibada ya Misa kwa ajili ya kumuaga kwenye makao ya Milele, Askofu Mkuu Novatus Rugambwa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, akisaidia na Askofu Mkuu Msaidizi wa Vatican  Edigar Pena Parra, Maaskofu wakuu wengine, maaskofu na mapadre. Katika mahubiri Kardinali Parolin yake alisema "tunaadhimisha misa hii kwa ajili ya mazishi ya Askofu Mkuu Novatus Rugambwa ambaye tarehe 16 Septemba iliyopita aliaga dunia baada ya ugonjwa wa muda mrefu, Bwana alimwita kwake.  Kardinali Parolin aliendelea kueleza wasifu wake kuwa,  alizaliwa huko Bukoba nchini Tanzania kunako tarehe 8 Oktoba 1957, na baada ya kupewa daraja la upadre kunako mwaka 1986, tangu 1991 kwa miaka mingi alitoa huduma yake katika Diplomasia ya Kiti Kitakatifu.

Kardinali Parolin wakati wa Mahubiri
Kardinali Parolin wakati wa Mahubiri   (@VATICAN MEDIA)

Shughuli zake za kwanza zilifanyika huko Amerika ya Kusini, Afrika, Asia na Oceania. Baada ya kipindi, kama Katibu Mkuu wa Baraza la Kipapa la Uchungaji wa Wahamiaji na wasafiri  kuanzia 2007 hadi 20210, Papa Benedikto XIV alimteua kuwa Askofu Mkuu na Balozi wa Vatican huko Angola na Sao Tome na Prince.  Baadaye alikuwa Mwakilishi wa Kipapa wa Honduras, Balozi wa Vatican wa New Zeland, Mwakilishi wa Kitume wa Oceania ya  Pasifiki  na visiwa vyake  mbali mbali vya Ghuba hiyo.

Misa ya mazishi ya Askofu Mkuu Novatus Rugambwa
Misa ya mazishi ya Askofu Mkuu Novatus Rugambwa   (@VATICAN MEDIA)

Baada ya miaka mingi ya shughuli zake, lakini "Bwana alimwomba mchango wa Kanisa, ule wa mateso kuyatoa katika muungano na Kristo kwa ajili ya wokovu wa ndugu. Alikabiliana kwa imani yake na mfano wa upendo katika ugonjwa, kwa kufanya hata katika fursa hii, kujibakidhi kwa mapenzi yake na kwa ujenzi  wa Watu wa Mungu, hasa  wale wote ambao kwa imani walimuuguza na kumfuatilia hadi mwisho wa maisha yake  hapa duniani."

Misa ya Mazishi ya Askofu Mkuu Novatus Rugambwa
Misa ya Mazishi ya Askofu Mkuu Novatus Rugambwa   (@VATICAN MEDIA)

Kardinali aliendelea kusema kuwa alituachia ushuhuda ambao unaweza kutusaidia kutafakari juu ya kile ambacho Mtakatifu Paulo aliandikia Wakristo wa Roma na leo hii Liturujia inapendekeza kwa umakini na sala kwamba: "Kwa maana nayahesabu mateso ya wakati huu wa sasa kuwa si kitu kama utukufu ule utakaofunuliwa kwetu."(Rm 8,18). Kwa upande wa Askofu Mkuu Rugambwa imefika siku ya uonesho mkubwa huu. Anajiwakilisha mbele ya Mungu na sadaka  kubwa aliyotimiza, tunda awali ya yote la neema yake, na kwa hiyo zawadi ya Bwana, lakini kwa hakika hata ushuhuda wa ukarimu, kwa namna aliyojikita nayo ya huduma ambayo iliendana bila kujibakia kwa zawadi alizozipokea .

Misa ya mazishi ya Askofu Mkuu Rugambwa
Misa ya mazishi ya Askofu Mkuu Rugambwa   (@VATICAN MEDIA)

Kardinali Parolin alisisitiza  kwamba kwa kusikiliza maneno haya, hatuwezi kutofikiria mfano ambao ametuachia wa upendo Monsinyo Novatus. Kilio cha Roho: "Abba Baba" (Rm, 8,15), kwa hakika kilipata ndani ya moyo wake, nguvu kubwa yenye mwitikio wa nguvu,  hadi kujaza maisha yote na yaliyojaa mahusiano na kaka na dada ambao walikutana naye katika safari yake. Diplomasia,  kama  tutujavyo, ni muktadha wa upendo wa kichungaji,  kati ya udharura zaidi na unyeti ambao unahitaji kuuendesha kwa uaminifu wa misingi ya Injili na mafundisho ya Kanisa ndani ya mifumo na mahusiano kati ya Nchi na Watu ambao wanaishi, kwa kuheshimu wote, na wakati huo huo kwa ukarimu shirikishi wa nuru na nguvu ambazo zinakuja kutoka katika imani. "

Wakati wa Usomaji wa Injili
Wakati wa Usomaji wa Injili   (@VATICAN MEDIA)

Kwa Askofu Mkuu Rugambwa, Kardinali Parolin aalibainisha: "alitoa mfano mzuri, kwa uthabiti wake wa maisha ya huruma, busara yake na wakati huo huo kwa uthabiti katika kutetea  misingi ya haki na heshima ya mtu ambayo ni muhimu  kwa ajili ya kuishi kwa amani  na ujenzi, licha ya utofauti, mbali na mipaka ya kitaifa. Kwa usikivu huu na kwa uvumilivu wa ubaba na wasiwasi wa kichungaji alitambua kufuma mahusiano thabiti na ya kujenga."

