Maoni ya Kardinali Ouellet kuhusu:Nafasi za Walei katika ngazi za Mamlaka ya Curia Romana
Angella Rwezaula, - Vatican.
Miongoni mwa maamuzi ya ujasiri ya Papa Francisko ni uteuzi wa watu wa kawaida na wanawake Watawa katika nafasi za mamlaka ambazo kwa kawaida huhifadhiwa kwa wahudumu waliowekwa wakfu, Maaskofu, au Makardinali, katika Mabaraza ya Kipapa ya Curia Romana. Papa alihalalisha uvumbuzi huu kwa kanuni ya Kisinodi, ambayo inahitaji ushiriki mkubwa wa waamini katika ushirika na utume wa Kanisa. Hata hivyo, mpango huu unapingana na desturi ya zamani ya kuwakabidhi wahudumu waliowekwa wakfu nafasi za mamlaka. Desturi hii hata hivyo kwa hakika inaweza kutegemea Mtaguso wa Pili wa Vatican, ambao ulifafanua kisakramenti kuhusu Uaskofu (LG 21).
Kwa hivyo kuanzia hapoo ndiyo wasiwasi unaozunguka uamuzi wa kipapa unaoheshimiwa lakini labda unaochukuliwa kuwa wa muda tu. Hadi kufikia hatua ya baadhi ya watu wanatumaini, kwamba mwanzoni mwa upapa mpya, uhusiano wa karibu kati ya huduma iliyowekwa wakfu na kazi ya utawala katika Kanisa utathibitishwa tena. Hii ni wazi si kuhoji maendeleo ya kimafundisho ya Mtaguso, ambao ulitambua kwamba uaskofu ulikuwa kiwango sahihi cha Sakramenti ya Daraja Takatifu, ambapo kazi za kufundisha, kutakasa, na kutawala (tria munera) zilihusishwa. Lakini hii haimaanishi kwamba sakramenti ya Daraja Takatifu ndiyo chanzo pekee cha utawala wote katika Kanisa.
Nitarudia hapa kwa ufupi tafakari juu ya uamuzi huu wa Papa ulionisukuma kufanya wakati wa kuchapishwa kwa Katiba ya Praedicate Evangelium kuhusu mageuzi ya Curia Romana. Uthibitisho wa kisheria uliowasilishwa wakati wa uwasilishaji wa Katiba hii haukupata makubaliano ya jumla kwa sababu ulionekana kutatua kwa hiari au kwa njia isiyo ya kiholela mzozo wa karne nyingi, ukichukua msimamo wa kitaaluma ambao Papa angeuchukua kwa hasara ya mazungumzo ya awali kati ya wataalimungu na wanasheria wa Kanisa. Nilipendekeza tafsiri ya Kitaalimungu ya uamuzi huu na Baba Mtakatifu ambayo inapita zaidi ya mfumo wa misimamo tata ya kisheria kuhusu asili na tofauti kati ya nguvu ya Daraja na nguvu ya mamlaka katika Kanisa. Hili limeainishwa katika makala niliyochapisha mnamo tarehe 21 Julai 2022, katika Gazeti la Osservatore Romano, na nilichunguza kwa njia hiyo hiyo katika kitabu changu cha: “Parola, Sacramento, Carisma, yaani "Neno, Sakramenti, Karama: Kanisa la Kisinodi, Hatari, Fursa (Siena, Cantagalli, 2024).
Kufuatia na tafakari hii, nimetumia nguvu nyingi kutafakari uhusiano kati ya Roho Mtakatifu na Kanisa, na hasa zaidi kati ya Roho Mtakatifu, sakramenti saba, na sakramenti ya Kanisa kwa ujumla. Wataalamu wanatambua kwamba taalimungu yetu ya sakramenti inakabiliwa na upungufu wa (pneumatolojia)upumuaji unaoenda sambamba na maono ya Kikristo ya upande mmoja. Ikiwa ni kweli kwamba sakramenti saba ni matendo ya Kristo, pia ni matendo ya Kanisa yanayotokana na matendo ya Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu huambatana kila mara na matendo ya sakramenti ya Kristo aliyefufuka, ili kujenga Kanisa la Kisakramenti, ambalo Mtaguso wa II wa Vatican wa Kiekumeni ulizungumzia kutoka aya ya kwanza ya Katiba ya Kidogma ya Lumen Gentium. Zaidi ya hayo, kitendo cha Roho Mtakatifu kinapita zaidi ya sakramenti na hujidhihirisha kwa uhuru katika karama na huduma ambazo Mtaguso kwa bahati nzuri ulitathmini upya baada ya karne nyingi za kutoaminiana na maendeleo duni.
