Papa asiyetarajiwa na wa kinabii,maonyesho huko Venezia kuhusu Papa Yohane Paulo I
Alvise Sperandio - Venezia
Ukumbusho uliowekwa alama za picha, maneno, na vitu vya kibinafsi, vinavyoashiria uhusiano wa karibu kati ya mawazo na vitendo, pia ulionekana wazi katika muda aliotumia katika ziwa kabla ya kuwa Papa. Katika Shule kubwa ya Mtakatifu Teodoro huko Venezia , hata nyingine ya Maonyesho yenye jina: Papa asiyetarajiwa-Mwenyeheri Luciani: Mtazamo wa Kinabii kwa Mtu wa Leo hii, "yalizinduliwa Jumamosi, tarehe 21 Februari 2026. Mpango huu wa kusafiri, uliandaliwa na Rivela Aps, Kampuni yenye makao yake makuu La Scala, Italia, kwa ushirikiano miongoni mwa mengine, na Jumba la Makumbusho la Mahali pa Kuzaliwa la Papa Albino Luciani, na kwa ufadhili wa Jimbo na manispaa zinazohusika katika mkoa wa Veneto.
Baada ya kuanza kwake katika jiji la Belluno na kusimama Oderzo, Vittorio Veneto (ambapo alikuwa Askofu) na Treviso, maonyesho hayo sasa yanaweza kutembelewa Venezia ambapo, mnamo 1978, Patriaki, Kardinali Luciani aliondoka kwenda kwenye Uchaguzi Mkuu wa Upapa, uliomchagua kuwa Papa, akichukua jina la Yohane Paulo I, Papa wa kwanza mwenye majina mawili, ambaye alitoa heshima kwa warithi wake wawili wa Mtum Petro waliomtangulia. Safari kupitia hatua za msingi za utoto, elimu, na ukuaji wa kibinadamu na kiroho wa mtu ambaye pia ana mengi ya kusema katika suala hilo.
![]()
Maonyesho ya Venezia “Papa asiyetarajiwa–Mwenyeheri Luciani:Mtazamo wa kinabii juu ya mwanadamu wa leo"
Mtoto wa Albino na Mundu wa Kukata Nyasi
Maonesha ulizaliwa kutokana na wazo la Nicola Panciera, mkufunzi na msimamizi wa maonyesho ya kielimu, na Milena d'Agostino, ambaye alisimamia uorodheshaji wa vitabu vya Luciani katika Kumbukumbu za Kihistoria za Upatriaki wa Venezia(pamoja na Simone Martuscelli, Rita Piutti, na Giovanni Bresadola), mpango huo una jina la kipekee: "Papa Asiyetarajiwa," si kwa sababu hakujulikana sana, bali kwa sababu alikuwa tofauti kabisa na kile ambacho kingeweza kutarajiwa, kuanzia na mtindo wake rahisi na wa kibinadamu. Akitarajia kwa kiasi fulani maadhimisho ya miaka 50 ya kifo cha Baba Mtakatifu, ambacho kitakumbukwa baada ya miaka miwili ijayo, maonyesho kw njia ya habari yana paneli 40 za picha na historia tatu za video, ikiwa ni pamoja na picha na vitu vya kibinafsi vya Papa Luciani: kuanzia mavazi ya Papa hadi vitabu kadhaa kutoka Jumba la Makumbusho la Mahali pa Kuzaliwa kwake.
Maonyesho hayo yamegawanywa katika sehemu nne za mada: "Uchaguzi kama Papa"; "Maeneo ya Luciani"; "Matukio ya Kikristo"; "Upapa." Miongoni mwa vitu vya kushangaza zaidi ni mundu ambao Albino akiwa mdogo sana, kama vijana wengine wa umri wake, aliondoka nyumbani saa nane usiku wa manane wakati wa kiangazi ili kukata nyasi milimani kwa ajili ya malisho na kuhakikisha ng'ombe wa jamii hiyo wakilishwa vizuri. Ilikuwa kazi ya kuchosha, ambayo Luciani kwa namna fulani alijaza vitabu kadhaa kwenye chungu chake, ambavyo kisha angesoma kati ya mapumziko kutoka kazini, akisubiri nyasi zilizokatwa zikauke kidogo na kuwa nyasi kavu na rahisi kubeba.
