Tafuta

2025.10.27 Nembo ya Ziara ya Uturuki na Lebanon ya Papa Leo XIV. 2025.10.27 Nembo ya Ziara ya Uturuki na Lebanon ya Papa Leo XIV. 

Ziara ya Papa ya"Uturuki ni fursa ya kufufua roho ya Mtaguso wa Vatican II"

Askofu Paolo Bizzeti,aliyekuwa Mwakilishi wa Kitume huko Anatolia,alizungumza na Radio Vatican kuhusu Ziara ijayo ya kitume ya Papa kwenda Urutuki na ambapo pia atatembelea"msikiti" wa jumuiya tofauti za kidini.Papa atakuwa Uturuki kuanzia,kuanzia tarehe 27 hadi 30 Novemba 2025.

Na Daniele Piccini – Vatican.

Askofu Paolo Bizzeti, ambaye alihudumu kama rais wa Caritas Uturuki kuanzia 2019 hadi siku chache zilizopita, bado anathamini ushirikiano kati ya dini kama mojawapo ya uzoefu wenye maana zaidi wa miaka yake mingi nchini humo.  Askofu huyo, ambaye alikuwa Mwakilishi wa  Kitume wa Kilatini huko  Anatolia kuanzia 2015 hadi 2024, anajua eneo hilo la Uturukki ambapo alissisitiza kwamba, “Katika miezi baada ya tetemeko la ardhi, tulifanya kazi pamoja, tukivunja kuta za zamani za mgawanyiko na kuonesha kwamba aina ya kina zaidi ya mazungumzo kati ya dini, kama Baba Mtakatifu  Francisko alivyokuwa akisema, ni mazungumzo ya maisha, hasa katika kuwahudumia maskini." Ni katika mahojiano na Radio Vatican, akishiriki tafakari na matumaini yake kabla ya Ziara  ijayo ya kitume ya Papa Leo XIV kwenda Uturuki, ambapo ziara itakayompeleka Ankara, Istanbul, na İznik, ambayo hapo awali ilijulikana kama Nicea, kwa ajili ya kumbukumbu ya miaka 1700 ya Mtaguso wa  kwanza la Kiekumeni.

Kuanzia tarehe 27 hadi 30 Novemba, Papa Leo XIV atafanya ziara yake ya kwanza ya kitume. Atakwenda Uturuki ambapo Wakristo ni wachache. Kwa maoni yako, ziara hii ina umuhimu gani kwao?

Kutembelea kundi ana kwa ana na kupeleka ukaribu wa Mchungaji Mwema,  hiyo ndiyo kusudi la safari hizi za kipapa. Uturuki ni nchi muhimu sana, si tu kwa sababu ya zamani zake, Ukristo kama tunavyoujua ulizaliwa Antiokia,huko Orontes, ambayo ni Uturuki ya sasa, lakini pia kwa sababu ya uhai wa maisha ya Kikristo leo hii. Uturuki ni aina ya maabara, ambapo hata Kanisa la Kilatini lazima liwepo, kikamilifu na kwa unyenyekevu.

Papa pia ataadhimisha kumbukumbu ya Mtaguso wa Nicea

Ziara ya Papa pia ni fursa kubwa ya kiekumene, na kumbukumbu ya Nicea itasaidia kufufua roho iliyowachochea Mababa wa Mtaguso kuonesha imani katika masharti na aina mpya, na kutafuta kinachounganisha, kama Papa Mtakatifu Yohane XXIII alivyohimiza. Hiyo ni kazi ambayo lazima tuanze upya kila wakati.

Ni aina gani ya mandhari ya kidini ambayo Papa Leo atakutana nayo atakapowasili?

Uturuki ni kama picha ya uzuri (mosaic). Kuna Uislamu wa kisiasa, Uislamu wa kidini wa kijadi, mkondo wa fumbo wa Sufi, harakati za Alevi,Wasioamini, au aina ya (deism)yaani inayobali kuwepo kwa muumba kwa msingi wa akili lakini ikakataa imani katika mungu wa ajabu anayeingiliana na wanadamu, kwa wengi  na kisha, bila shaka, Wakristo wachache muhimu. Hata hivyo, kazi ya uchungaji ya Wakatoliki imepunguzwa sana na sheria na desturi zinazofanya iwe vigumu kujenga makanisa, vituo vya vijana, au kumbi za kiutamaduni. Kila kitu hutokea ndani ya Parokia chache, zilizoanzishwa karne moja iliyopita chini ya Mkataba wa Lausanne.

Mnamo tarehe 6 Februari 2023, tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 7.8 kwenye kipimo cha Richter lilipiga maeneo ya mpaka kati ya Sria na Uturuki na kusababisha, kulingana na ripoti, zaidi ya majeruhi 50,000. Mwitikio wa Caritas Uturuki, licha ya matatizo makubwa, ulikuwa mkubwa, wa kujitolea na wenye ufanisi. Uzoefu ulikuwaje?

Idadi halisi ya vifo inaaminika kuwa kubwa zaidi, na mamia ya maelfu walihamishwa. Ilikuwa janga kubwa lililofichua udhaifu wetu wa kibinadamu, na athari zake bado zina uzito mkubwa kwa jamii maskini zaidi. Kwetu sisi huko Caritas, ilikuwa jaribio lililotulazimisha kukua haraka - bila matatizo na makosa. Lakini tulifurahi sana kutoa mchango wetu, kushirikiana na mashirika ya misaada ya ndani na ya kitaifa, na kuitwa na kushukuru rasmi huko Ankara. Tulitambuliwa, jambo ambalo halijawahi kutokea hapo awali, kama shirika linalowasaidia watu bila ubinafsi, bila ubaguzi. Kama Wakatoliki, tunajivunia kutoa mchango wetu mdogo, kwa kutumia vyema msaada uliofika kwa ukarimu kutoka pembe nne za ulimwengu.

Je, kazi ya Caritas Uturuki, ambayo huwasaidia Waislamu na Wakristo bila ubaguzi, ina athari chanya katika mahusiano kati ya makundi hayo mawili ya kidini?

Katika miezi iliyofuata tetemeko la ardhi, tulifanya kazi pamoja, tukivunja kuta za zamani za mgawanyiko na kuonesha kwamba aina ya kina zaidi ya mazungumzo kati ya dini mbalimbali, kama Papa Francisko alivyosema, ni mazungumzo ya maisha, hasa katika kuwahudumia maskini.

Unafikiri ziara ya kitume ya Papa itakuwa na athari gani kwa wale wanaofanya kazi kwa Caritas Uturuki?

Kwa wafanyakazi wote wa Caritas, itakuwa tukio zuri la kuhisi sehemu ya Watu wa Mungu - umoja katika huduma na katika kuwatunza walio hatarini zaidi, kama Wakristo walivyokuwa siku zote, wakimfuata Yesu, mtumishi wa wote.

12 Novemba 2025, 18:02