Kongamano ya Ibada ya Kina,Semeraro:Tafakari husababisha upendo
Na Daniele Piccini - Vatican.
"Katika enzi ambayo usikivu kwa Mungu unakosekana, katika ulimwengu ambapo lugha kame ya sayansi na teknolojia inatawala, Ibada ya Kina huchukuliwa na kutamaniwa kama rasilimali inayoweza kushirikisha akili na mtu, roho na mwili, roho na hisia." Kwa maneno haya, Kardinali Marcello Semeraro, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Kuwatangaza Watakatifu, alifungua alasiri ya Jumatatu tarehe 10 Novemba 2025, Kongamano linalojikita na "Ibada ya kina, Matukio ya Ibada ya kina na Utakatifu" katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Urbaniana.
Kongamano hilo, ambalo kwa uzuri na kimaudhui linakamilisha matoleo mengine mawili yaliyopita ambayo yalijikita juu ya "utakatifu leo," katika "kipimo chake cha kijumuiya," na "ushuhuda na kujitoa maisha, ambalo lilifunguliwa katika Ukumbi Mkuu wa Chuo cha Kipapa cha Urbaniana hadi Jumatano, tarehe 13 Novemba 2025 ambapo siku ya Alhamisi , washiriki watapokelewa na Papa Leo XIV katika Ukumbi wa Clementina. Kardinali alisisitiza kwamba utakatifu, ambao kimsingi unajumuisha upendo kwa Mungu na jirani, unaweza kupatikana kupitia njia tofauti na kwa hivyo sio lazima uambatane na neema za ajabu, za fumbo, au za karama, kama vile kutafakari." Kardinali Semeraro alimnukuu Papa Francisko, ambaye mara nyingi alirudia kwamba "wale wanaojua kutafakari hawaketi tu bila kufanya kazi, bali huanza kufanya kazi."
Kwa kifupi, "tafakari husababisha vitendo." Kwa hivyo maisha ya upendo na maisha ya kutafakari yanakamilishana, Kardinali Semeraro alirudia, akimnukuu Mtakatifu Vincent wa Paulo: "Maisha ya vitendo humlisha mtu anayetafakari, na hii, kwa upande wake, ndiyo roho ya maisha ya vitendo." Hatimaye, Kardinali, akiwatakia wazungumzaji na hadhira "kazi njema," alitumaini kwamba mawasilisho ya mkutano yangesaidia sio tu "kufafanua maswali mengi haya yanayohusu mada ngumu kama hizo," lakini pia "kutia moyo uzoefu wetu wa Mungu."
![]()
Alhamisi washiriki wa Kongamano watakutana na Papa Leo XIV katika Ukumbi wa Clementina
Mipaka ya Ibada ya Kina Kikristo
Alasiri ya kwanza ya Kongamano ilitoa ufahamu wa kushangaza kuhusu ibada ya kina, ambayo, katika kiini chake cha ndani kabisa, kama wasemaji wawili wa kwanza wa Kongamano la siku tatu huko Urbaniana walivyoelezea, ni uhusiano na huduma kwa wengine. "Uwezo wa kujenga mahusiano ya watu wazima ni mojawapo ya matokeo ya uzoefu wa ibada ya kina, kwani kumkaribisha Mwingine kabisa katika maisha ya mtu hutafsiriwa kuwa kuwakaribisha wengine." Wazo hili lilikuwa msingi wa hotuba ya uzinduzi ya Askofu Mkuu Felice Accrocca, wa Jimbo Kuu la Benevento, yenye kichwa: "Fumbo: Vipengele Maalum na Masuala yenye matata."
Askofu Mkuu huyo alibishana, akifafanua awali mipaka ya ibada ya Kina ya Kikristo, kwamba haiwezi kamwe kupita uzoefu wa Ufunuo, unaowakilishwa na "fumbo la Mungu wa Yesu Kristo." "Mungu wa Utatu, aliyefunuliwa naye, ndiye mpaka wa Ibada ya Kikristo, na unaweza tu kuwa ndani yake," aliongeza. "Uzoefu wa Ibada ya kina ya Kikristo," Askofu Mkuu Accrocca alisisitiza, kwa hivyo, kila wakati hutokea "ndani ya imani." Kwa hivyo, mtu wa mafumbo "hajui chochote zaidi ya Wakristo wote wanavyoweza kujua; anakijua tu kwa njia tofauti," aliongeza Askofu Mkuu wa Benevento, akimnukuu mwanatheolojia Giovanni Moioli, mtaalamu wa mafumbo na mambo ya kiroho.
Wakati wa kutoa mada mchana katika semina huko Chuo Kikuu cha Kipapa, Urbaniana
Muungano na Mungu katika Maisha ya Kawaida: Mfano wa Maria
"Kwa hivyo, ikiwa matukio ya Ibada ya Kina hayaleti ukamilifu na mtu hawezi kuishia hapo, utimilifu wa fumbo haupaswi kupatikana si wakati matukio kama hayo yanajidhihirisha, bali katika maisha yanayopatana kabisa na Mungu," Askofu Mkuu huyo alisema. Katika hili pia, kawaida ya maisha ya Maria wa Nazareti ni mfano, kwani katika maisha yake "muungano kamili na Mungu unafikiwa, bila kutaja fenomenolojia kama ile ambayo tumezoea kuifafanua kama fumbo."