![]()
Maonyesho ya Mwenyeheri Luciani katika Shule Kubwa ya Mtakatifu Teodori huko Venezia
Imeandikwa "katika vumbi"
Patriaki wa Venezia, Patriaki Francesco Moraglia, alikuwepo katika uzinduzi huo alisema kuwa: "Luciani, Patriaki aliyekuwa ameteuliwa wa Venezia, katika mahubiri yake mnamo tarehe 8 Februari 1970, alitumia picha yenye nguvu sana aliposema kwamba Mungu anapenda kuandika mambo makubwa si kwenye shaba au marumaru, bali kwenye vumbi." Shaba na marumaru huibua wazo la kazi za kudumu, makaburi, na nguvu inayoonekana; kwa upande mwingine, vumbi huibua udhaifu na hatari. Kwa picha hii, Luciani anapendekeza kwamba Mungu hufanikisha mambo muhimu zaidi kupitia vyombo vya unyenyekevu na dhaifu, si kupitia ukuu wa nje.
Kifungu hiki kimetafsiriwa kama cha kinabii kwa sababu upapa wake ulidumu kwa siku thelathini na tatu tu, mfupi sana kuacha alama za kudumu za kitaasisi, lakini wa kutosha kuchapisha mtindo mpya: lugha rahisi, 'sisi' badala ya 'Mimi,' kukataliwa kwa kiti cha kubebwa, ukaribu wa kichungaji ambao ungewashawishi wale waliofuata baada yake. Ni kana kwamba Mungu alikuwa ameandika kweli kitu muhimu 'vumbini,' lakini kilichokusudiwa kudumu kwa muda mrefu kuliko marumaru."
![]()
Patriaki Moraglia akizindua maonyesho
Matumaini, fadhila pendwa ya Luciani
Loris Serafini, mkurugenzi wa Jumba la Makumbusho na Mfuko wa Canale d'Agordo na Mfuko wa Yohane Paulo I, alikumbusha uhusiano mkubwa wa Luciani na Venezia na kwamba mpnago huo ulibuniwa wakati wa Jubilei ya Matumaini: "Programu yake ya kiaskofu, katika Vittorio Veneto, Venezia, na Roma, ilijumuisha, pamoja na unyenyekevu, fadhila tatu za kitaalimungu: imani, matumaini, na upendo. Ningependa kusisitiza ya pili, muhimu sana leo. Fadhila hii ilikuwa mojawapo ya 'nyota' zilizochaguliwa na Mwenyeheri Luciani wakati, kwa mfano, alisisitiza: 'Tumaini ni tabasamu la maisha ya Kikristo'; maneno ambayo yana nguvu zaidi katika ulimwengu wetu huu, uliyojaa vitisho, vifo, na vita." Aidha alisema "Mafundisho ya Yohane Paulo I, yaliyofahamika kupitia mpango huu katika miji mbalimbali ya Veneto na katika muktadha wa kisasa, magumu lakini pia yaliyojaa matumaini, yawe faraja kwa wote wanaoona maonyesho hayo."
![]()
Baadhi ya picha zilizowekwa kwenye maonyesho
Mtu rahisi lakini wa kushangaza, msomi mkubwa, na mpenda Kanisa
Giovanni Bresadola na Ermanno Benetti, wa Rivela Aps, walielezea jinsi safari ilianza: "Maisha ya Albino Luciani yanatuambia nini leo? Tulianza na maswali haya, tukijikita katika maisha yake ya kila siku, hata kabla ya upapa wake. Nasi tulipata mtu rahisi, lakini, na hii inashangaza kweli, mtu wa taalimungu, msomi mkubwa, mtu wa utamaduni, lakini zaidi ya yote, mtu mdadisi, anayevutiwa na kila kitu. Alitafuta kuwasiliana na kila mtu, kwa kila njia, kwamba maana ya ukweli ni Yesu. Mtu aliyependa Kanisa sana na ambaye tuna uhakika anaweza kuchangia kwa manufaa ya wote, hasa vizazi vichanga. Mfano wake utawatia moyo vijana wengi ambao, katika nyakati hizi ngumu, wanaweza kupata ndani yake mwanga unaoongoza njiani."
Maonyesho hayo yanaweza kutembelea kuanzia tarehe 1 Machi kwa siku zote kuanzia asubuhi saa 4.30 hadi saa 6.30 na Alasiri kuanzia saa 9.30 hasi saa 12 Jioni masaa ya Ulaya pia pamoja na uwezekano wa ziara zinazoongozwa na baada ya kujiandikishwa kwa nafasi za vikundi vilivyopangwa.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here