Semeraro:Kwa Mtakatifu Carlo Acutis kuna mtazamo wa unyenyekevu kwa wadhaifu zaidi
Rosario Capomasi na Angella Rwezaula – Vatican.
Siku tunapoadhimisha Kuzaliwa kwa Bikira Maria, ambaye alifanya unyenyekevu kuwa alama yake kuu, inafaa kumtazama Mtakatifu Carlo Acutis, ambaye alianzisha safari yake yote ya kiroho na ya kibinadamu juu ya unyenyekevu. Kardinali Marcello Semeraro, Mwenyekiti qa Baraza la kipapa la ukuwatangaza Watakatifu ndivyo alianza kusema wakati wa Ibada ya Misa Takatifu ya kutoa Shukrani kwa Mungu kwa kutangazwa Mtakatifu wa kijana huyo na mwezake, Misa iliyandishishwa Jumatatu tarehe 8 Septemba 2025 kwenye Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro.
Carlo na kujitolea kwake kwa Maria
Ushuhuda katika mchakato wa kisheria wa kutangazwa kuwa Mwenyeheri na kutangazwa kuwa Mtakatifu, Kardinali alibainisha katika mahubiri yake, kuwa "unatuambia kwa kauli moja kwamba wema huu ulikuwa ni 'jambo lake zuri zaidi,' na kwamba aliutenda, akionesha mfano kwa wenye umri wake. Na unyenyekevu huu hasa ndio uliomruhusu kupanua upeo wake wa upeo wa juu wa umaskini na mahitaji makubwa zaidi." Na hayo yote, Kardinali Semeraro aliongeza, yalitokana na "ibada yake ya Maria, ambayo ilipata udhihirisho wake muhimu zaidi katika kusali Rozari Takatifu: ilikuwa kukutana kwake kila siku na Yeye, ambaye alimwita 'mwanamke pekee katika maisha yake."
Tamaa hiyo hiyo ya kutembelea madhabahu ya Maria, kama ile ya Pompei, ambayo aliipenda zaidi, pia kwa sababu za kifamilia, "inaweza kueleweka kuwa ni shauku ya kukutana na mpendwa wake. Kutoka kwake, ambaye 'aliweka mambo yote moyoni mwake'(Lk, 2:19 ), Carlo alihisi kutiwa moyo kutafuta ukimya wa ndani unaohitajika ili kusikia sauti ya Mungu. Kwa sababu hii, alikadiria upya Moyo wake mara kwa mara ili kuashiria tena kitendo cha Maria.
![]()
Misa ya shukrani kwa ajili ya kutangazwa kwa Mtakatifu Carlo Acutis (@Vatican Media)
Maria, Nuru ya Mapambazuko
Akiendelea na tafakari yake, Kardinali alisimama kwa muda ili kuzama katika maana ya sikukuu ya kiliturujia ya leo, akikumbuka jinsi Mtakatifu Paulo VI alivyokazia “wakati wa pekee na usio na kifani” unaowakilishwa na kuzaliwa kwa Mama wa Mungu; tukio sio tu "la furaha, kwani kuzaliwa kwa kiumbe kipya ni katika kila familia," alifafanua, "lakini pia jambo lisiloweza kurudiwa katika historia ya mwanadamu, kwa sababu linahusishwa moja kwa moja na fumbo la Umwilisho." Kusherehekea kuzaliwa kwa Mariamu, kwa hiyo, kunamaanisha kukumbatia mpango wa Mungu, unaofanya kazi katika historia, "kwa uzuri na uvumilivu, kuanzia matukio madogo ili kukamilisha kazi ya ulimwengu wote." Hakika si “tukio la ghafula na lililoboreshwa,” mshereheshaji alirudia tena, “lakini ni hatua ya mwisho ya maandalizi marefu ya kufanyika mwili kwa Mwana wa milele wa Mungu.
Ni kama nuru ya kwanza ya mapambazuko." Alfajiri inaeleweka kama "tumaini," fadhila ambayo, "kama Papa Francisko alivyotukumbusha katika Bull of Indiction ya Mwaka huu wa Jubilee, Mariamu ndiye shahidi mkuu." Kwa hiyo, uhusiano wa Semeraro na wazo la Mtakatifu Bernard, ambaye, alijitolea sana kwa Bikira, "alipenda kurudia unyenyekevu huo: Kama vile, katika mfululizo wa saa, huondoa giza na kutangaza nuru, ndivyo unyenyekevu huweka msingi wa maisha ya kiroho. Bila unyenyekevu, hakuna safari ya kweli ya imani inayoweza kuanza, wala mtu hawezi kukua kiroho.” Kimsingi, bila unyenyekevu, hakuna utakatifu.
Carlo katika Mbingu ya Kanisa
Mtakatifu Carlo Acutis sasa anang'aa mbinguni kama nyota inayoongoza njia ya baharia, mshereheshaji alikumbuka kwa sauti kubwa. “Watakatifu pia ni hivi kwetu: pamoja na Maria, ‘Nyota ya Bahari,’ wanatusaidia kuendelea katika urambazaji wa maisha, unaoelekezwa daima kuelekea Kristo. Tukitazama nyota zinazong’aa katika mbingu ya Kanisa, leo pia tunamwona” huyu mtakatifu mpya wa Kanisa, ambaye anahimiza kila mwamini kufuata ushuhuda wake, “kufurahia maisha kikamilifu na kwenda kumlaki Bwana katika sikukuu ya Mbinguni.
![]()
Waamini katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro kwa ajili ya misa ya Shukrani ya kutangazwa Mtakatifu Carlo Acutis, iliyoadhimishwa na Kardinali Semeraro (@Vatican Media)
Misa ya kushukuru Mungu kwa ajili ya Kutangazwa kwa Mtakatifu Carlo Acutis