Uhusiano na Mwingine Unaofunguka kwa Wengine
Ikiwa uzoefu wa Ibada ya kina ya Kikristo hauwezi kuwepo isipokuwa ndani ya imani, kwa kuwa si "kizuizi," basi, "hasa katika Ukatoliki, unaweza kuwepo tu ndani ya imani ya Kanisa." Mtakatifu Francis wa Assisi mwenyewe, Askofu Mkuu Accrocca alikumbuka, "katika uzoefu wake wa zawadi ya Ibada ya Kina " na ufunuo, "haipuuzi upatanishi wa kanisa."
Kwa hivyo, anamruhusu Papa kuthibitisha "aina hiyo ya maisha" aliyofunuliwa na Mungu. Ikiwa imani ya mafumbo ni "umoja wa Utatu ndani ya mtu" na "Utatu ni uhusiano wa kwanza kabisa," basi, Askofu Mkuu alihitimisha, "muungano wa mafumbo unaweza tu kuimarisha uhusiano wa mtu na wanadamu wenzake."
![]()
Mtakatifu Francis wa Assisi akihubiria ndege (Mongolo1984)
Padre Manzi:Katika Biblia,Ibada ya kina Si Uzoefu wa Kibinafsi
Ibada kuu ya kina ya Kikristo si kutoroka, bali ni utume. Wazo hili lilikuwa lengo la hotuba ya Padre Franco Manzi, yenye kichwa: "Manabii, Mwonaji Yohane, na Mtume Paulo. Ufahamu wa Uzoefu wa Kiroho Wenye Sifa za Ibada ya Kina, unaothibitishwa katika Biblia," ambayo ililenga mizizi ya kibiblia ya uzoefu wa Ibada ya Kina
Akifuatilia njia kupitia Maandiko, Padre Manzi, profesa wa Agano la Kale na Jipya katika Kitivo cha Taalimungu cha Kaskazini mwa Italia huko Milano, alionesha kwamba ufunuo, katika utamaduni wa kibiblia, si uzoefu wa pekee au wa kibinafsi, bali ni kukutana na Mungu ambao unakuwa neno na wajibu, kwa kuwa wale wanaotafakari Umungu wanaitwa kuusimulia. "Ufunuo," msomi wa Biblia alisema, "unakuwa historia na jamii." Manabii wa Agano la Kale ndiyo mfano mkuu wa hili. Kuanzia Isaya hadi Yeremia, maono ya Mungu daima hutafsiriwa kuwa agizo, mara nyingi machungu, la kutangaza na kukemea. "Ufunui ni jeraha na agizo," Manzi alielezea, akisisitiza kwamba ibada ya Kina ya kweli haijifichi katika ukimya, bali hulibadilisha kuwa maneno ya unabii.
Zawadi ambayo inakuwa huduma na kuunda mashahidi
Agano Jipya linatimiza uzoefu huu katika watu wawili wenye mfano: Yohane na Paulo. Yule wa kwanza, "mwonaji wa Ufunuo," anatafakari "mbingu mpya na dunia mpya," akiipa Kanisa linaloteswa maono ya matumaini. Huyu wa mwisho anaishi fumbo lililounganishwa kikamilifu na Kristo: "Si mimi tena ninayeishi," anaandika Paulo katika Barua yake kwa Wagalatia, "bali Kristo anaishi ndani yangu." Katika Mtume kwa Mataifa, ushirika na Mungu unakuwa kitendo, utume, na upendo. Padre Manzi alisisitiza zaidi jinsi fumbo halisi la Kikristo lisivyojikita tu kwenye kutafakari, bali hujifungulia kwa huduma na ushuhuda. Fumbo, katika mizizi yake ya kibiblia, haliukimbii ulimwengu, bali huubadilisha. "Katika ufunuo wa kibiblia," msomi alisema, "maono ya Mungu si fursa ya wachache, bali ni zawadi inayounda jumuiya ya mashahidi."
Kile ambacho Padre Manzi alihitimisha kwa kuita "upatikanaji wa uhakika wa uhusiano kati ya imani ya mafumbo na utakatifu" ni kwamba "kulingana na ufunuo wa Agano Jipya, si kila Mkristo ni fumbo wala haitwa na Mungu kuwa mmoja. Lakini kila Mkristo ana wito wa kimungu wa kuwa mtakatifu." Kwa hivyo, msomi huyo wa Biblia alisema mwishoni mwa uwasilishaji wake, mtu si Mkristo halisi "kwa sababu tu anapitia matukio ya ajabu ya mafumbo. Lakini hali halisi ya kuwa fumbo halisi ni kwamba mtu anaishi kimsingi kama Mkristo halisi."
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku:Just click here