Tafuta

2025.10.30 Papa akutana na Rais  Ratu Naiqama Tawake Lalabalavu, wa Fiji 2025.10.30 Papa akutana na Rais Ratu Naiqama Tawake Lalabalavu, wa Fiji  (@VATICAN MEDIA)

Papa akutana na Rais Lalabalavu wa Fiji

Papa alikutana na Rais wa Jamhuri ya Fiji Bwana Ratu Naiqama Tawakecolati Lalabalavu,katika Jumba la Kitume ambapo mara baada ya mkutano huo alikutana na Kardinali Pietro Parolin, Katibu Mkuu wa Vatican akiambatana na Monsinyo Daniel Pacho,Katibu Msaidizi kwa ajili ya Kitengo cha kimataifa cha Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa.

Vatican News

Baba Mtakatifu Leo XIV, Alhamisi tarehe 30 Oktoba 2025, amekutana na Rais wa Jamhuri ya Fiji Bwana Ratu Naiqama Tawakecolati Lalabalavu, katika Jumba la Kitume ambapo mara baada ya Mkutano huo alikutana na Kardinali Pietro Parolin, Katibu Mkuu wa Vatican akiambatana na Monsinyo Daniel Pacho, Katibu Msaidizi kwa ajili ya Kitengo cha kimataifa cha Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa.

RAIS WA FIJI
RAIS WA FIJI   (@VATICAN MEDIA)

Wakati wa Mazunguzo yao na Sekretarieti ya Vatican, wamepongezana mahusiano mazuri yaliyopo sehemu zote mbili kati ya Vatican na Jamhuri ya Fiji, ikiwa ni pamoja na chango wa Kanisa Katoliki katika huduma kwa jamii.

Katika mwendelezo wa mazungumzo hayo, wamekuwa na mtazamo juu ya hali ya siasa kijamii ya Nchi, kwa kujikita zaidi kwa namna ya pekee juu ya mada yenye maslahi ya pamoja, miongoni mwake ulinzi wa mazingiria, na mapambanano dhidi ya uhalifu wa kimataifa.

30 Oktoba 2025, 16:45