Tafuta

Kongamano la II la Kuhusu utunzaji wa wazee Kongamano la II la Kuhusu utunzaji wa wazee 

Kongamano la II la Utunzaji wa Wazee Kichungaji:"Wazee wenu wataota ndoto"

Mkutano huo ulioandaliwa kuanzia tarehe 2 hadi 4 Oktoba 2025 mjini Roma na Baraza la Kipapa la Walei,Familia na Maisha,utawaleta pamoja wajumbe 150 kutoka nchi 65,wanaowakilisha Mabaraza 55 ya Maaskofu,Mashirika ya kitawa na vyama vya kitume.Siku ya Ijumaa tarehe 3 Oktoba 2025,wanatarajiwa kukutana na Papa Leo XIV.

 Vatican News

Katika Kongamano la Pili la Kimataifa la Malezi ya Kichungaji kwa Wazee, lililoandaliwa na Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha, litakalofanyika kuanzia tarehe 2 hadi 4 Oktoba 2025, kwenye Ukumbi Mkuu wa Shirika la Yesu (Jesuit) huko Roma litaongozwa na Kauli mbiu: "Wazee wako wataota ndoto," kifungu cha  maneno kutoka katika Kitabu cha Nabii Yoeli 2, 28-30, ambacho kimekuwa kikitajwa mara kadhaa na Hayati Baba Mtakatifu Francisko. Kwa njia hiyo  wajumbe 150 kutoka nchi 65, wanaowakilisha Mabaraza 55 ya Maaskofu, , Mashirikia ya Kitatawa na Vyama vya kitume  wote wanaohusika katika shughuli za uchungaji wa wazee watakutana.

Kardinali Farrell: Wazee: Sasa na Wakati Ujao wa Kanisa

Kwa mujibu wa Baraza linalooandaa tukio hiko, Mwenyekiti wa Baraza hilo Kardinali Kevin Farelli alisema: "Katika ulimwengu unaobadilika ambamo jinsi tunavyozeeka pia tunapitia mabadiliko makubwa na kwa hiyo  Kongamano hilo linalenga kujibu haja inayozidi kuwa kubwa: ili kuendeleza huduma ya kichungaji kwa wazee inayoendana na changamoto za wakati wetu. Wazee si historia ya Kanisa pekee, lakini pia maisha yake ya sasa na ya baadaye. Kongamano hili ni fursa ya kusikiliza, kutafakari, na kwa pamoja kuendeleza majibu mapya kwa maswali mapya."

Safari ilianza na Kongamano la kwanza la 2020

Safari ambayo inaendelea  inafuata kutoka katika mkutano wa kwanza wa kimataifa wa 2020, wenye mada: "Utajiri wa Miaka." Tangu wakati huo, safari haijasimama: kuanzishwa kwa Siku ya Mababu na Wazee Duniani mwaka 2021 na mfululizo wa Katekesi za Papa Francisko kuhusu uzee mwaka 2022 zimeunganisha usikivu wa Kanisa kwa kundi hili la umri. Kongamano la Kimataifa linawakilisha hatua zaidi katika safari hii, kwa lengo la kutafakari kwa kina na kutambua njia mpya za siku zijazo."

Ndoto za Wazee: Maono ya Wakati Ujao

Kaulimbiu ya Kongamano hilo, iliyoongozwa na Nabii Yoeli, inaalika tafakari ya “ndoto za wazee” kama chanzo cha msukumo kwa Kanisa na jamii. Baadhi ya wazee watashiriki maono yao juu ya masuala muhimu kama vile amani, maisha pamoja, uenezaji wa imani, na utunzaji wa nyumba yetu ya kawaida. Zitakuwa shuhuda hai, kwa maoni ya Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha  zenye uwezo wa kuonesha jinsi ndoto zisivyozeeka na bado zinaweza kuelekeza njia kwa vizazi vipya."

Tafakari ya Ulimwengu ambayo haijawahi kutokea

Katibu Msaidizi wa Baraza hilo Monsinyo Dario Gervasi, alieleza kuwa "Kongamano hili linalenga kuwa maabara ya mawazo na matumaini, fursa ya kipekee ya kujenga maono ya pamoja ambayo yanakumbatia kila kona ya sayari. Wazee ndio moyo unaopiga wa jumuiya zetu, na mchango wao ni muhimu kwa mustakabali wa Kanisa. Mpango huu unajumuisha nyakati za tafakari ya jumla, kazi ya kikundi kwa lugha, na fursa za mazungumzo na kubadilishana uzoefu, ikiwa ni pamoja na wale wazee wenyewe."

Mpango wa Kongamano

Mkutano huo utafunguliwa asubuhi ya tarehe 2 Oktoba 2025  kwa utangulizi wa Hotuba ya Kardinali Farrell, ikifuatiwa na vikao vinavyohusu "Ukweli wa Wazee Leo," "Utamaduni wa Kuachana," na "Hali ya Kiroho ya Wazee." Mkutano na  Papa Leo XIV umepangwa asubuhi ya tarehe 3 Oktoba 2025, wakati Katibu Msaidizi Baraza hilo, Askofu Dario Gervasi, atatoa hotuba ya mwisho, wakati  mwishoni mwa asubuhi ya  tarehe 4 Oktoba  2025.  Mpango kamili wa Kongamano hilo unapatikana hapa:Il programma completo.

26 Septemba 2025, 16:00