Ukraine,Padre Oros ametangazwa kuwa Mwenyeheri:mtu wa ushirika katika Ulimwengu uliopasuka
Vatican News
Katika dunia ya leo, iliyosambaratishwa na vita vya kutisha, vilivyogawanyika zaidi ya hapo awali, na ambapo ubinadamu umepoteza uwezo wa kukutana kwa kina na unakabiliwa na upweke wa kutisha, tunahitaji watu wa kukutana na ushirika wa kweli, kama Baba Petro Paolo Oros." Hivi ndivyo Kardinali Grzegorz Ryś wa Poland, Askofu Mkuu wa Łódź, na mwakilishi wa Papa, walivyoeleza Padre wa Kanisa la Byzantine wa Upatriaki wa Mukachevo, ambaye aliuawa mwaka 1953 na kutangazwa mwenyeheri, Jumamosi tarehe tarehe 27 Septemba 2025, huko Bilky nchini Ukraine. Tukio lililokuwa likitazamiwa sana, lililoahirishwa mara kadhaa kutokana na vita vya Ukraine na kifo cha Papa Francisko na pia kukumbukwa na Papa Leo XIV katika Katekesi ya Jubilei katika Uwanja wa Mtakatifu Petro.
Maisha ya upendo
Kardinali Ryś alirejea maisha mafupi ya Mwenyeheri, aliyeuawa na utawala wa kikomunisti akiwa na umri wa miaka 36 tu, bado maisha ya wema, huruma na upendo. "Leo tunamtangaza kuwa Mwenyeheri shahidi ambaye Msalaba wake haukuwa kifo tu, bali maisha yake yote, imani ya kina na hali ya kiroho ya Oros, ambaye magoti yake yalikuwa magumu kama viatu kutoka kwa sala. Na alikufa kwa magoti yake, akiilinda Sakramenti Takatifu, ambayo alikuwa akiibeba kwa ajili ya mgonjwa."
Hakufundisha kwa maneno, bali kwa mfano
Kardinali aliendelea kufafanua kuwa "Yeye, hakufundisha kwa neno lililoandikwa; alifundisha kwa maisha yake, kwa mfano. Hakika, hakuna maandishi ya mahubiri na katekesi zake nyingi zilizobaki. Hata hivyo, licha ya hayo, kutenda kwake mema kunabaki kuwa kumbukumbu ya wengi. Kwa Padre Oros, umaskini na upendo viliunganishwa katika mtazamo mmoja, kama pande mbili zenye uso wake. Alikuwa maskini kwa sababu alitoa; alitoa kwa sababu alijua jinsi ya kuwa maskini. Katika nyumba ambako aliishi, hapakuwa na chochote ila meza rahisi sana na vitu vichache. Alichopokea, aligawa, akikumbatia ubinadamu katika mahitaji yake yote: kutoka kwa kina zaidi na kiroho hadi kwa nyenzo rahisi na zaidi, kwa sababu aliamini kwamba wale wanaohitaji wanapaswa daima kupokea ubora zaidi, na vipya."
![]()
Mchoro wa Padre Petro Paulo Oros
Kuwa huruma hata wakati wa Vita
Kwa kutazama mfano huu, Kardinali aliwahubiria waamini wa Kiukraine kwa mwaliko ufaao: "Ninyi ambao mmekabiliwa na uchokozi na vita kwa miaka mingi; nyinyi ambao mmepoteza sio nyumba zenu tu na mali zenu, lakini pia yale ambayo hayana hesabu, yaani, maisha na afya yenu na ya wapendwa wenu: ni dhahiri kwamba mna haki ya kutarajia msaada kutoka kwa kila mtu. Lakini, hasa leo hii, katika hali hiyo ya kushangaza, ambayo mna kila haki ya kujifikiria kwanza, Mwenyeheri Padre Pietro anawaambia: 'Kuweni na huruma!' alisisitiza Kardinali.
Hali ya Kiroho ya Kukutana
Hatimaye, Kardinali Ryś aliakisi “ushirika wa kiroho wa kukutana unaopatikana kwa yule aliyetangaza kuwa Mwenyeheri , ambaye alipumua kwa mapafu mawili ya Ukristo ya Mashariki na Magharibi, hivyo kuwa “daraja” kati ya dunia mbili, hata katika mazingira magumu. Sote tunahitaji madaraja, lakini tunajua vyema kwamba nyakati za vita, madaraja huwa ya kwanza kupigwa mabomu," alisisitiza Kardinali huyo. Kuwa “daraja” maana yake ni kuwa mtu anayeunganisha, si mtu anayegawanya; akiwa mtu anayegeuza panga kuwa majembe, yaani, anayegeuza silaha kuwa zana za kazi ya kawaida.” Na Padre Petro aliweza kupata lugha ya kawaida kati ya kila mtu: na Wakatoliki wa Kilatini na Byzantine, Wakristo Waorthodox, na wasioamini Mungu."
![]()
Wakati wa maadhimisho ya kutangazwa Mwenyeheri mpya
Hija ya Vijana
Maisha ya mapya ya Mwenyeheri pamoja na yale ya makuhani kaka zake waliokamatwa, kuteswa, kuuawa, na kufa gerezani, Kardinali Ryś alihitimisha, kuwa hufundisha upendo wenye nguvu na mkali, katika maisha na kifo. Hata hivyo maadhimisho hayo, yalitanguliwa Septemba 26, kwa hija kwa miguu kwenda Bilky na takriban vijana elfu moja, ikifuatiwa na Ibada ya Kimungu iliyoongozwa na Askofu Mfransiskani Nil Yuriy Lushchak, Askofu Msaidizi wa Mukachevo wa Ibada ya Byzantine.