Mawasiliano,Ruffini:kujenga upya imani katika habari halisi
Na Mariane Rodrigues – Vatican.
"Kila taarifa tunayosambaza ni kama chakula: inaweza kulisha au kuua." Hili lilisisitizwa na Dk. Paolo Ruffini, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano,katika hotuba yake ya Semina ya 12 ya Mawasiliano ya Jimbo Kuu la Rio de Janeiro, iliyofanyika kuanzia tarehe 28 hadi 31 Oktoba 2025, Mkuu huyo alitafakari kuhusu jukumu la wawasilianaji katika nyakati za kisasa, akizungumzia mada za mada kuu: akili unde, taarifa potofu na habari ya kugushi, nguvu ya mfumo wa kimashine katika kudhibiti maudhui, na upweke unaotokana na majukwaa ya kidijitali, ambapo mawasiliano ya moja kwa moja kati ya watu hupotea. Akikabiliana na hali hii ya kutatanisha na isiyo na uhakika, Dk. Ruffini alielezea, kila mtu anaweza kuchagua kujenga upya imani katika habari njema na za kweli, kukumbatia wingi, na kuunda fursa za kukuza nafasi za kusikiliza, mazungumzo, na kutafuta ukweli bila kuchoka.
Mada ya semina ya mwaka huu 2025 ilikuwa ni: "Tweka hadi kilindini! (Lk 5:4) - Kujenga sauti na uwepo katika mikakati ya mawasiliano na usimamizi wa mitandao ya kijamii." Mkuu wa Baraza la Kipapa alishiriki katika mjadala wa meza ya mduara uliopewa jina: "Elimu, Siasa, Uandishi wa Habari, na Afya: Madaraja ya Majadiliano ya Kijamii." Dk. Ruffini aliambatana na Margreth Dalcolmo, mtaalamu wa magonjwa ya mapafu na mtafiti huko Fiocruz, mwandishi wa habari Gerson Camarotti, na mwalimu Cláudia Sabino, ambaye amejitolea katika elimu ya uraia na ujumuishaji wa elimu na mawasiliano.
![]()
Wakati wa Semina ya mawasiliano huko Rio de Janeiro(Emerson Fernandes, Jimbo la Tubarão)
Mawasiliano Yanayojenga Madaraja
Dk. Ruffini alizungumza na wale waliokuwepo kuhusu hitaji la mawasiliano yanayolenga kujenga madaraja, kubadilishana mawazo, ndoto, magumu, na matumaini, ili kukabiliana na mawasiliano ya chuki, kutovumiliana, kutoaminiana, mgawanyiko, na kujiuzulu. "Tunahitaji kusikiliza historia za mema, lakini pia historia za uovu, ambazo kila mara kuna uwezekano wa mabadiliko na ukombozi; lazima tugundue upya, katika kusikilizana, uzuri wa ubinadamu wetu." Kukumbatia wingi pia ni hatua muhimu kuelekea mawasiliano ya heshima kati ya watu. Dk. Ruffini alimnukuu Papa Paulo VI, ambaye alisema: "Sisi ni watu wa wingi hasa kwa sababu sisi ni Wakatoliki, yaani, wa ulimwengu wote," na heshima kwa ukweli na ukweli haipaswi kupunguzwa.
Janga na taarifa potofu
Janga la Uviko-19, Dk. Ruffini alikumbusha, kuwa limewajaribu sio wanasayansi na wafanyakazi wa afya pekee, bali pia waandishi wa habari na wataalamu waliojitolea kusambaza taarifa za kweli. Kuenea bila kudhibitiwa kwa habari za kugushi, kuzaliwa katika jamii zilizofungwa za kidijitali, kulienea haraka kwa makundi mengine, hatimaye kufikia vyombo vya habari vya kitamaduni, alisisitiza Dk. Ruffini. "Wakati wa enzi ya Uviko," alielezea, "tuliona jinsi maoni yasiyo ya kisayansi yalivyosambazwa sana na hata kuaminiwa kwenye mitandao ya kijamii, hata ndani ya jamii kwa matibabu. Na hii ilisababisha mkanganyiko, kupoteza uaminifu, utegemezi wa kiolojia kwa vyanzo mbadala, na kuenea kwa nadharia zisizo za kweli." Katika hali ya mkanganyiko, wengi waliishia kuamini uongo na kutilia shaka ukweli. "Kila mtu anatafuta ukweli lakini hauamini," alirudia. "Au, hatimaye, wanawaamini wale ambao hawastahili uaminifu huo."
![]()
Dk.Paolo Ruffini (katika) na Watoa mada ya Semina ya Mawasiliano huko Rio de Janeiro (Emerson Fernandes, Jimbo la Tubarão)
Akili Unde
Kuhusu akili Unde, Mkuu wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano alisisitiza kwamba inatoa maarifa na vitendo vingi, lakini wakati huo huo inaendeshwa na mfumo wa kimashine, zinazochuja maudhui kupitia mibofyo na zinaweza kusababisha jamii kuamini katika kitu ambacho hakipo au hakijawahi kutokea. "Nafasi inayoonekana kuwa ya umma na isiyo na upande wowote ya majukwaa na akili unde inatawaliwa na mifumo ya kimashine ambazo hakuna hata mmoja wetu amejadili, lakini ambazo zinaweka sheria za mchezo. Mchezo ambao unaweza kuwa hatari sana," alionya. "Kwa mara ya kwanza katika historia," Dk. Ruffini alisisitiza, "ubinadamu unajiuliza kama kile unachokiona na kusikia ni kweli au si kweli."