Kwa hivyo, mwelekeo huu wa Mtaguso unamaanisha umakini mpya kwa uwepo na utendaji wa Roho Mtakatifu katika huduma ya ushirika na utume wa Kanisa. Hata hivyo, tunatambua kwamba hatujazoea kutambua uwepo na utendaji wake, kwani tumejifunza kuzungumza kuhusu neema kwa maneno ya kibinadamu, bila kumtaja Mtu wa kimungu anayeunda matokeo ya Fumbo la Pasaka katika roho na miundo ya Kanisa. Nafsi hii ya kimungu ni Roho Mtakatifu anayetoka kwa Baba kupitia upatanisho wa Kristo aliyefufuka, Ushirika wa Kipaji ambao Kanisa ni tunda na sakramenti yake. Bado tunafanya kazi kuelewa sakramenti ya Kanisa kwa ujumla, kama ushirika wa kimungu-mwanadamu unaofanya uwepo wa fumbo la ushirika wa Utatu. Ushirika huu unaonekana kuwa mgumu kufafanua na kubainisha katika maudhui yake. Hata hivyo sakramenti saba zipo kwa usahihi kuelezea ushirika huu wa kikanisa ili uwe na maana na mvuto, hivyo kufanya Kanisa kuwa la kimisionari na muhimu zaidi katika jamii.
Je, marejeo haya kwa Roho Mtakatifu, mbunifu wa ushirika wa Kanisa, yanahusiana na huduma ya utawala katika Kanisa? Je, haitoshi kuwa na ahadi za Yesu kwa mitume wake katika Injili, ambazo zinahakikisha mamlaka yao na kuwapa uhakika wa uwepo wake wa kudumu? Je, Roho Mtakatifu analeta maana au ufanisi gani wa ziada katika sakramenti ya Kanisa? Je, jukumu lake halijapunguzwa hadi lile la msaidizi wa Kristo aliyefufuka, ambaye anabaki kuwa mhusika mkuu wa utaratibu mzima wa sakramenti? Lakini, je, tunawezaje kuongeza uhusiano kati ya Ekaristi na Kanisa, ambalo ni ufunguo wa ushirika wa Kanisa na injini ya upanuzi wake wa kimisionari?
Maswali haya yanaonesha kwamba kuna uwanja wa utafiti ambao haujachunguzwa ambao unahitaji kuchunguzwa ili kutoa mwanga zaidi juu ya ishara ya unabii ya Papa Francisko. Hili la mwisho linatambua mamlaka ya Roho Mtakatifu anayefanya kazi zaidi ya kiungo kilichowekwa kati ya huduma iliyowekwa wakfu na utawala wa Kanisa. Hili si kuhusu kubadilisha utawala wa kikarama wa utawala wa kihierarkia. Hata hivyo, kulingana na mwongozo ambao tayari umeainishwa katika sheria ya Kanisa (Kanoni 129, §2), wahudumu waliowekwa wakfu lazima waweze kutegemea watu waliopewa karama, ambao wanatambuliwa hivyo na wameunganishwa kikamilifu katika vyombo vya utawala, kisheria, na kichungaji vya Curia Romana. Hii haimaanishi kuwakabidhi kazi za sakramenti kwa maana ya Kristo, bali kuunganisha karama zao katika huduma ya Roho Mtakatifu, ambaye anasimamia ushirika wa Kanisa katika maonesho yake yote. Kwamba mabaraza yaliyojitolea kwa ajili ya mawasiliano, utawala Mkuu wa Jiji la Vatican, kuhamasisha maendeleo Fungamani ya Binadamu, kwa maisha, familia na walei, kuhamasisha karama za kitawa au vyama vya maisha ya kitume, viongozwe na watu wenye uwezo, walei au watawa, wenye karama zinazotambuliwa na Mamlaka Kuu, haipunguzi thamani ya huduma yao kutokana na ukosefu wa mamlaka ya kutekeleza sheria
Karama za Roho Mtakatifu hutumia uzito wake wa mamlaka katika maeneo ambapo Sakramenti ya daraja, si lazima, ambapo inaweza hata kuwa sahihi kwa utaalamu kuwa wa mpangilio tofauti; kwa mfano, katika usimamizi wa rasilimali watu, usimamizi wa haki, utambuzi wa kiutamaduni na kisiasa, usimamizi wa fedha, na mazungumzo ya kiekumeni. Katika maeneo haya yote, yaliyotajwa kwa mfano, mtu anaweza kufikiria ushirikiano kati ya Mapadre, walei, na watawa ambapo nafasi ya chini ya mhudumu aliyewekwa wakfu haitakuwa haifai au yenye shaka. Uzoefu wa kihistoria wa Kanisa unaonesha kwamba utamaduni wa mashirika makubwa ya kitawa na aina mbalimbali za maisha ya wakfu au ya kitume hudhania utawala wa ndani wa karama, mara tu utakapotambuliwa rasmi na kuidhinishwa na mamlaka ya kihierarkia.
