Tafuta

2025.11.21 Semina ya Kimataifa kuhusu Nostra Aetate  Chuo Kikuu cha Kipapa Santa Croce (Gianni Proietti) 2025.11.21 Semina ya Kimataifa kuhusu Nostra Aetate Chuo Kikuu cha Kipapa Santa Croce (Gianni Proietti) 

Miaka 60 ya Nostra Aetate:kutoka katika mbegu ya matumaini mti mkubwa umemea

Washiriki kutoka nchi mbalimbali na mapokeo mbalimbali ya kidini walikusanyika katika Kongamano la Kimataifa la"Nostra Aetate:Miaka 60 Baadaye"katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Msalaba Mtakatifu,Roma.Kardinali George Koovakad,Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Majadiliano ya Kidini na wazungumzaji pia,alisisitiza kwamba mazungumzo baina ya dini lazima yazingatie zaidi jukwaa la kimataifa na kwamba roho ya Nostra Aetate inabakia kuwa muhimu kwa juhudi za kisasa za kujenga amani.

Na Monika Stojowska,Ks na Paweł Rytel-Andrianik.

"Mazungumzo ya kidini yanahitaji nafasi zaidi katika nyanja ya kimataifa, katika utungaji sera, kwa sababu dini ina jukumu muhimu kutekeleza," Kadinali George Koovakad, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Majadiliano ya kidini alizungumza na Vatican News. Pia alikuwa miongoni mwa wazungumzaji katika Kongamano la "Nostra Aetate: Miaka 60 Baadaye," lililoandaliwa katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha ‘Santa Croce’- Msalaba Mtakatifu. Kongamano hilo lilfanyika tarehe 18–19 Novemba 2025 likiwa leta pamoja wawakilishi wa dini mbalimbali kutoka ulimwenguni kote. Siku hizo, wawakilishi wa Dini ya Kiyahudi, Uislamu, Ubudha, na Kanisa Katoliki walitafakari madaraka muhimu ya kidini na uwezo wa kugusa mioyo kuelekea amani na upatanisho. Washiriki pia walitembelea Sinagogi Kuu iliyoko katika sehemu ya zamani ya Wayahudi jijini  Roma na Msikiti Mkuu wa Roma. Ziara hizi zilitoa fursa kwa maombi na mazungumzo.

Dini inasukuma mioyo

Kongamano hilo lilikuwa la kitaaluma na lilihusisha mawasilisho ya wawakilishi wa Dini ya Kiyahudi, Uislamu, Ubudha, na Ukatoliki. Majadiliano yalilenga tamko la Nostra Aetate na ushawishi wake katika upatanisho. “Migogoro na matatizo mengine yote yanatokana na kukosekana kwa amani, haki na upatanisho. Viongozi wa kidini wana nafasi kubwa sana duniani, kwani wanaweza kuchangia katika kujenga amani,” alisema Prof Philip Goyret wa Chuo Kikuu cha Kipapa cha Msalaba Mtakatifu, mmoja wa waandaaji wa Kongamano hilo.

Takwimu kubwa za upatanisho

Hiroshi Munehiro Kiwano, mjukuu wa Nikkyō Niwano, ambaye, kwa mwaliko wa Papa Paulo VI, alichangia maendeleo ya Tamko la  Nostra Aetate, alishiriki kumbukumbu na ujumbe wa babu yake. "Wakristo huombea Wabudha, na Wabudha wanaombea Wakristo; tunahitaji siku nyingi kama hizi katika siku zijazo," alisema. Watu wengine muhimu waliochangia mawazo kuhusu Hati ya Mtaguso ya Nostra Aetate pia walikumbukwa. "Mkuu wa Kiyahudi,  Abraham Joshua Heschel, pamoja na Kardinali Augustin Bea, walichukua jukumu muhimu katika kukuza mazungumzo ya Kikristo na Kiyahudi wakati wa Mtaguso wa Pili wa Vatican," alibainisha Mkuu wa Kiyahudi  Ariel Stofenmacher,ambaye ni  Mkuu wa Seminari ya Kiyahudi ya Amerika Kusini  huko Buenos Aires na mwanzilishi wa Taasisi ya Chuo Kikuu cha Isaac Abarbanel. Kwa mawazo yake alisema kuwa  Kongamano lenyewe linajumuisha "ushahidi wa wazi wa uaminifu mkubwa ambao umesitawi kati ya Kanisa Katoliki na Dini ya Kiyahudi katika kipindi cha miaka sitini iliyopita. Uhusiano huu umekomaa kutokana na kujitolea kwa Mapapa na Wakuu wa Kiyahudi waliojitolea katika kukuza mazungumzo."

