Tafuta

Maaskofu wakati wa Sinodi mjini Vatican. Maaskofu wakati wa Sinodi mjini Vatican.  (Vatican Media)

Jubilei ya Timu ya Kisinodi kutoka Ulimwenguni Oktoba 24-26

Kuanzia tarehe 24 hadi 26 Oktoba,timu ya makundi ya Kisinodi na Mashirika ya ushiriki yatakutana kwa ajili ya tukio ambalo ni muhimu katika hatua ya kukamilisha maelekezo yaliyoibuka katika Hati ya Mwisho ya Mkutano wa Kawaida wa XVI wa Sinodi ya Maaskofu.Oktoba 25 alasiri kuna mkutano wa mazungymzo na Papa ambaye ataadhimisha misa ya Dominika ikitanguliwa na mkesha wa Jumamosi wa sala katika Uwanja wa Mtakatifu Petro.

Vatican News

Wakati wa maombi, kushiriki, na utambuzi. Hivi ndivyo timu za sinodi na mashirika ya ushiriki yanajiandaa kupata uzoefu kwa Jubilei yao, ambayo itafanyika kuanzia tarehe 24 hadi 26 Oktoba 2025. Tukio hili, kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari, inasisitiza kuwa ni wakati muhimu katika utekelezaji wa miongozo inayotoka katika Hati ya Mwisho ya Baraza la XVI la Kawaida la Sinodi ya Maaskofu. Mkutano na Papa Leo XIV utafanyika siku ya Ijumaa alasiri 24 Oktoba, ukifuatiwa na tafakari juu ya mada za kisinodi na mkesha wa kufunga katika uwanja wa Mtakatifu Petro.  Na Dominika saa 4:00 asubuhi, majira ya Ulaya, itafanyika Misa itakayoongozwa na Papa Leo XIV, katika Kanisa Kuu la Vatican.

Kutafsiri Miongozo ya Hati ya Mwisho kuwa Chaguo za Kichungaji

Takriban washiriki 2,000 wa timu za Kisinodi na mashirika ya ushiriki (baraza la kipresbiteri, baraza la wachungaji, baraza la masuala ya uchumi, n.k.) wanatarajiwa kushiriki katika ngazi ya Kijimboi/Kipatriaki, kitaifa, na/au kimataifa. Tukio hili linaashiria hatua ya kwanza ya pamoja katika awamu ya utekelezaji, ambayo inalenga kutafsiri miongozo ya Hati ya Mwisho katika uchaguzi wa kichungaji na kimuundo unaolingana na asili ya sinodi ya Kanisa. "Wakati huo huo," taarifa hiyo inaendelea, "tukio hilo linanuia kutambua huduma muhimu inayotolewa na mashirika haya na watu wanaofanya kazi ndani yao, na kuweka ujenzi wa Kanisa la Sinodi linaloongezeka katika upeo wa matumaini ya Jubilei."

Kikao cha Ufunguzi

Kikao cha Ufunguzi kimepangwa kufanyika saa 3:00 asubuhi majira ya Ualaya  siku ya Ijumaa tarehe 25 Oktoba (utiririshaji wa moja kwa moja utatolewa kwenye Vatican News na idhaa za Sekretarieti Kuu ya Sinodi). Programu hiyo inajumuisha mawasilisho ya Kardinali Grzegorz Ryś, Askofu Mkuu wa Łódź (Poland), juu ya Sinodi Katika Kukabiliana na Mivutano katika Kanisa; Profesa Miguel De Salis Amaral, Profesa katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Msalaba Mtakatifu(Santa Croce), ambaye atazungumza juu ya mada ya "Uongofu wa Mahusiano"; na Mariana Aparecida Venâncio, mshiriki wa Timu ya Sinodi ya Baraza la Maaskofu la Brazili, ambaye atashughulikia ‘sinodi kama unabii wa kijamii.’ Pamoja na Papa Leo XIV katika, mkutano wa mazungumzo siku ya Ijumaa na Misa katika Basilika siku ya Dominika ijayo. Mazungumzo ya mkutano na Leo XIV yamepangwa kufanyika saa 17:00 siku ya Ijumaa.

Wawakilishi kutoka maeneo saba ya mbali watawasilisha ripoti kuhusu changamoto na mabadiliko yaliyoanzishwa ili kuendeleza sinodi katika maeneo yao, likifuatiwa na swali kutoka kwa Mrithi wa Petro. Kipindi hicho pia kitajumuisha michango ya muziki kutoka kwa Padre Cristobal Fones SJ, Mkurugenzi wa Mtandao wa Maombi ya Papa Ulimwenguni. Papa mwenyewe ataongoza Misa ya Jubilei siku ya Dominika saa 4:00 asubuhi katika Kanisa kuu la Mtakatifu Petro.

Warsha, semina mada na mkesha wa mwisho katika Uwanja wa Mtakatifu Petro

Jumamosi tarehe 26 Oktoba 2025, kuanzia saa 2:00 asubuhi, imewakwa kwa ajili ya kuvuka Mlango Mtakatifu. Zaidi ya vikundi mia vya lugha ndogo vitashiriki uzoefu wao kupitia njia ya Mazungumzo katika Roho. Warsha na semina za kina zitafanyika mwishoni mwa asubuhi na mapema alasiri, ukijumuisha semina 25 za lugha na semina sita za mada juu ya ubadilishaji wa kimisionari na sinodi ya Kanisa.

Kikao cha mwisho, kuanzia saa 5:00 asubuhi hadi saa 6:30 jioni pia itatiririshwa moja kwa moja kwenye chaneli zile zile, ikishiriki uzoefu wa sinodi na mbinu bora zaidi. Tukio hili litasimamiwa na Enrico Selleri (TV2000) na Paola Arriaza (EWTN), na maonesho ya kikundi cha ScalaMusic. Ili kuhitimisha tukio la Jubilei, Mkesha wa Sala ya Maria utafanyika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, kuanzia saa 3:00 usiku, ambayo itakuwa wazi kwa mahujaji wote jijini  Roma. Kwa njia hiyo Dominika tarehe 26 hadi Jumatano 27 Oktoba 2025, Baraza la Kawaidia la Skretarieti ya Sinodi itakutana.

Asante kwa kusoma makala hii. Kama unataka kubaki umesasishwa, tunakualika ujiandikishe hapa: cliccando qui

22 Oktoba 2025, 18:48