Tafuta

2024.09.24 Mkutano wa vyombo vya habari kuhusu WYD ya Seoul 2027 2024.09.24 Mkutano wa vyombo vya habari kuhusu WYD ya Seoul 2027  (Dicastero per i laici, la famiglia e la vita)

Sala ya Siku ya Vijana(WYD)kuelekea Seoul:"Jipeni moyo! Nimeushinda ulimwengu"

Katika Sherehe ya Kristo Mfalme,ilitolewa sala rasmi itakayosindikiza vijana wakati wa Siku ya Vijana Duniani(WYD),iliyopangwa kufanyika nchini Korea Kusini kuanzia tarehe 3 hadi 8 Agosti 2027."Kila mtu agundue tumaini lililo katika wito wako wa ujasiri,akielewa kwamba msalaba wa upendo na msamaha ndio ushindi wa kweli juu ya ulimwengu."

Vatican News

Mama Kanisa akiwa anaadhimisha Sherehe ya Kristo Mfalme, Dominika tarehe 23 Novemba 2025, Kamati ya Ndani ya Nchi  kuhusu  Siku ya Vijana Ulimwenguni (WYD) ilichapisha sala ya Kuongoza vijana katika kuelekea kilele hicho ambayo inaongozwa na kifungu cha Injili ya Yohane: “Jipeni moyo! Nimeushinda ulimwengu.” Ni sala itakayowaongoza  vijana na jumuiya nzima ya kikanisa katika safari ya kuelekea Siku ya Vijana Duniani ijayo huko Seoul nchini Korea Kusini kunako 2027, iliyopangwa kufanyika kuanzia Agosti 3-8. Sala hiyo mekusudiwa kama ilivyoelezwa katika taarifa,  kuwa “mwaliko kwa vijana kuamini ushindi wa kudumu wa Kristo na kuishi Injili ya matumaini, umoja, na huruma katika wakati uliojaa changamoto na mabadiliko makubwa.” Sala hiyo kwa WYD inaambatana na picha ya Papa katika Jubilei ya Vijana huko Tor Vergata, Roma.

WYD Seoul
WYD Seoul

Kuna mada tano zilizomo katika sala hiyo: shukrani kwa wito wa Mungu wa ulimwengu wote na kwa upendo wake usio na masharti kwa kila kijana; kujikabidhi kwa Baba anayewakusanya watoto wake katika ushirika na umoja; ushindi wa mwisho wa Kristo, anayemwita kila mtu kuwa na ujasiri na kujitolea, akitambua katika Msalaba ushindi wa upendo na msamaha; wito wa Roho Mtakatifu, "Mwali wa Upendo," kumbukumbu ya uhai wa asili ya Kanisa huko Korea, ya kuuawa kishahidi, na matunda ya amani, upendo, na ukweli ambayo yameunda historia yake; kujitolea kusafiri kama Kanisa la sinodi, mhujaji katika kusikiliza, kupambanua, na uwajibikaji wa pamoja. Sala inamalizika kwa maombezi ya Bikira Maria, mlinzi wa Korea, na wa watakatifu walinzi wa WYD Seoul 2027.

Sala ya Sinodi

Mojawapo ya mambo mapya ya maandishi haya yanahusu asili yake: mwanzoni ilianzishwa na maaskofu wa eneo hilo lakini kisha ikageuka kuwa safari ya pamoja ya kusikiliza, kusali na utambuzi. Mafungo ya siku mbili, yaliyoandaliwa kwa miezi miwili na watu wa kujitolea, mapadre, wafanyakazi, na wageni vijana wadogo wanaoishi Seoul, yalijumuisha katekesi ya mada, ibada ya Ekaristi, neno la Mungu, nyakati za sala ya kibinafsi na ya pamoja, na vikao vilivyopangwa vya kuandika na kurekebisha maandishi. Mafungo  hayo yalihudhuriwa na watu 77, wakiwakilisha utofauti wa Kanisa nchini Korea: vijana waliotumwa na majimbo na taasisi za kitawa, vijana kutoka tamaduni zingine, mapadre, wanaume na wanawake watawa, na wanachama wa kamati ya maandalizi. Baada ya kuchunguza rasimu ya kwanza, maandishi hayo yalipitishwa kwa Mkutano wa Maaskofu wa Korea na baadaye kupitishwa na Baraza la Kipapa la Walei, Familia, na Maisha.

Kugundua Upya Sinodi

"WYD Seoul 2027 itaadhimishwa wakati ambapo Kanisa litaitwa kugundua upya sinodi halisi," alisema Askofu Mkuu Peter Soon-taick Chung, rais wa Kamati ya Maandalizi mahalia. Korea, ikiwa na historia yake iliyojaa utafutaji wa ukweli, upendo, na amani, inawapatia vijana nafasi ya kuhoji ujasiri unaohitajika kushuhudia maadili haya kwa mshikamano." Kardinali Kevin Farrell, Mwenyekiti wa  Baraza la Kipapa la Walei, Familia, na Maisha, alibainisha kuwa ni bahati maalum ya kuchapisha sala katika Sherehe ya Kristo Mfalme. "Hii,"siku ambayo Makanisa yote maalum huadhimisha WYD kila mwaka katika ngazi mahalia. Kwa hivyo ninawaalika vijana kuungana katika ushirika, katika jumuiya zao na pamoja na maaskofu wao, wakiinua pamoja kilio cha amani, udugu, na matumaini ambayo ulimwengu unahitaji sana."

Sala rasmi ya WYD Seoul 2027

Bwana mpendwa wa vijana wote, Tunakushukuru kwa kutuita kwa upendo wako na huruma yako isiyo na kikomo.

Baba yetu, tunajikabidhi kwako. Vijana ulimwenguni kote waweze kufarijiwa katika kukumbatiwa na Kanisa lako na kushiriki kwa undani furaha ya ushirika na umoja.

Bwana Yesu Kristo, unashinda Ulimwengu, sasa na milele. Kila mtu agundue tumaini lililo katika wito wako wa ujasiri, akielewa kwamba msalaba wa upendo na msamaha ndio ushindi wa kweli juu ya ulimwengu.

Ee Roho Mtakatifu, Mwali wa Upendo, kwa mkono wako wa ajabu ulipanda mbegu za imani huko Korea.

Washa mioyoni mwetu mwali wa imani ya mashahidi wa Kikorea, utufanye wanafunzi wanaoishi Injili ya amani, upendo, na kweli.

Bwana, tunaomba kwamba kupitia hija hii ya Siku ya Vijana (WYD)tuweze kusikilizana, kutambua mapenzi yako na kuwa Kanisa la kisinodi, tukitembea pamoja na watu wote wa Mungu. Amina

Mama yetu wa Huruma  na Amani, utuombe.

Watakatifu Walinzi wa WYD Seoul 2027 waombee vijana wote.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here

 

24 Novemba 2025, 13:07