Jukwaa la Wakatoliki la ‘Huduma ya Matumaini’ kuhusu Ustawi wa Akili lafunguliwa Roma
Vatican News
Jukwaa la huduma ya Matumaini linawaleta pamoja kuanzia tarehe 5 hadi 7 Novemba 2025, viongozi wa Kanisa, wataalamu, na wafanyakazi wa kichungaji kutoka ulimwenguni kote ili kuimarisha ushiriki wa kichungaji wa Kanisa Katoliki katika ustawi wa akili. Tukio hilo la kimataifa la siku tatu, lililoandaliwa kwa usaidizi wa Chama cha Kimataifa cha Wahudumu Wakatoliki wa Afya ya Akili na chini ya ufadhili wa Chuo cha Kipapa cha Maisha, linalenga kukuza usikilizaji, tafakari, na ushirikiano miongoni mwa watu binafsi na jumuiya zinazosindikiza, zinazokabiliwa na dhiki ya kisaikolojia, kijamii, na kiroho.
Katika hali ya vita, uhamisho, ukosefu wa usawa, na mgawanyiko wa kijamii, Jukwaa hilo linalenga kuongeza uelewa wa Kanisa kuhusu jinsi imani, jamii, na utunzaji wa kichungaji wenye taarifa zinavyoweza kukuza uponyaji na ustahimilivu. Jukwaa linasisitiza kwamba huduma ya kichungaji lazima iwe ya huruma na iliyoandaliwa—iliyojengwa katika ukaribu wa kibinadamu, na pia katika maarifa na utambuzi thabiti.
Jukwaa hili hatahili lilifunguliwa Jumatano alasiri kwa Misa ya hadhara katika Kanisa la Roho Mtakatifu huko Sassia, karibu na Uwanja wa Mtakatifu Petro, na kwendaa sambamba na nia ya maombi ya kila mwezi ya Papa Leo XIV, mwezi huu ikizingatia kuzuia kujiua.
Misa hiyo ilifuatiwa na Meza ya Mduara wa Kichungaji katika ukumbi wa mkutano ulio karibu, ikionesha tafakari na ushuhuda wa pamoja kuhusu kuzuia kujiua na utunzaji wa kichungaji. Lengo ni kuongeza uelewa, kukuza sala ya pamoja, na kualika ushiriki wa umma katika roho ya mshikamano na maombezi. Jukwaa la mwaliko la siku mbili pekee linawaleta pamoja takriban washiriki 50, wakiwemo mapadre, watawa, wafanyakazi wa kichungaji walei, wataalamu wa afya ya akili, na watu binafsi wenye uzoefu wa maisha.
Vipindi hivyo vinafuatiwa na tafakari ya kitaalimungu na ufahamu wa kitaaluma, kuhimiza mazungumzo ya wazi, kujifunza kwa pamoja, na kushiriki mbinu za vitendo kutoka katika miktadha mbalimbali ya kichungaji, kama vile maeneo ya migogoro, jumuiya za wahamiaji, shule, na parokia.
Jukwaa hilo pia limeakisiwa na pia uzinduzi wa hati mpya kutoka kwa Baraza la Kipapa la Kukuza Maendeleo fungamani ya Binadamu, yenye kichwa: "Afya ya Akili na Usindikizaji wa Kichungaji katika Muktadha wa Mgogoro wa Kibinadamu."
Mada kuu ni pamoja na: "Miktadha ya Dhiki na Ustahimilivu", kuelewa jinsi mateso na ustahimilivu vinavyoonyeshwa katika hali halisi za kijamii, kiutamaduni, na kijiografia leo hii; "Uzoefu wa Maisha na Mazoea ya Kichungaji," kuchunguza jinsi huduma za kichungaji zinavyokuza muunganisho na usindikizaji katika parokia, shule, na jumuiya; "Kuwatunza Walezi na Huduma ya Uwepo”katika kuunganisha maarifa ya afya ya akili katika malezi ya kichungaji na kuhakikisha ustawi wa wale wanaohudumu; na, "Taalimungu, Anthropolojia, na Swali la Ustawi wa Akili”katika kutafakari maana ya ustawi wa akili kwa kuzingatia taalimungu Katoliki, kiroho, na anthropolojia ya binadamu.
Huduma ya Matumaini inatafuta kuwa zaidi ya ubadilishanaji wa kitaaluma au kitaaluma na ni mkutano wa kiroho na kichungaji ulioundwa ili kufufua dhamira ya Kanisa ya usindikizaji. Jukwaa linawaalika washiriki kutambua jinsi Kanisa linavyoweza kuendelea kukuza uaminifu, utu, na ushirika, hasa miongoni mwa wale wanaoteseka kutokana na kutengwa, kiwewe, au kukata tamaa. Pia linasisitiza umuhimu wa kuunda wahudumu ambao wanaweza kuunganisha uelewa wa kisaikolojia na kina cha kiroho katika huduma yao.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Bonyeza hapa tu: Just click here