Tafuta

Baba Mtakatifu Leo XIV, Ijumaa tarehe 10 Aprili 2026 amekutana na kuzungumza na Bwana Emmanuel Macron, Rais wa Ufaransa Baba Mtakatifu Leo XIV, Ijumaa tarehe 10 Aprili 2026 amekutana na kuzungumza na Bwana Emmanuel Macron, Rais wa Ufaransa  

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa Akutana na Papa Leo XIV Mjini Vatican

Katika mazungumzo yao, viongozi hawa wawili yaani Baba Mtakatifu na Rais wa Ufaransa wamegusia uhusiano mzuri wa kidiplomasia uliopo kati ya nchi hizi mbili na baadaye wakajielekeza katika masuala ya Kimataifa kwa kuzama zaidi katika vita inayoendelea sehemu mbalimbali za dunia na hivyo kuonesha matumaini yao kwamba, kwa njia ya majadiliano katika ukweli na uwazi, amani itaweza kurejea tena na hivyo kuwawezesha watu kuishi kwa utulivu.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV, Ijumaa tarehe 10 Aprili 2026 amekutana na kuzungumza na Bwana Emmanuel Macron, Rais wa Ufaransa ambaye baadaye amekutana na kuzungumza pia na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican aliyekuwa ameambatana na Askofu mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu mkuu wa Mambo ya Nchi za Nje, Ushirikiano na Mashirika ya Kimataifa. Katika mazungumzo yao, viongozi hawa wawili, wamegusia uhusiano mzuri wa kidiplomasia uliopo kati ya nchi hizi mbili na baadaye wakajielekeza katika masuala ya Kimataifa kwa kuzama zaidi katika vita inayoendelea sehemu mbalimbali za dunia na hivyo kuonesha matumaini yao kwamba, kwa njia ya majadiliano katika ukweli na uwazi, amani itaweza kurejea tena na hivyo kuwawezesha watu kuishi kwa utulivu.

Rais Macron wa Ufaransa tarehe 10 Aprili 2026 amekutana na Papa Leo XIV
Rais Macron wa Ufaransa tarehe 10 Aprili 2026 amekutana na Papa Leo XIV   (@Vatican Media)

Itakumbukwa kuwa, hii ni mara ya nne kwa Rais Emmanuel Macron kukutana na viongozi wakuu wa Vatican kwani kwa mara ya kwanza ilikuwa ni mwaka 2018, 2021 na Mwaka 2022 alipokutana na kuzungumza na Hayati Baba Mtakatifu Francisko mjini Vatican. Baba Mtakatifu Leo XIV na Rais Macron ni viongozi wanaotamani kuona mchakato wa ujenzi wa Jumuiya ya Kimataifa unasimikwa katika utawala wa sheria.

Rais wa Ufaransa
11 Aprili 2026, 17:35