Tafuta

Mandalizi ya Maadhimisho ya Kila Mwaka ya Deepavali ya Wahindi tarehe 20 Oktoba 2025. Mandalizi ya Maadhimisho ya Kila Mwaka ya Deepavali ya Wahindi tarehe 20 Oktoba 2025.  (ANSA)

Vatican Deepavali:katika roho ya Nostra Aetate Wakristo na Wahindu na amani

Waamini waliokita mizizi katika tamaduni zao za kidini na kama watu wa maadili ya pamoja na kujali pamoja amani,Wahindu,Wakristo na wale wa dini nyingine na wenye mapenzi mema wanaweza kuungana ili kukuza amani duniani.Katika Ulimwengu,ambapo kutoaminiana,migawanyiko na mivutano inaongezeka,mazungumzo baina ya dini ni ya lazima zaidi kuliko wakati mwingine wowote,hivyo kuna umuhimu wa kuhimiza ushirikiano wa kidini.

Na Angella Rwezaula -Vatican.

Katika fursa ya maadhimisho ya Siku kuu ya kila mwaka ya Kihindi iitwayo Deepavali itakayofanyika tarehe 20 Oktoba 2025, Kardinali George Jacob Koovakad, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mazungumzo ya Kidini, pamoja na Katibu Mkuu wa Baraza hilo Monsinyo Indunil Janakaratne Kodithuwakku Kankanamalage walituma ujumbe wao unaongoza na kauli mbiu: “Wahindu na Wakristo: Kujenga amani ya ulimwengu kupitia mazungumzo na ushirikiano katika roho ya Nostra Aetate. Ujumbe huo unaelezea jinsi ambavyo baraza la Kipapa la Mazungumzo ya Kidini ilivyo na furaha ya  kutoa salamu zake za uchangamfu na heri njema kwao wanaposherehekea Deepavali tarehe 20 Oktoba mwaka huu. “Tamasha hilo la taa na liangaze maisha yenu na kuleta furaha, umoja na amani kwa familia na jamii zenu!”

Miaka 60 ya Waraka wa Kitume wa Nostra Aetate

Katika ujumbe huo aidha wanabainisha juu ya Tukio la Kanisa kwamba “Siku ya nane baada ya Deepavali mwaka huu itaadhimisha kumbukumbu ya miaka sitini ya Nostra Aetate (28 Oktoba 1965), Hati ya kihistoria ya Kanisa Katoliki ya Mtagauso wa II wa Vatican, ambayo uliwahimiza Wakatoliki duniani kote kushiriki katika mazungumzo na ushirikiano na watu wa tamaduni nyingine za kidini.” Hati hiyo iliwahimiza wote "kutambua, kuhifadhi na kuendeleza mambo mazuri, ya kiroho na ya kiadili, na vile vile maadili ya kijamii na kitamaduni" yanayopatikana kati yao (NA, 2) katika huduma ya kukuza amani. Ujumbe huo kadhalika unasisitiza kuwa “Katika kipindi cha miongo sita iliyopita, mpango huu wa kihistoria wa mazungumzo ya kidini umebadilika na kuwa mpango wa kimataifa, unaoungwa mkono kwa ukarimu na kufadhiliwa na watu wa imani tofauti za kidini na wasio na imani sawa, na hivyo kutoa mchango mkubwa kwa amani ya ulimwengu. Ujumbe huu wenyewe ni tunda la maono hayo bora.”

Tupyaishe ahadi zetu za kukuza mazungumzo ya kidini

“Katika jubilei hii ya almasi, Nostra Aetate inatualika kupyaisha ahadi yetu ya kukuza mazungumzo ya kidini kama njia ya amani. Katika msimu huu wa sikukuu, tunawaaalika mjiunge nasi katika kutafakari jinsi  ambavyo Wakristo na Wahindu, pamoja na watu wa dini zote na nia njema, wanaweza kuimarisha juhudi zetu za pamoja za amani kupitia mazungumzo na ushirikiano katika roho ya Nostra Aetate.”  Roho kama hiyo imekita mizizi katika “kukuza umoja na upendo miongoni mwa watu, hakika miongoni mwa mataifa” kwa kuzingatia “kile ambacho watu wanacho sawa na kile kinachowavuta kwenye ushirika” (NA 1). Inatuita kukataa “chochote ambacho si cha kweli na kitakatifu” katika dini nyingine na kushikilia “kwa heshima ya kweli zile njia za mwenendo na za maisha, yale maagizo na mafundisho” ambayo “yanaakisi mwali wa Ukweli huo unaowaangazia watu wote” (NA 2).

