Jubilei,kufungwa kwa Milango Mitakatifu ya Basilika za Kipapa,kwanza ya Maria Mkuu
Vatican News
Mlango Mtakatifu wa Basilika ya Mtakatifu Maria Mkuu utakuwa wa kwanza kufungwa kati ya Basilika za kipapa wakati wa Jubilei ya 2025. Sherehe hiyo itafanyika Siku ya Noeli saa 11:00 jioni na itaongozwa na Mkuu wa Basilika ya Liberia, Kardinali Rolandas Makrickas. Kufuatia hili, Jumamosi, Desemba 27, utafungwa Mlango Mtakatifu wa Basilika ya Mtakatifu Yohane, Lateran. Ibada imepangwa kufanyika saa 5:00 asubuhi na itaongozwa na Mkuu wa Kanisa hilo Kardinali Baldo Reina. Siku inayofuata, Dominika tarehe 28 Desemba 2025, Mkuu wa Basilika ya Mtakatifu Paulo Nje ya Kuta, Kardinali James Michael Harvey, ataongoza ibada kama hiyo ya kufunga Mlango Mtakatifu.
Sherehe za Kufunga Mlango Mtakatifu wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria Mkuu
Mlango Mtakatifu wa Basilika ya Liberia(Mtakatifu Maria Mkuu), uliofunguliwa tarehe 1 Januari 2025, umewakaribisha mahujaji na waamini zaidi ya milioni ishirini kupitia milango yake. Tarehe ya kufungwa haikuchaguliwa kwa bahati mbaya: Mtakatifu Maria Mkuu kiukweli, ni Basilika ya Noeli Takatifu, mlinzi wa masalio ya Kitanda Kitakatifu ambapo Mtoto Yesu akiwa mchanga alipumzishwa. Kwa hiyo Sherehe ya kufungwa kwa Mlango huo itaanza kwa nyimbo za Masifu ya jioni ikifuatiwa saa 12:00 kufungwa kwa ibada ya Mlango Mtakatifu, ikiambatana na kupigwa kwa kengegele yenye jina Sperduta,ambayo ni ya kale ya Basilika. Ili kuruhusu maandalizi ya ibada, Basilika itafungwa kwa umma saa 9:00 alasiri kwa waamini. Kisha ufikiawaji utaanza saa 10:00 jioni na utaruhusiwa, kulingana na upatikanaji, tu kwa kushiriki katika sherehe zilizopangwa. Hizi pia zitatangazwa kwenye skrini kubwa zitakzowekwa kwenye Uwanja wa Kanisa hilo Kuu la Mtakatifu Maria Mkuu kwa ajili ya wale ambao watakuwa nje.
Ibada katika Mtakatifu Yohane Lateran na Mtakatifu Paulo Nje ya Kuta
Wakati huo huo Ibada ya kufunga Mlango Mtakatifu wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Yohane Lateran itafuatiwa na Ibada ya Misa Takatifu ikiongozwa na kwaya ya Jimbo la Roma, na mwalimu wake Monsinyori Marco Frisina. Wakati wa Mwaka Mtakatifu, Mlango Mtakatifu wa Yohane Laterano ulivukwa na waamini wa parokia nyingi za Roma: jumuiya za parokia, ama moja moja au zilizopangwa katika wilaya, kwa kiasi kikubwa zilichagua kusherehekea Jubilei yao katika Kanisa kuu la Roma. Wamini pia wataweza kuingia kwenye basilika kwa tiketi ya bure kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 4:00 asubuhi, masaa ya Ulaya. Mara tu Mlango Mtakatifu wa Basilika ya Papa ya Mtakatifu Paulo Nje ya Kuta utakapofungwa, wataweza kushiriki kwa uhuru bila tiketi.