Tume ya Petrocchi:Hakuna ushemasi wa kike,hata kama hukumu siyo ya mwisho
Vatican News
“Lo status quaestionis “yaani "Hoja ya hadhi inayozungukia utafiti wa kihistoria na uchunguzi wa kitaalimungu, ikizingatiwa katika matokeo yake ya pande zote mbili, haijumuishi uwezekano wa kuwakubali wanawake kwenye ushemasi, unaoeleweka kama ngazi ya sakramenti ya Daraja Takatifu. Kwa kuzingatia nuru ya Maandiko Matakatifu, Mapokeo, na Majisterio ya kikanisa, tathmini hii ni imara, ingawa kwa sasa hairuhusu hukumu ya mwisho, kama ilivyo katika muktadha wa kuwekwa wakfu kwa ukuhani." Hili ndilo hitimisho lililofikiwa na Tume ya pili iliyoongozwa na Kardinali Giuseppe Petrocchi, Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu la Aquila, nchini Italia ambayo, kwa agizo la Papa Francisko, ilichunguza uwezekano wa kuendelea na kuwekwa wakfu kwa mashemasi wanawake na kuhitimisha kazi yake kunako mwezi Februari iliyopita.
Hii imeelezwa katika ripoti ya kurasa saba ambayo Kardinali aliituma kwa Baba Mtakatifu Leo XIV mnamo tarehe 18 Septemba 2025 ambayo sasa imetangazwa rasimu kwa ruhusa ya Papa mwenyewe. Tume hiyo, katika kikao chake cha kwanza cha kazi (2021), ilihitimisha kwamba "Kanisa limetambua wadhifa wa shemasi/shemasi kwa wanawake kwa nyakati tofauti, katika sehemu mbalimbali, na katika aina mbalimbali, lakini limehusisha na maana isiyo ya umoja." Mwaka 2021, mjadala wa kitaalimungu ulihitimisha kwa kauli moja kwamba "utafiti wa kimfumo wa shemasi, ndani ya mfumo wa taalimungu ya sakramenti ya Daraja Takatifu, unaibua maswali kuhusu utangamano wa kuwekwa wakfu kwa wanawake kwa ushemasi na mafundisho ya Kikatoliki ya huduma iliyowekwa wakfu.".
Tume pia kwa kauli moja ilielezea uungaji mkono wake kwa ajili ya kuanzishwa kwa huduma mpya ambazo "zingeweza kuchangia katika ushirikiano kati ya wanaume na wanawake." Katika kikao chake cha pili cha kazi (Julai 2022), tume iliidhinisha (kwa kura saba kuunga mkono na moja kupinga) maneno yaliyoripotiwa kikamilifu mwanzoni mwa makala haya, ambayo hayajumuishi uwezekano wa kuwakubali wanawake kwenye ushemasi kama daraja la sakramenti ya Daraja Takatifu, lakini bila kutoa "uamuzi dhahiri" leo.
Hatimaye, katika kikao chake cha mwisho cha kazi (Februari 2025), baada ya Sinodi kumruhusu mtu yeyote aliyetaka kuwasilisha mchango, tume ilichunguza nyenzo zote zilizopokelewa. "Ingawa michango mingi ilipokelewa, ni watu binafsi au vikundi ishirini na viwili pekee vilivyowasilisha karatasi zao, zikiwakilisha nchi chache tu.Kwa hivyo, ingawa nyenzo hizo ni nyingi na katika baadhi ya matukio zinajadiliwa kwa ustadi, haziwezi kuchukuliwa kuwa sauti ya Sinodi, sembuse ya Watu wa Mungu kwa ujumla. Ripoti hiyo inafupisha faida na hasara. Wale wanaounga mkono wanasema kwamba utamaduni wa Kikatoliki na Kiorthodox wa kuweka upadrisho wa kishemasi (lakini pia upadrisho wa kikuhani na kiaskofu) kwa wanaume unaonekana tu kupingana na "hadhi sawa ya mwanamume na mwanamke kama mfano wa Mungu," "hadhi sawa ya jinsia zote mbili, kulingana na ukweli huu wa kibiblia"; tamko la imani kwamba "hakuna tena Myahudi na Mgiriki, mtumwa na huru, mwanamume na mwanamke, kwa maana nyote ni 'mmoja' katika Kristo Yesu" (Wagalatia 3:28); maendeleo ya kijamii "ambayo hutoa ufikiaji sawa kwa jinsia zote mbili kwa kazi zote za kitaasisi na kiutendaji."
Kwa upande mwingine, nadharia hii imeendelezwa: "Uanaume wa Kristo, na kwa hivyo uanaume wa wale wanaopokea maagizo, si bahati mbaya, bali ni sehemu muhimu ya utambulisho wa kisakramenti, kuhifadhi utaratibu wa kimungu wa wokovu katika Kristo. Kubadilisha ukweli huu hakutakuwa marekebisho rahisi ya huduma bali ni kuvuruga maana ya harusi ya wokovu." Aya hii ilipigwa kura na kupokea kura 5 za kuiunga mkono ili kuithibitisha kwa maneno haya, huku wajumbe wengine 5 wakipiga kura ya kuifuta. Kwa kura tisa zilizounga mkono na moja dhidi yake, matumaini yalitolewa kwamba "upatikanaji wa wanawake katika huduma zilizoanzishwa kwa ajili ya huduma ya jamii utapanuliwa (...) hivyo pia kuhakikisha utambuzi wa kutosha wa kikanisa kwa diakonia ya waliobatizwa, hasa wanawake.
Utambuzi huu utathibitika kuwa ishara ya kinabii, hasa pale ambapo wanawake bado wanakabiliwa na ubaguzi wa kijinsia." Katika hitimisho lake, Kardinali Petrocchi anasisitiza kuwepo kwa "dialektiki kali" kati ya mwelekeo mbili wa kitaalimungua. Ya kwanza inathibitisha kwamba kuwekwa wakfu kwa shemasi ni kwa ajili ya huduma na si kwa ajili ya ukuhani: "jambo hili lingefungua njia kuelekea kuwekwa wakfu kwa mashemasi wa kike." Ya pili, hata hivyo, inasisitiza "juu ya umoja wa sakramenti ya Daraja Takatifu na inakataa dhana ya ushemasi wa kike.
Pia anabainisha kwamba ikiwa kukubaliwa kwa wanawake katika daraja la kwanza la Daraja Takatifu kungeidhinishwa, kutengwa kwao kutoka kwa wengine hakungeeleweka." Kwa hivyo, kulingana na kardinali, "uchunguzi mkali na mpana wa kina wa ushemasi wenyewe ni muhimu ili kuendelea na utafiti, " yaani, kuhusu utambulisho wake wa kisakramenti na utume wake wa kikanisa, ukifafanua baadhi ya vipengele vya kimuundo na kichungaji ambavyo kwa sasa havijafafanuliwa kikamilifu". Kwa kweli kuna mabara yote ambapo huduma ya kidiakonia "karibu haipo" na mengine ambapo inafanya kazi na shughuli ambazo mara nyingi "huendana na majukumu yanayofaa kwa huduma za walei au watumishi wa madhabahu katika liturujia".