Tafuta

2025.09.22 Papa alikutana na Washiriki wa Mpango wa Mawasiliano ya Imani katika Juma la Makazi Roma,wa Ulimwengu wa Kidijitali. 2025.09.22 Papa alikutana na Washiriki wa Mpango wa Mawasiliano ya Imani katika Juma la Makazi Roma,wa Ulimwengu wa Kidijitali. 

Vatican:”Mawasiliano ya Imani katika Ulimwengu wa Kidijitali”

Vijana 16 waliobobea katika mawasiliano,kutoka nchi kumi na moja na walishiriki toleo la V la mpango wa "Imani Mawasiliano katika Ulimwengu wa Kidijitali" unaohamaishwa na Baraza la Kipapa la Mwasiliano.Katika siku zao za mazoezi walisalimiana na Papa Leo na kuzungukia Mabaraza ya Kipapa.Samwel Abesi,kutoka,Jimbo la Kitale,Kenya alikuwa mmojawapo.Meneja Uendeshaji wa Kituo cha Mitume Radio kinachomilikiwa na Jimbo Katoliki la Kitale nchini Kenya.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Hivi karibuni Vijana 16 waliobobea katika mawasiliano,kutoka nchi kumi na moja na walihitimisha toleo la tano la mpango wa "Imani Mawasiliano katika Ulimwengu wa Kidijitali", kuanzia 12-19 Septemba 2025 unaohamasishwa na Baraza la Kipapa la Mwasiliano. Kabla ya kurudi kwao, vijana hawa walifanya uzoefu mbali mbali na baada ya uzoefu huo  mjini Vatican, walikutana na kusalimiana na Baba Mtakatifu Leo XIV, Jumatano tarehe 18 Septemba 2025.

Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mwasiliano, Dk. Paolo Ruffini akikutana nao pia alisema kwa niaba ya kundi zima la Baraza kwamba: "Ni juu yetu kujumuisha kwenye mitandao ya kijamii na katika ulimwengu roho ya Pentekoste. Ndoto yetu ni kupata pamoja na ninyi ambao ni wanadijitali asilia na ambao tayari mnashiriki kwa uhai wa jumuiya zenu, njia mpya na bunifu za kuwasiliana na imani katika mazingira ya kidijitali.”Kwa mujibu wake aisha alingeza kusema kwamba “ Katika muktadha wa mitandao ya kijamii, ambapo watu binafsi mara nyingi huwa watumiaji na bidhaa, tutatafuta pamoja kwa jibu lililojaa imani. Mpango huu uwe hatua ya kwanza ya mwongozo wa njia ambayo tutafuatilia pamoja, tukitembea pamoja."

Kadhalika katika mpango huko kikundi hiki  kilitembelea Radio Vatican,  ambapo idhaa ya Kiswahili ilizungumza na kijana kutoka Jimbo nchini Kenya  aliyekuwa mmojawapo wao akaelezea uzoefu wake kwa Juma moja. Yafuatayo ni maelezo yake: Jina langu ni Samwel Abesi, na ninahudumu kama Meneja Uendeshaji wa Kituo cha Mitume Radio kinachomilikiwa na Jimbo Katoliki la Kitale nchini Kenya. Mimi pia ni mshiriki wa Dawati la Mawasiliano la Jimbo. Kwa sasa niko Roma, nikishiriki na wawasiliani wenzangu vijana walio na umri wa chini ya miaka 35 katika programu ya Mawasiliano ya Imani katika Ulimwengu wa kidijitali. Mpango huu wa mwaka mzima umeundwa ili kuwapa wawasiliani wachanga wa Kikatoliki ujuzi wa kuinjilisha vyema katika mazingira ya kisasa ya kidijitali.

Vijana na Mawasiliano kidijitali
Vijana na Mawasiliano kidijitali

Kivutio kikuu cha programu ni Juma la kuwa na makazi huko Roma, ambapo washiriki wanapewa fursa ya kuona maisha ya Mji Mtakatifu, Vatican na Roma kwa ujumla, na kutembelea maeneo mengi matakatifu na ya kihistoria ndani ya Jiji la Vatican na kwingineko. Katika Juma hili yenye manufaa, tulitembelea maeneo kadhaa muhimu, ikiwa ni pamoja na: Basilika ya Mtakatifu Petro, ambapo kuna kaburi la Mtakatifu Petro na Mapapa wengine, Basilika ya Mtakatifu Yohane Laterano, Kanisa Kuu la Roma, Basilika ya Msalaba Mtakatifu wa Yerusalemu, ambapo masalia ya Msalaba wa Kweli wa Yesu yamehifadhiwa, Basilika ya Mtakatifu Maria Mkuu, Basilika kuu ya kipapa na moja ya makanisa kongwe ya Bikira Maria Roma, ambamo amezikwa Papa Francisko hivi karibuni, Basilika ya Mtakatifu Paulo, Nje ya Ukuta.

Mojawapo ya nyakati za kupendeza  na zisizosahaulika ni kuhudhuria Katekesi kuu ya Papa Francisko siku ya Jumatano, 18 Septemba 2025. Baada ya katekesi yake, tulipata fursa nzuri sana ya kukutana naye ana kwa ana na kupiga picha ya pamoja. Ilikuwa ni uzoefu wa kina wa kiroho. Tulitembelea  Baraza la Kipapa la Mawasiliano na Ofisi zake za mawasiliano za Vatican, pamoja na: Radio ya Vatican, Makumbusho ya Radio ya Vatican, Chumba cha kudhibiti media cha Vatican, Mtazamo wa Ofisi ya waandishi wa habari, Baraza la Kipapa la Makanisa ya Mashariki, vitengo mbali mbali za Baraza la Kipapa la Uinjilishaji.

