Kard.Parolin huko Pompei:mji wa matumaini,sala na huruma!
Na Angella Rwezaula - Vatican
Katika fursa ya kumbukizi ya Miaka 150 ya kuwasili kwa Picha ya Mama Maria wa Rozari huko Pompei, Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican aliongoza Ibada ya Misa Takatifu akimwakilisha Baba Mtakatifu katika Madhabahu ya Mama Yetu wa Rozari huko Pompei, Alhamisi tarehe 13 Novemba 2025.
Kardinali aliendelea kusema kuwa “Leo tunaadhimisha kumbukumbu ya miaka 150 ya kuwasili kwa Picha ya Bikira Maria katika nchi hii, ambayo hapo awali ilijulikana kama "bonde la lilioacha." Ilikuwa tarehe 13 Novemba 1875, wakati Mtakatifu Bartolo Longo aliposafirishaPicha ya Bikira hapa. Yeye mwenyewe anasimulia kwamba turubai ilikabidhiwa kwa msafiri ambaye aliisafirisha kwenye gari lililojaa mbolea. Kutokana na ishara hiyo rahisi na ya bidii ya imani, historia mpya ilizaliwa, iliyooneshwa na neema na uwepo wa mama wa Maria. Papa pia anajiunga nasi kiroho katika sala yetu. Katika siku hii, tunamhisi yuko karibu, yupo kati yetu, na tunamkabidhi utu wake na huduma yake ya kitume kwa ulinzi wa Maria, ili aweze kuliongoza Kanisa kwa hekima na nguvu zitokazo juu.”
Kardinali alisema kuwa Papa Francisko aliitaja Madhabahu hii kama "chanzo kikuu na kisichoisha cha uenezaji wa Rozari," akiiita "sala inayosaidia kujenga amani." Pia alisisitiza umuhimu wa majaliwa wa Jubilei Picha ya Mama Yetu wa Pompeii sanjari na Mwaka wa Jubilei unajikita na “ Yesu Tumaini letu na miaka mia 1700 ya Mtaguso wa Nicea (Ujumbe wa Baba Mtakatifu wakati wa Maadhimisho ya Miaka 150 ya kuwasili kwa Picha ya wa Mama Yetu wa Rozari huko Pompeii, 10 Novemba 2024).
Kardinali “Ni Jubilei ya kweli ndani ya Jubilei," kama Askofu Mkuu wenu alivyoandika, ambayo inaambatana na "Pompeii Mpya" katika wakati huu wa neema, iliyofanywa kuwa muhimu zaidi na kutangazwa kwa Bartolo Longo kuwa mtakatifu, ambayo ilifanyika tarehe 19 Oktoba 2025 iliyopita katika Uwanja wa Mtakatifu Petro. Alikuwa mtu wa kawaida ambaye alitoa mwitikio wa kielimu wa ajabu kwa mahitaji ya wakati wake, akitamani, pamoja na kujitolea kwa Maria, kurejesha heshima na mtazamo kwa watu kupitia kazi za elimu na Upendo.”
Kardinali Parolin kwa kuhitimisha alisali hivi: “Ee Maria,Mama wa Rozari,wewe uliyeamini Neno na kulileta ulimwenguni,ufanye upya ndani yetu pia furaha ya imani. Pompei,katika maadhimisho yake ya miaka 150,iendelee kuwa mahali patakatifu pa nuru, shule ya sala, warsha ya upendo. Kila mhujaji anayevuka kizingiti cha nyumba hii ahisi kwamba Mungu yuko karibu, kwamba huruma ina nguvu kuliko dhambi, kwamba tumaini halikatishi tamaa. Na hivyo, tukitafakari pamoja nanyi uso wa Kristo, nasi pia tuwe, kama ninyi, watumishi wa Neno, wamisionari wa upendo, waimbaji wa tumaini.”
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku: Just click here