Tafuta

Uteuzi wa  Maaskofu. Uteuzi wa Maaskofu. 

Papa amemteua Askofu Touabli kuwa wa Mtakatifu Petro huko Ivory Cost

Askofu Youlo Alexis Touabli ameteuliwa na Baba Mtakatifu Leo XIV kuwa wa Jimbo la Mtakatifu Petro,nchini Ivory Coast ambapo kabla ya uteuzi alikuwa wa Jimbo la Agboville na Rais wa Shirikisho Baraza la Maaskofu wa Afrika Magharibi(CERAO).

Vatican Nwes.

Baba Mtakatifu Leo XIV amemteaua Askofu Askofu Youlo Alexis Touabli, kuwa Askofu wa Mtakatifu Petro huko Ivory Cost kwa kumuhamishia kutoka makao yake ya kiaskofu ya  Agboville. Hadi utezi huo alikuwa Askofu wa Agboville, na Rais wa Shirikisho la Mabaraza la Maaskofu ya Afrika Magharibi  (CERAO).

Wasifu wake

Askofu Youlo Alexis Touabli alizaliwa tarehe 1 Januari  1961 huko  Bereblo Tabou. Akajiunga na kuoenda daraja la Upadre kunako tarehe 8 Agosti 1987 kwa ajili ya Jimbo la Mtakatifu Petro wa Ivory Coast nchii Ivory Coast. Alijikita na majukumu kadhaa pamoja na masomo: mwalimu wa Seminari ndogo ya Gagnoa (1987-1990) na Seminari ndogo ya  Yopougon (1990-1992); Leseni  ya  Falsafa katika Taasisi Katoliki ya Paris,  Ufaransa (1992-1995); Makamu Paroko wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro  (1995-1997); Mwalimu wa Seminari Kuu ya Daloa (1997-1999); Leseni ya Kanuni za Sheria  katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Santa Croce, Roma (1999-2001);

Kadhalika ameshikilia nafasi ya kuwa Mhudumu  wa Parokia ya Mtakatifu André, Sassansra (2001-2002);  Paroko wa Mtakatifu  Paulo huko  Mtakatifu  Pedro na Makamu wa jimbo hilo (2003-2006); Rais wa Baraza la Maaskofu katoliki la Ivory Coast(2011-2017); Msimamizi wa Kitume wa Jimbo la Yamoussoukro (2018-2023). Kunako tarehe 14 Oktoba 2006 alichaguliwa kuwa Askofu wa Agboville, na kuwekwa wakfu wa kiaskofu kunako tarehe 6 Desemba. Na tangu tarehe 5 Mei 2022, alikuwa na Rais wa Shirikisho ma Mabaraza ya Maaskofu wa Afrika Magharibi(CERAO).

 

22 Oktoba 2025, 16:59