Kukuza na kuhifadhi pamoja manufaa ya watu,haki ya kijamii na ustawi wa maadili

Hati hiyo pia inahimiza azimio thabiti "kuhifadhi na kukuza pamoja kwa manufaa ya wanadamu wote haki ya kijamii na ustawi wa maadili, pamoja na amani na uhuru" (NA 3). Ingawa maendeleo mengi yamefanywa tangu Nostra Aetate, mengi zaidi yanapaswa kufanywa. Katika ulimwengu wa leo, ambapo kutoaminiana, ubaguzi, mivutano na migawanyiko inaongezeka, mazungumzo kati ya dini ni muhimu zaidi kuliko hapo awali. Ni lazima iendelee kupanda mbegu ya umoja na upatanisho, na kuwa mwanga wa tumaini kwa wote."

Kwa pamoja tunaweza kudumisha amani inayosimika mizizi katika ukweli,haki,upendo na uhuru

Uelewa wa kidini na ushirikiano lazima upate nafasi katika maisha yetu ya kila siku na kuwa njia ya asili ya kuishi pamoja.  Papa Leo XIV ametoa wito kwa watu wote "kujenga madaraja kwa njia ya mazungumzo na kukutana, kuungana pamoja kama watu wamoja" (Urbi et Orbi, 8 Mei 2025). Anatukumbusha kwamba kukuza utamaduni wa mazungumzo na ushirikiano kwa ajili ya amani ni "kazi iliyokabidhiwa kwa wote, waamini na wasioamini, ambao lazima waiendeleze kwa tafakari na  hatua inayochochewa na utu wa mtu na manufaa ya wote" (Ujumbe kwa Harakati na vyama kuhusu mkutano wa amani” Verona, 30 Mei20). Ni kwa kufanya kazi pamoja tu ndipo tunaweza kupata na kudumisha amani inayosimikwa katika ukweli, haki, upendo na uhuru (taz. Yohane Paul II, Ujumbe wa Maadhimisho ya Siku ya Amani Duniani, 1 Januari 2003).

Familia ni msingi wa Elimu katika maisha ya imani 

Baraza la Kipapa la Mazungumzo ya Kidini kadhalika linasisitiza kwamba "Familia, kama mahali pa msingi pa elimu katika maisha na imani, ina jukumu kuu katika kukuza maadili haya. Tamaduni za kidini pia zina jukumu muhimu katika kukuza amani, huku viongozi wa kidini wakiwa na wajibu wa kimaadili wa kuongoza kwa mfano - kuwahimiza wafuasi wao kuheshimu utofauti na kujenga madaraja ya urafiki na udugu.  Taasisi za elimu na vyombo vya habari vilevile hutekeleza majukumu muhimu katika kuunda mioyo na akili kuelekea kuishi pamoja kwa amani. Kwa njia hiyo  mazungumzo baina ya dini na ushirikiano unaweza na lazima ukumbwe kama nyenzo za lazima katika kukuza utamaduni wa amani; wanapaswa kukua na kuwa harakati lenye nguvu na mvuto linalojitolea kujenga na kulinda amani wakati wote.

Kama waamini waliokita mizizi katika mapokeo ya imani yetu, na kama watu waliounganishwa kwa maadili ya pamoja na kujali kwa pamoja amani, naomba sisi - Wahindu na Wakristo, pamoja na wale wa dini nyingine na watu wote wa nia njema - tushikane mikono kwa njia ndogo na kuu za kulea amani katika nyumba zetu, jumuiya na jamii zetu.  Na tujitahidi kujenga amani ya ulimwengu kwa kukuza "utamaduni wa mazungumzo kama njia; ushirikiano wa pande zote kama kanuni ya maadili; kuelewana kama mbinu na kiwango." Tunawatakia nyote Heri ya Deepavali!"

Rais wa Tume ya haki na amani Tanzania

Asante sana kusoma makala hii. Kama unataka kubaki na sasisho, tunakualika kujiandikisha hapa ili kupata habari za kila siku: cliccando qui

14 Oktoba 2025, 11:49