Tafuta

Askofu Mkuu Gallagher. Askofu Mkuu Gallagher. 

Gallagher nchini Sri Lanka kwa kumbukizi ya miaka 50 ya uhusiano wa kidiplomasia na Vatican

Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa anatembelea nchi ya Asia kuanzia Novemba 3 hadi 8 ili kuimarisha dhamira ya pamoja ya amani na ushirikiano. Atakutana na Rais na Waziri Mkuu, viongozi wa kisiasa na kidini, na kutembelea maeneo ya mashambulizi ya Dominika ya Pasaka 2019.

Vatican News

Kuanzia tarehe 3 Novemba 2025, hadi Dominika tarehe 9 Novemba 2025 Askofu Mkuu Paul R. Gallagher, Katibu wa  Vatican wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa, ataadhimisha miaka 50 ya uhusiano wa kidiplomasia na Vatican na kuimarisha dhamira ya pamoja ya amani na ushirikiano nchini Sri Lanka. Pia atatembelea maeneo yaliyoathiriwa na mashambulizi mabaya ya Pasaka 2019.

Programu ya safari

Maelezo zaidi yanaweza kupatikana katika programu iliyochapishwa na akaunti rasmi ya X ya Sekretarieti ya Vatican @TerzaLoggia, Askofu Mkuu Gallagher atakutana na Waziri Mkuu Harini Amarasuriya. Siku ya Jumanne, Novemba 4, atakutana na Rais Anura Kumara Dissanayake, ikifuatiwa na mkutano na Vijitha Herath, Waziri wa Mambo ya Nje. Siku hiyo hiyo, askofu atashiriki katika Mkutano kuhusu Mtazamo wa Vatican na Kujitolea kwa Mazungumzo na Amani, na sherehe ya kumbukumbu ya miaka 50 ya uhusiano wa kidiplomasia.

Ziara ya Maeneo ya Mashambulizi ya 2019

Siku ya tarehe 5 Novemba itaanza na ziara ya maeneo ya mashambulizi ya Pasaka 2019, ambayo yalisababisha vifo vya zaidi ya watu 250. Mara tu baada ya hapo, Askofu Mkuu Gallagher ataadhimisha Misa ya Shukrani katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Lucia huko Colombo na kukutana na Baraza  la Maaskofu wa Sri Lanka.

Siku ya Novemba 6, mikutano imepangwa na mamlaka ya kidini ya Malwatta huko Kandy na mamlaka ya kidini ya Asgiriya, pia huko Kandy, ikifuatiwa na ziara ya Hekalu la Wabuddha la Kandy. Siku ya mwisho, Katibu wa Mahusiano na Nchi na Mashirikia ya Kimataifa atatembelea Seminari ya Kitaifa ya Mama Yetu wa Sri Lanka na kukutana na waseminari na wafanyakazi wa kitaaluma.

Mons Gallagher

Asante sana kusoma makala hii. Kama unataka kusasishwa, jiandikishe hapa: cliccando qui

03 Novemba 2025, 16:28