Kitabu:“Kubadli Afrika na kubadili namna ya kuitazama,”siyo tu uhamiaji
Na Angella Rwezaula – Vatican.
"Afrika ni nini? Swali hili lilikuwa lengo la majadiliano wakati wa uwasilishaji wa kitabu chenye kichwa: kubadili Afrika ni kubadili namna ya kuitazama:"Mabadiliko ya Afrika Magharibi - Sio uhamiaji pekee,"Utendaji wa Maadili, kilichohaririwa na Askofu Samuel Sangalli, Mwanzilishi na Rais wa Mfuko wa Sinderesi, Katibu Msaidizi wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji, wa Kitengo cha Uinjilishaji wa Kwanza na Makanisa Mapya Maalum na Dkt. Antonella Piccinin, mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregorian.
Kitabu hichi kiliwasilisha mjini Roma tarehe 2 Desemba 2025 alasiri pamoja na michango wa hotuba kutoka kwa Askofu Fortunatus Nwachukwu, Katibu Mkuu Baraza la Kipapa la Uinjilishaji, Kitengo cha Uinjilishaji wa Kwanza na Makanisa Mapya Maalum; Dk. Abdellah Redouane, Katibu Mkuu wa Kituo cha Utamaduni wa Kiislamu cha Italia; Lucio Caracciolo, Mkurugenzi wa jarida la Limes la kijiografia la Italia na Askofu Sangalli.
"Swali lililoulizwa kutokana na mapungufu ya mtazamo wa Magharibi, ambayo mara nyingi humruhusu mtu kuona mambo kutoka upande mmoja tu," Askofu Sangalli alibainisha katika maelezo yake kuwa "Ni jambo la ajabu kufikiria hatuna mawazo ya awali, lakini jambo muhimu ni kwamba yasiwe ya ubaguzi," aliendelea Rais wa Mfuko wa Sinderesi.
Kama Caracciolo alivyosema: "Tatizo ambalo sisi Wazungu tunalo na Afrika ni kwamba tunalidharau. Tunaliona kwa sauti ya ubora unaotokana na historia tunayodhani ni ya kipekee kwetu. Kitendo cha kuzungumzia Afrika kama taifa zima lililoungana kinatupotosha," alisisitiza mkurugenzi wa Limes, kwamba kuna "Waafrika wengi. Kiukweli, ni Waafrika wanaojua mengi zaidi kuliko sisi Wazungu. Maono haya yasiyo na ulinganifu ni tatizo kubwa kwa sababu huwezi kuanza mazungumzo kuanzia mtazamo mmoja," Caracciolo alisisitiza
Tatizo hili linaakisiwa na jinsi Wazungu wanavyoona demokrasia za Afrika, wakizilinganisha na mfumo wa demokrasia wa Magharibi (ambao pia uko katika mgogoro, alibainisha Caracciolo, akimaanisha kupungua kwa idadi ya wapiga kura), wakishindwa kuelewa kwamba kunaweza kuwa na mifumo tofauti na yao. Na hii ni kikwazo zaidi cha uelewano wa pande zote mbili. Mkurugenzi wa The Limes alimalizia kwa kusisitiza jinsi mgogoro wa Marekani na kupungua kwa ushawishi wa Ulaya barani kumeipatia nafasi mawazo ya Kiafrika, ambayo, hata hivyo, yana hatari ya kugongana, na pia kuruhusu wahusika wasio wa Magharibi kupenya Afrika, kila mmoja akiwa na maslahi yake mwenyewe.
Mada ya ushawishi wa nguvu za zamani na mpya barani ilichukuliwa na kupanuliwa na Dk. Abdellah Redouane, ambaye alikumbuka maovu ya ukoloni lakini hakuficha hatari zilizomo katika sera mbalimbali za nguvu zisizo za Magharibi ambazo zimejiimarisha katika maeneo mbalimbali ya Afrika.
Afrika inatendewa kama uwanja wa vita na mgodi
"Afrika leo inatendewa kama uwanja wa vita na mgodi ambapo kila mtu anatenda kama fisi ili kunyakua kipande cha utajiri wake," alisisitiza Mtukufu Askofu Fortunatus Nwachukwu. "Kama Waafrika, lazima tuwe waangalifu tusiunge mkono taswira hii mbaya ya bara letu." Akirudi katika kichwa cha kitabu, Askofu Mkuu Nwachukwu alisema kwamba Afrika lazima ichukue umbo jipya, lakini wakati huo huo, mtazamo wa wale wanaolitazama bara lazima pia ubadilike.
"Mbadiliko wa Afrika una pande mbili: mabadiliko yanayopaswa kutokea katika nchi za Afrika na mabadiliko katika mtazamo wetu wa Afrika." Mabadiliko haya katika mtazamo ni muhimu zaidi kushughulikia suala la ukabila (mchango wa Askofu Nwachukwu katika juzuu): kutowaangalia wengine tena kulingana na asili yao, bali kulingana na mtazamo wa Mungu kwetu; kama watoto wake, kwa hivyo lazima tujione kama kaka na dada bila ubaguzi wa rangi au kabila.
Kwa hivyo, utambulisho wa kweli, katika hitimisho Askofu Sangalli, alisema ni "wale ambao wako katika mazungumzo kila wakati." Changamoto ambayo haihusishi Afrika pekee bali ubinadamu wote.