Tafuta

Watoto wakati wa siku yao mwaka 2024 jiji  Vatican. Watoto wakati wa siku yao mwaka 2024 jiji Vatican.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Siku ya Watoto Duniani jijini Roma imefutwa!

Kufutwa kwa tukio lililopangwa kufanyika mwishoni mwa Septemba kulipitishwa na Baraza la Kipapa la Walei,Familia na Maisha kufuatia Maandishi ya Mkono wake Papa ya Mwezi Februari 2026.Ujumbe unaeleza kwamba:"mipango yote inayolenga utunzaji wa kichungaji wa watoto inaweza kufanywa,kwa hiari ya Maaskofu,katika ngazi ya Jimbo au Parokia."

Vatican News

Kuafuatia na maandishi ya mkono wake (chirografo) Papa  Leo XIV, ya tarehe 12 Februari 2026 kuhusu Siku ya Watoto Duniani, Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha, "baada ya kutafakari kwa makini na kwa makubaliano na Baba Mtakatifu, limeona inafaa kufuta maadhimisho ya Siku ya II ya Watoto Duniani, ambayo awali ilipangwa kufanyika jijini Roma kuanzia tarehe 25 hadi 27 Septemba 2026."

Hii imeelezwa katika taarifa kutoka Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha, ambalo linasisitiza kwamba: "mipango yote inayolenga utunzaji wa kichungaji wa watoto inaweza kutekelezwa, kwa hiari ya Maaskofu, katika ngazi ya jimbo au parokia na kwa ushiriki wa familia, mahali pa ukuaji wa kibinadamu na kiroho wa kila mtoto."

Taarifa hiyo inahitimisha kwa kuthibitisha tena kujitolea kuhamaisha "utunzaji wa kichungaji wa familia katika vipengele vyake vyote."

SIKU YA WATOTO DUNIANI KUAHIRISHWA

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku:Just click here.

31 Machi 2026, 17:20