Msimamizi wa Kikanisa cha Watawa, kwa mfano, hawezi kujipatia haki ya kulazimisha maoni yake kwa wale wanaohusika na Jumuiya anayoitumikia. Huduma ya kichungaji haiwezi kuchukua nafasi ya mamlaka ya karama. Papa anapomteua mwanamke kuwa mkuu wa Baraza la Kipapa, hakabidhi mamlaka yake kwa mtu yeyote tu; anamkabidhi mtu anayetambulika mwenye uwezo wa kiwango fulani cha uzoefu wa kikanisa, kwa sababu ya karama, jukumu bora zaidi ambalo linabaki limeundwa na kuhakikishwa na mamlaka ya jumla ya Baba Mtakatifu ya Curia Romana. Mtazamo wa kisheria hauonekani kupendelea kumfikiria Roho Mtakatifu kwa kitu kingine chochote isipokuwa mdhamini mkuu wa taasisi; inaonekana kukosa njia za kutambua ishara za Roho, misukumo yake binafsi na ya kijumuiya,karama maalum ambayo inawapatia washiriki wa Mwili wa Kristo, kukosa pumzi ( pneumatolojia,) ambayo imebadilishwa na mtazamo chanya wa kihistoria, au kwa ujumla sambamba na sheria za kiraia, kama ilivyo katika Kanuni ya 1983, ambayo inapuuza neno karama na kuizungumzia tu kwa upande wa urithi.
Ni muhimu kuanza tena mazungumzo kati ya wanasheria wa Kanisa na Wataalimungu ili “sheria ya neema iweze kukua kwa amani, nahadi kusababisha uhuru wa kuwajumuisha watu wenye karama, walei au wa watawa, katika nafasi za mamlaka za Curia Romana na tawala za kijimbo. Hii tayari iko hivyo katika sehemu nyingi, na si tu kwa sababu ya uhaba wa mapadre. Ruhusa ya muda inapaswa kuzingatiwa upya au maendeleo ya kikanisa? Sina shaka kwamba ishara ya Papa Francisko ina ahadi kwa siku zijazo, kwani inazindua utambuzi wa mamlaka ya karama kwa mamlaka ya kihierarkia, kulingana na miongozo ya Mtaguso, ambayo inawaalika wachungaji "kutambua ndani yao huduma na karama (za walei), ili wote waweze kushirikiana kulingana na uwezo wao na kwa moyo mmoja katika kazi ya pamoja" (LG 30:33).
Hii itachangia hasa katika kurejesha taswira ya mamlaka ya kichungaji, iliyodharauliwa na pigo la: ukuhani, roho ya tabaka, uhifadhi wa marupurupu, hamu ya kupanda ngazi ya uongozi, kwa kifupi, kutoka katika mawazo yaliyofungwa ambayo yanafikiria utumishi wa serikali kwa maana ya nguvu na ambaya haiwezi kuthamini karama kulingana na kiwango cha mamlaka yao. Kwa sababu, kama Mtaguso unavyosema, ni muhimu kwetu sote "kwa njia ya kutenda upendo wa kweli, tunapaswa kukua katika kila njia katika yeye aliye kichwa, yaani Kristo; kutoka kwake mwili wote, ukiunganishwa na kuunganishwa pamoja kwa kila kiungo, kila kiungo kikifanya kazi vizuri, hukua na kujijenga katika upendo" (Efe 4:15-16)" (LG 30).
Kardinali, Mwenyekiti Mstaafu wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Maaskofu.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here