Huruma inaunganisha watu

Imam Nader Akkad wa Msikiti Mkuu wa Roma aliwasilisha kanuni za kimsingi za Uislamu na nafasi yake katika jamii. Alisisitiza kwamba neno "huruma” inayotahwa mara kwa mara katika Qur'an, pia ni mada kuu katika dini zingine na hutumika kama dhamana kati ya watu. Akijibu maswali wakati wa mjadala huo, alibainisha kwamba "kuna chuki nyingi kuhusu Uislamu kwa sababu watu wanaijua dini hiyo kupitia magazeti badala ya kuisoma Qur'ani." Aliwahimiza kwa hiyo washiriki kujifunza kuhusu kila dini kutoka vyanzo vyake.

Mazungumzo kama mbegu ya matumaini

Kongamano hilo lilihitimishwa kwa hotuba kuu ya Kardinali George Koovakad kuhusu hali ya kimataifa ya mazungumzo ya kidini. "Zaidi ya nusu karne iliyopita, mbegu ya matumaini ya mazungumzo baina ya dini ilipandwa. Uwepo wako leo ni ushuhuda kwamba umekua na kuwa mti mrefu wenye matawi mazuri. Roho ya Tamko la  Nostra Aetate inahitajika sana leo hii," alisema. Kardinali Koovakad pia alibainisha kuwa Nostra Aetate, iliyoendelezwa kwa ushirikiano wa wawakilishi wa mapokeo mbalimbali ya imani, ilianzisha juhudi endelevu kuelekea mazungumzo na kuwa hati muhimu ya umuhimu wa kimataifa. Kongamano hilo la kimataifa liliandaliwa na Chuo Kikuu cha Kipapa cha Msalaba Mtakatifu pamoja na Taasisi ya Chuo Kikuu cha Abarbanel (Buenos Aires), kwa ushirikiano na Kituo cha Abraham J. Heschel cha Mahusiano ya Kikatoliki na Kiyahudi katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Yohane Paulo II cha Lublin, na Ubalozi wa Argentina unaowakilishia nchi yao mjini Vatican.

Ikumbukwe Tamko la Nostra aetate”, ambayo inaadhimisha miaka 60 yake, ni Tamko kuhusu Mahusiano ya Kanisa Katoliki na Dini Zisizo za Kikristo. Hati hii iliyoidhinishwa na Mababa wa Mtaguso wa Pili wa Vatican na kutangazwa na Papa Paulo VI, inachukuliwa kuwa maandishi ya msingi ya mazungumzo na imani zingine za kidini. Chapisho lake, mnamo tarehe 28 Oktoba  1965, lilitanguliwa hata kabla ya kuandikwa kwake na mkutano: ule kati ya Papa Yohane XXIII na mwanahistoria wa Kiyahudi Jules Isaak, ambaye mnamo tarehe 13 Juni 1960, alimkabidhi Papa Denkschrift, mkusanyiko wenye ombi la kukuza maono mapya ya uhusiano kati ya Kanisa na Uyahudi. Ulikuwa wakati ambapo majeraha yaliyosababishwa na Vita vya Pili vya Dunia kwa wanadamu yalikuwa bado makubwa.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here

 

25 Novemba 2025, 10:32