Tafuta

Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Mataifa na Mashirikia ya Kimataifa akihutubia katika UNGA80,New York Marekani. Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Mataifa na Mashirikia ya Kimataifa akihutubia katika UNGA80,New York Marekani. 

Vatican yahimiza hatua juu ya uwezeshaji wa vijana,afya na ustawi katika UN

Vatican inatoa wito kwa Ulimwengu kufanya zaidi kwa ajili ya vijana na kuongeza juhudi za kupambana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza na changamoto za afya ya akili.Ni dhamira ya Kanisa Katoliki katika kutoa huduma za afya na kukuza ustawi,hasa miongoni mwa maskini na wanaoishi katika mazingira magumu,kupitia taasisi zake duniani kote.

Na Sr. Christine Masivo Cps.

Akizungumza katika Mikutano miwili ya ngazi ya juu ya Umoja wa Mataifa, Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa  kwa Mahusiano na Mataifa, alizitaka serikali kutambua vijana kama   wasanii wa amani na wasimamizi wa uvumbuzi, kufanya upya ahadi yake ya kuwawezesha vijana, wakati pia kukabiliana na mzozo wa afya duniani.

Uwezeshaji wa vijana

Kwenye ukumbusho wa Mpango wa Ulimwengu wa tekelezaji kwa vijana wenye umri wa miaka 30, Askofu Mkuu Gallagher alisema, “vijana wanakumbana na vita, ukosefu wa haki wa kijamii, njaa, ukosefu wa usawa, na unyonyaji wa mazingira.” Alitaja takwimu zinazosumbua za zaidi ya asilimia 20 ya vijana duniani kote hawapo katika elimu, ajira, au mafunzo. Alionya kwamba vita, dhuluma za kijamii, njaa, ukosefu wa usawa, na unyonyaji wa watu na mazingira vinadhoofisha uwezo wa vijana na ufahamu wao wa heshima waliyopewa na Mungu.

Elimu

"Zaidi ya asilimia ishirini ya vijana duniani kote wametengwa na elimu, ajira, au mafunzo," alibainisha, huku akisisitiza kuwa kutengwa huongeza hatari ya masuala ya afya ya akili. Alitoa wito wa elimu bora, inayofikika na inayoheshimu nyanja za kitamaduni, kijamii, kisiasa na kiroho huku akisisitiza umuhimu wa kulinda haki za kimsingi, ikiwa ni pamoja na uhuru wa dini na imani.

Wajibu wa familia

Askofu Mkuu Gallagher pia alisisitiza jukumu muhimu la familia katika kuunda watu wazima wanaowajibika kwa njia ya mazungumzo kati ya vizazi. Akinukuu maneno ya Papa Leo XIV, alitoa wito kwa vijana kukumbatia utume wao wa matumaini, amani, na upatano: “Ulimwengu unawatazama ninyi, tunawahitaji ninyi, tunataka mje pamoja ili kushiriki nasi katika utume huu wa pamoja.

Afya ya akili na magonjwa ya kuambukiza.

Baadaye, akihutubia katika mkutano wa nne wa ngazi ya juu wa kinga na udhibiti wa magonjwa yasioambukiza (NCDs) na uendelezaji wa ufya ya ukili na ustawi, Askofu Mkuu alisisitiza kwamba afya ni haki ya binadamu na msingi wa maendeleo Aliwakumbusha wajumbe kuwa magonjwa yasiyoambukiza na hali ya afya ya akili bado ni sababu kuu za vifo na ulemavu, haswa katika nchi za kipato cha chini na cha kati. "Kuhakikisha afya na ustawi kwa wote ni jambo lisiloweza kutenganishwa na kutokomeza umaskini," alisema, akitoa wito wa huduma ya afya kwa wote kwa kuzingatia sana huduma ya afya ya msingi, kinga, na matibabu kwa wakati. Pia aliakisi idadi ya kutisha ya watu wanaojiua, hasa miongoni mwa vijana.

“Jamii ina wajibu muhimu wa kuthibitisha utakatifu wa maisha na hadhi iliyotolewa na Mungu ya wale ambao hawawezi kuitambua wenyewe kwa muda," alisisitiza, akikataa kwa uthabiti kujiua kwa kusaidiwa kuwa hakupatani na maadili ya matibabu na utu wa binadamu. Askofu Mkuu Gallagher alisisitiza dhamira ya Kanisa Katoliki katika kutoa huduma za afya na kukuza ustawi, hasa miongoni mwa maskini na wanaoishi katika mazingira magumu, kupitia taasisi zake duniani kote.

Wito kwa uwekezaji wa vijana na afya ya pamoja

Katika hotuba zote mbili, Askofu Mkuu aliashiria muunganiko wa uwezeshaji wa vijana na afya kwa pamoja, akisema jumuiya ya kimataifa ina wajibu wa pamoja wa kuhakikisha utu, matumaini na mustakabali mwema kwa wote. Wito wake ulitoa wito kwa serikali, taasisi na jumuiya kufanya kazi pamoja katika vizazi vyote ili kujenga jamii yenye haki, amani na afya zaidi.

Hotuba ya Askofu Mkuu Gallagher
01 Oktoba 2025, 08:43