Utupu wa kutokuwa na uhakika na fursa
Ingawa mazingira ya mawasiliano yamejaa changamoto, mitego, na utupu wa kidijitali, kwa upande wa Dk. Ruffini, huu pia ni wakati wa fursa na chaguo. "Uwanja wazi ambapo tunaweza kuchagua kushirikiana," alielezea, "kujenga madaraja na ushirikiano kati ya wanaume na wanawake wenye mapenzi mema; au kuwaacha wengine waujaze na machafuko na udanganyifu." Kushughulikia hali hii kunahitaji kujenga upya uaminifu "ili kuhifadhi ubinadamu wetu," kwani mawasiliano potofu huzaa vikundi vya uadui badala ya jamii zinazounga mkono. "Tunaweza na lazima turudishe mawasiliano katika maana yake ya asili, karibu sana na ushirika. Kwa njia hiyo, "kuwasiliana kunamaanisha kutafuta, hata kwa ukaidi, uhusiano."
![]()
Wakati wa hotuba yake Dk. Paolo Ruffini,Mwenyekiti wa baraza la Kipapa la Mawasiliano (Emerson Fernandes, Jimbo la Tubarão)
Upweke na Kutengwa Kidijitali
Badala ya kujenga madaraja, Dk Ruffini aliesema, mawasiliano yanaweza kuwa chombo cha mgawanyiko, na upendeleo, yanapotumika kwa malengo yasiyoeleweka au ya kibinafsi. Lazima tutoe njia mbadala, aliongeza, "kwa wale wanaotumia hofu vibaya, wanaoendesha mahitaji halisi kwa faida ya kiitikadi au ya kibinafsi, na kuunda maadui wa kupigana na vita visivyokuwepo ili kujionyesha kama viongozi na waokozi." Kisha Mkuu wa Baraza la kipapa alizungumzia jambo la upweke unaosababishwa na muunganisho mkubwa na mlipuko wa habari. "Ukuaji wa majukwaa ya kidijitali umetuzoeza maisha yasiyogusana," alisema, "kuagiza chakula badala ya kula na marafiki, kununua vitabu mtandaoni badala ya kutembelea maktaba, kufanya kazi kwa mbali, kukaa nyumbani bila mawasiliano halisi ya kibinadamu na bila kujenga uhusiano na wafanyakazi wenzangu."
Kwa njia hiyo, kulingana na Dk. Ruffini, tunapoteza matukio ya ghafla, hata yasiyotarajiwa, na uwezo wa kujenga mahusiano nje ya miduara yetu ya kawaida. Maisha yetu ya kimwili yameanza kufanana na yale yetu ya kidijitali. Ulimwengu wa kutaka sifa za juu, uliogawanyika kati ya 'sisi na wao, na ambao ni mgawanyiko unaosababisha wanadamu kupoteza uwezo wa kuishi katika wingi na kukubali utofauti. "Ni juu yetu kuvunja hali hii ya kujidanyanya ili kujigundua upya. Dk Ruffini alisisitiza tena kwamba "ni kujigundua upya katika uzuri wa mazungumzo, wa kukutana, katika utafutaji mgumu wa ukweli, ambao si supu iliyotengenezwa tayari."
![]()
Fundisho la Dk.Ruffini wakati wa Semina ya Mawasiliano Rio de Janeiro (Emerson Fernandes, Jimbo Tubarão)
Jukumu la Msingi la Kanisa
Kanisa lina jukumu la msingi katika kuunda maoni ya umma, kwa sababu "linagusa mioyo na akili za watu na kukuza ujenzi upya wa uwezo wa mazungumzo "na kukutana ana kwa ana." Sinodi katika Kanisa inaelezea, kanuni halisi ya "kutembea pamoja." Lakini anaonya kwamba haipaswi kubaki dhana tu ya kufikirika: lazima iwe harakati halisi: chaguo maishani lazima iwe kati ya kutumikia ubinafsi wa mtu mwenyewe au matunda ya mazungumzo na jumuiya, "katika jikoni la supu ya umma ambapo sote tunajilisha wenyewe."
Semina ya Mawasiliano
Wakati wa shughuli zake za siku nne, Semina ya 12 ya Mawasiliano ya Jimbo Kuu la Rio ilitoa mikutano, meza za duara, na warsha kuhusu uinjilishaji wa kidijitali, ofisi ya vyombo vya habari, maadili ya mawasiliano, na uwepo wa Kikristo kwenye mitandao ya kijamii. Kulingana na mratibu wa tukio hilo, Padre Arnaldo Rodrigues, ambaye pia ni mkuu wa mawasiliano wa CNBB, lengo la mkutano huo lilikuwa kukuza mkutano kati ya imani, utamaduni, na uraia katika muktadha wa mawasiliano, kushughulikia changamoto za kijamii zilizopo. Ilikuwa zaidi ya mkutano: "Nafasi ya kusikiliza, kutafakari, na kuchukua hatua za pamoja ili kukabiliana na changamoto za kisasa za mawasiliano, teknolojia, maadili, na maisha ya umma."
Asante kwa kusoma makala haya. Ikiwa unataka kuendelea kupata taarifa mpya, tunakualika ujiandikishe kwa jarida letu:cliccando qui.