Tafuta

 Alessandro Gisotti Rais mpya wa EBU katika Mkutano mkuu wa 2025 huko Geneva Uswiss. Alessandro Gisotti Rais mpya wa EBU katika Mkutano mkuu wa 2025 huko Geneva Uswiss. 

Alessandro Gisotti ni Rais Mpya wa Radio News Group ya EBU

Naibu Mkurugenzi wa Uhariri wa Vatican achukua nafasi ya Mwandishi wa Habari wa Ujerumani,Stephanie Pieper wa Rundfunk Berlin-Brandenburg:"Nina uhakika kwamba radio inabaki kuwa muhimu katika enzi ya Akili Unde kwa sababu inatoa taarifa za kuaminika na muunganisho na jamii ambayo algoriti haziwezi kuchukua nafasi yake."

Vatican News.

Dk. Alessandro Gisotti, Naibu Mkurugenzi wa Uhariri wa Vyomvo vya habari Vatican, amechaguliwa kuwa Rais wa Kikundi cha Habari za Radio na Sauti(RANG) cha Umoja wa Watangazaji wa Ulaya(EBU), ambapo anawakilisha Radio Vatican. Yeye anarithi mwandishi wa habari wa Ujerumani, Stephanie Pieper wa Rundfunk Berlin-Brandenburg. Dk. Gisotti alianza kufanya kazi katika kituo cha utangazaji cha kipapa mnamo mwaka 2000 na amekuwa mwanachama wa RANG tangu 2021. Kikundi hiki cha Habari za Radio na Sauti huleta pamoja maadili na mbinu bora kuhusu masuala ya uhariri na maadili katika sekta ya radio na sauti katika ngazi ya Ulaya. Huunganisha utaalamu wa wakurugenzi, waandishi wa habari, na wazalishaji kwa manufaa ya wanachama wote wa EBU. Hukutana mara kadhaa kwa mwaka ili kujadili masuala makubwa ya sasa, kwa kuzingatia hasa athari za teknolojia mpya kwenye habari za Ulaya. Radio  Vatican ni mwanachama mwanzilishi wa EBU, ambayo mwaka huu 2025  inaadhimisha miaka 75 yake na kuwaleta pamoja watangazaji 113 wa umma kutoka nchi 56.

Neno ya EBU
Neno ya EBU

"Nimekuwa na fursa ya kubadilishana mawazo na uzoefu na wenzangu"

"Nimeheshimiwa sana," alisema Dk. Gisotti, "kuwa rais mpya wa Kikundi cha Habari za Radio na Sauti za EBU, ambapo kwa miaka kadhaa nimepata fursa ya kubadilishana mawazo na uzoefu na wenzangu kutoka watangazaji wakuu wa radio za umma barani Ulaya. Nina hakika kwamba radio inabaki kuwa muhimu katika enzi ya akili unde(AI) kwa sababu inatoa taarifa za kuaminika na muunganisho na jamii ambao algoriti haziwezi kuchukua nafasi. Hii ni thamani kubwa leo hii, wakati ambapo tunashuhudia kuenea kwa habari za uongozi na taarifa potofu, hasa kwenye majukwaa ya mtandaoni."

Asante kwa kusoma makala haya. Ikiwa unataka kuendelea kupata taarifa mpya, tunakualika ujiandikishe kwa jarida kwa kubofya hapa: Just click here

15 Desemba 2025, 20:35