Chuo cha Kipapa cha Sayansi Jamii:Mkutano kuhusu Matumizi ya Madaraka katika ngazi ya Dunia!
Vatican News
Wakati Baba Mtakatifu Papa Leo XIV anarudia "kukataa" vita alipokuwa akisafiri kwa ndege kwenda Algeria katika ziara yake ya Kitume barani Afrika, huku akiwahimiza viongozi wa dunia kutafuta njia za amani, Mkutano Mkuu uliandaliwa mjini Vatican ili kutafakari masuala yanayozunguka mageuzi ya mahusiano ya kijiografia na kisiasa. Baada ya vikao viwili vya jumla mwaka 1998 na 2000, vilivyojitolea kwa ajili ya uchambuzi wa demokrasia katika aina zake mbalimbali za kisasa, kuanzia tarehe 14 Aprili 2026 Chuo cha Kipapa cha Sayansi ya Jamii kimanza kushughulika mada ya: Matumizi ya Nguvu: Uhalali, Demokrasia, na Ufafanuzi Mpya wa Utaratibu wa Kimataifa. Kama ilivykuwa kabla ya mwaka 2000, demokrasia ilionekana kuwa upeo usioepukika kwa nchi zote zilizostaarabika, miongo mitatu baadaye, hali si sawa tena.
Njia ya amani inahitaji mioyo na akili zilizofunzwa
Kama Papa Leo XIV alivyokumbuka mnamo tarehe 30 Mei 2025 kuwa, "Njia ya amani inahitaji mioyo na akili zilizofunzwa kuwajali wengine na zenye uwezo wa kuona mema ya wote katika ulimwengu wa leo. Njia ya amani, kiukweli, inahusisha kila mtu na inaongoza katika kukuza mahusiano ya haki miongoni mwa viumbe vyote hai.” Kama Mtakatifu Yohane Paulo II alivyosisitiza, kuwa amani ni mema yasiyogawanyika; ama ni ya kila mtu au si ya mtu yeyote (Rej Sollicitudo rei socialis, 26). Inaweza kupatikana na kuhisiwa kweli kama ukweli wa maisha na maendeleo kamilifu tu ikiwa kuna dhamiri za watu "azimio thabiti na la kudumu la kujitolea kwa manufaa ya wote."
Mada kuhusu demokrasia huria na ukosoaji wake; na upangaji upya wa utaratibu wa kimataifa
Mkutano huo unashughulikia masuala yanayohusiana na nguvu na uhalali; demokrasia huria na ukosoaji wake; na upangaji upya wa utaratibu wa kimataifa. Kazi ya Wanazuoni hao itafunguliwa na Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Profesa Helen Alford, na vikao vitaratibiwa na Vittorio Hõsle (Chuo Kikuu cha Notre Dame, Marekani), Rodrigo Guerra-Lopez (Tume ya Kipapa ya Amerika Kusini), Krzysztof Wielecki (Chuo Kikuu cha Warsaw), Fabio Ferrucci (Chuo Kikuu cha Molise), Niraja Gopal Jayal (Chuo cha Mfalme London), na Kardinali Stephen Chow Sau-Yan (Jimbo la Hong Kong).
Tunaposhuhudia ujio wa mpangilio mpya wa dunia, ina mantiki kutafakari sababu na sababu zilizosababisha kuanguka kwa ule wa zamani. Ni udhaifu na dosari gani za mpangilio huo wa dunia zilizoacha mlango wazi kwa athari kubwa na za kina kama zile tunazoshuhudia leo? Na, zaidi ya yote, tunachoweza kufanya katika hali ya sasa ili kuhakikisha haki na amani..
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku:Just click here.