Kard.Parolin kwa Balozi wa Israeli:Masikitiko kwa tukio la Kaburi Takatifu
Vatican News
Katibu Mkuu wa Vatican Kardinali Pietro Parolin, akifuatana na Askofu Mkuu Paul R. Gallagher, Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa, walikutana Jumatatu tarehe 30 Machi 2026, na Yaron Sideman, Balozi wa Israeli anayewakilisha nchi yake Vatican.
Kwa mujibu wa Ofisi ya Vyombo vya Habari ya Vatican ilitangaza hilo kupitia chaneli yake ya Telegram, ikielezea kwamba mkutano huo unafuatia na "kitendo kisichofurahisha" kilichotokea tarehe 29 Machi, katika Dominika ya Matawi, kilichomhusisha Kardinali Pierbattista Pizzaballa, OFM, Patriaki wa Kilatini wa Yerusalemu, na Padre Francesco Ielpo, OFM, Msimamizi wa Nchi Takatifu, "ambao walikataliwa kuingia katika Basilika ya Kaburi Takatifu huko Yerusalemu na Polisi wa Israeli."
"Wakati wa mazungumzo," inasomeka taarifa hiyo "masikitiko yalioneshwa kwa tukio hilo, ambalo ufafanuzi ulitolewa, na makubaliano yaliyofikiwa kati ya Patriaki wa Kilatini ya Yerusalemu na mamlaka mahalia kuhusu ushiriki katika liturujia za (Triduum)-'Siku Tatu Takatifu', katika Basilika ya Kaburi Takatifu huko Yerusalemu yalitambuliwa."
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku bonyeza hapa: Just click here.