Kijana Samwel Abes ktuoka Jimbo katoliki Kitale,Kenya

Kwa upande nyumbani huko Kitale nchini Kenya, tuna dawati la mawasiliano la Jimbo linalofanya kazi kikamilifu, ambalo linajumuisha: Radio ya Mitume,  Dawati la media la kidijitali, Idara ya Uzalishaji wa Video,  Sehemu ya kuchapisha, na Mtandao wa Mawakala wa Mawasiliano wa Parokia. Tunaendesha kipindi maalum cha habari za Kikatoliki kwenye Mitume Radio, kinachoruka kila siku kuanzia saa 3:30 usiku hadi saa 4:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki na Kati.  Yaliyomo pia yanashirikishwa kwenye wavuti wetu, ukurasa wa Facebook, na vikundi vya WhatsApp. Kila jioni kuanzia 1:30  hadi 2:00 , tunapeperusha taarifa ya Kiswahili iliyorekodiwa mapema kutoka Vatican News, ili kusaidia wasikilizaji wetu kuendelea kuwasiliana na Kanisa na Jumuiya ya Kikatoliki duniani kote. Tunashukuru Vatican News kwa kuendelea kutufahamisha kuhusu kile kinachotokea katika Kiti Kitakatifu. Ninawashukuru sana Baraza la Mawasiliano kwa kuandaa tukio la maana katika Jiji la Milele, na Radio Vatican kwa kutupa fursa ya kuoneshwa katika vipindi vyao. Shukrani za pekee kwa Askofu wangu, Mwashamu Henry Juma Odonya, kwa uongozi wake wa maono na kwa kuandaa timu yetu na kamera na zana nyingine muhimu ambazo zimetuwezesha kubadili uinjilishaji wa kidijitali na utangazaji wa moja kwa moja wa matukio.

Kundi la vijana 16 katika ubobezi wa mitandao ya kidijitali
Kundi la vijana 16 katika ubobezi wa mitandao ya kidijitali

Ushuhuda mwingine

Mwingine alikuwa Miraal, miaka 25, kutoka Bethlehemu, aliyeajiriwa katika idara ya mawasiliano ya  Upatriaki wa Kilatini wa Yerusalemu, ambaye alisema hivi: “Nilikuja kwa moyo mkunjufu ili kusikiliza na kujifunza yale ambayo Bwana ameniwekea katika juma hili tutalokaa pamoja jijini Roma.

Na Kendall, miaka 25, kutoka Washington, D.C., akifanya kazi katika ofisi ya mawasiliano ya Baraza la Maaskofu Katoliki Marekani, ambaye alionesha shauku kuhusu “fursa ya kuingiliana na wafanyakazi wenzangu na marika kutoka  Ulimwenguni kote : inaniweka wazi kwa mitazamo tofauti, na zaidi ya yote kwa umoja wa Kanisa.”

Lakini kwa nini Program hii?

Kwa mujibu wa Waandaji wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano, wanabainisha kuwa katika uzoefu wa kipekee wa mafunzo ya ufundi kwa wanawasilianaji vijana 16 kwa mwaka, ni “Uzoefu wa kujifunza kwa kufanya ili kupata utaalamu wa maudhui na mawasiliano katika kutumia vyombo vya habari vya kidijitali ili kuwasiliana vyema na imani na kuhudumu kwa ufanisi misheni ya Kanisa. Katika mtazamo wa sinodi ya kusikilizana na kushirikiana, sambamba na utabiri wa Yesu na Majisterio ya Papa Francisko.”

Malengo ya programu

Kukuza mbinu bora za malezi ya kiroho na kueneza msukumo wa njia mpya na bora za Mawasiliano ya Imani kupitia vyombo vya habari vya dijitali. Kukuza ubadilishanaji wa zawadi na mikoa/nchi ambapo Kanisa linakabiliwa na kutengwa. Ili kujenga ufahamu wa jinsi Wakatoliki, hasa kizazi kipya, wanavyotumia vyombo vya habari vya kidijitali katika maisha ya kila siku.

Nini kinafanyika?

Mikutano ya kila Juma kwenye jukwaa la  Zoom kwa miezi 11. Hii inahusisha: Kazi ya mtu binafsi na ya kikundi; Mipango ya mawasiliano kwa taasisi washirika; Juma  moja ya makazi jijini Roma; Miongoni mwa vigezo vya uteuzi; Umri usiozidi miaka 35; Uundaji na uzoefu wa kufanya kazi katika mawasiliano na media ya kidijitali; Asili thabiti ya Kikatoliki: mgombea anayefaa anahudumu katika Jumuiya ya Kikatoliki katika Uwanja wa mawasiliano. Na hatimaye inapendekezwa: ustadi wa hali ya juu wa Kiingereza kwani ndio lugha  inayotumiak ya kufanya kazi ya programu nzima.

Mawasiliano ya kidigitali
22 Septemba 2025, 11:36