Tafuta

2025.10.22 Mhs.Jean-Pierre Tanoh Tiémélé, Askofu Mpya wa Jimbo Katoliki la Abengourou - Ivory Coast 2025.10.22 Mhs.Jean-Pierre Tanoh Tiémélé, Askofu Mpya wa Jimbo Katoliki la Abengourou - Ivory Coast 

Papa Leo XIV amteua Askofu mpya wa Jimbo la Abengourou,Ivory Coast.

Padre Jean-Pierre Tanoh Tiémélé alizaliwa tarehe 22 Februari 1969 huko Treichville.Baada ya mafunzo yake katika Chuo Kikuu cha Félix-Houphouët-Boigny huko Abidjan,alipata Shahada ya Uzamili katika Utawala wa Biashara.Masomo ya Falsafa na Taalimungu katika Seminari Kuu ya Anyama na ya Mtakatifu Paulo VI huko Abidjan.Alipewa Daraja la Upadre kunako tarehe 29 Januari 2011.

Vatican News.

Baba Mtakatifu Leo XIV tarehe 22 Oktoba 2025, alipokea na kukubali barua ya maombi iliyowakilishwa ya kung’atuka katika shughuli za kichungaji kwa Jimbo Katoliki la  Abengourou nchini (Ivory Coast) iliyowakilishwa na Askofu Boniface Ziri Gbaya. Na wakati huo huo Papa akamteua Askofu mpya wa Jimbo hilo  la Abengourou, Mheshimiwa Padre  Jean-Pierre Tanoh Tiémélé, ambaye hadi uteuzi huo alikuwa Makamu Paroko wa Parokia ya Aliyepaa Bwana Yetu Yesu Kristo.

Wasifu wake

Padre Jean-Pierre Tanoh Tiémélé alizaliwa tarehe  22 Februari  1969 huko  Treichville. Baada ya mafunzo yake katika Chuo Kikuu cha Félix-Houphouët-Boigny huko  Abidjan, alipata Shahada ya Uzamili katika Utawala wa Biashara (MBA) katika Chaguo la Ujasiriamali na Maendeleo Endelevu katika Kituo cha Utafiti na Matendo kwa ajili ya amani, Cha Taasisi ya Hadhi na Haki za Binadamu(CERAP/DDH), na shahada ya Uhandisi katika Ukaguzi na Udhibiti wa Usimamizi kutoka Shule ya Biashara ya Castaing huko Abidjan. Baadaye alimaliza masomo yake ya Falsafa na Taalimungu  katika Seminari Kuu ya Moyo Safi wa maria huko Anyama na Seminari Kuu ya Mtakatifu Paulo VI huko Abidjan, na kupata Leseni katika Taalimungu.

Askofu Mteule huyo,  alipewa daraja la upadre kunako tarehe 29 Januari 2011.

Ameshika nyadhifa nyingine zifuatazo: Mkurugenzi Mkuu na Msimamizi wa Kituo cha Padre Mathieu Ray cha Koumassi (2011-2015); Padre wa  Jimbo kwa ajili ya Skauti Katoliki (2013-2015); Mshauri wa Baraza la Jimbo kwa Masuala ya Uchumi (2014-2015); Katibu wa Uchungaji wa Kijamii wa Baraza la Maaskofu (2015-2016) na Katibu Mtendaji wa Taifa wa Caritas Ivory Coast (2015-2024); na, hadi uteuzi huo alikuwa Padre kwenye Parokia ya Aliyepaa Bwana wetu Yesu Kristo.

Kung'atuka katika usimamizi wa Kitume huko Tripoli nchini Libya

Papa Leo XIV vile vile  amekubali kung’atuka kwa shughuli za kichungaji katika Usimamizi wa Kitume wa Tripoli nchini Libya, uliowakilishwa na Monsinyo George Bugeja, O.F.M.

22 Oktoba 2025, 18:10