Wakati wa Baraka
Wakati wa Baraka   (@VATICAN MEDIA)

Kardinali Parolini, kadhalika katika muktadha huo alipenda "kukumbuka sehemu ya pili ya mtindo wake kibinafsi : uadilifu wa maisha aliyokuwa nayo, ya ushuhuda wa mamlaka na uaminifu wa ukweli ambao aliutangaza." Mtakatifu Paulo VI alikuwa anasema kuwa:"mwanadamu wa sasa anasikiliza kwa hiari zaidi mashuhuda kuliko walimu."(Consilium de Laicis,2 oktoba 1974). Ni kweli kwamba mfano mzuri unatosha zaidi ya maneno elfu. Zaidi ya yote Bwana kwa wachungaji wake anaomba,  awali ya yote jitihada na ushuhuda wa maisha matakatifu na ikiwa hicho kinakuwa mfano, basi  kinakuwa sababu kubwa muhimu kwa anayejikita na utume nyeti kama ule wa Mwakilishi wa Kipapa ambao, kando kando ya maandalizi yanayofaa na maalum kwa ngazi  ya kidiplomasia na kisiasa, tabia ya mfano ni muhimu!

Misa ya Mazishi ya Askofu Mkuu Rugambwa
Misa ya Mazishi ya Askofu Mkuu Rugambwa   (@VATICAN MEDIA)

Katibu Mkuu wa Vatican akijikita katika sura ya Injili iliyosomwa kwamba "inatupatika picha kubwa ya "Hukumu ya mwisho (Mt 25, 31-46). Hiyo inatukumbusha kuwa kile ambacho tutakuja kuhukumiwa  mwishoni  mwa mchakato wa maisha yetu hapa duniani, hayatakuwa mafanikio, wala kushindwa, bali upendo ambao tuliutoa kwa kile tulichopokea. Kadhalika aliongeza kusema, kwamba wakati mwingine inaweza kutuogopesha kufikiria jinsi ambavyo Bwana anatuwekea katika mikono yetu wito wake. Faraja peke yake ni  imani ambayo kwamba Yeye hatuachi kamwe, katika jitihada ya kijikabidhi kila wakati na kamili, katika upendo, na kile ambacho upendo  wenyewe, alitupatia Mungu.

Mazishi ya Askofu Mkuu Novatus Rugambwa
Mazishi ya Askofu Mkuu Novatus Rugambwa   (@VATICAN MEDIA)

Unyeti huo kwa sauti ya walio wa mwisho, ambao Askofu Mkuu Rugambwa aliupata kwa moto ulio hai katika moyo wake, sio mapambo ya hiari  ya maisha ya kikristo, bali yapo katika mzizi kama sehemu muafaka wa kukutana na Mungu. Kardinali Parolini kwa njia hiyo alitaka kuhitimisha kwa kutazama tafakari hii kwa maneno ya Mtakatifu Leo Mkuu, Mchungaji, na mtu wa amani: Wale ambao wameelekeza macho yao kwa Mungu  wakitafuta kuhifadhi umoja katika Roho, kwa njia ya dhamana ya amani (Ef 4,3) hawatengenishwi kamwe na sheria ya milele. Wao wanasali  kwa imani ya kweli sala kwamba: "Utakalo na lifanyike duniani na mbinguni.(Rm 8,17)." Kiukweli upendo wa Mungu na upendo wa jirani utamwezesha  kupata zawadi kubwa inayostahili. Hawasikia tena shida, hawataogopa vizingiti au mitego, bali baada ya kumaliza mapambano na mahangiko yote watapumzika katika utulivu wa amani ya Mungu (Sermo XCV,PL 54.465-466).

Kijana Avitus akipewa mkono wa pole na Kardinali Parolin,Katibu Mkuu wa Vatican.
Kijana Avitus akipewa mkono wa pole na Kardinali Parolin,Katibu Mkuu wa Vatican.   (@VATICAN MEDIA)

Na hicho ndicho ambacho kwa  pamoja na familia na wajumbe wote wa majimbo asilia, tunamwombea Monsinyo Novatus, mtumishi mwaminvu katika shamba la Bwana, na hata kwa ajili yetu. Baba wa Mbinguni atupatie kujua daima na kuelewa vema mipango yake ili kutufanya  kuwa katika mikono yake wanaofaa na wanyenyekevu, vyombo vya wokovu wa mmoja kwa wengine, na hivyo kuweza kujikuta  tuko pamoja wote siku moja katika nyumva yake. Amina.

Mazishi ya Askofu Mkuu Novatusi Rugambwa
Mazishi ya Askofu Mkuu Novatusi Rugambwa   (@VATICAN MEDIA)

Mbali na maaskofu, mapadre kutoka sehemu mbali mbali za dunia na hasa alipozaliwa(Bukoba Tanzania) na mahali alipofanyia kazi, kulikuwa na waamini, wengi, na wawakilishi kutoka sehemu mbali mbali. Hawakukosa Uwakilishi kutoka  Ubalozi wa Tanzania nchini Italia ukiongozwa na Balozi Mpya akiwa na watumishi wengine wa Ubalozi huo wa Tanzania.

Askofu Novatus Rugambwa
WAKATI WA MISA YA MAZISHI YA ASKOFU MKUU RUGAMBWA
Mazisihi rugambwa
25 Septemba 2025, 12:01