Tafuta

Olimpiki Cortina- Milano 2026 Olimpiki Cortina- Milano 2026  (ANSA)

Wanariadha wa Olimpiki na Paralimpiki watakutana na Papa:ushuhuda na mshikamano

Kundi la wanariadha wanaorejea kutoka Michezo ya Milan-Cortina watakutana na Papa Leo XIV mnamo Aprili 9,katika mpango wa Baraza la Kipapa Utamaduni na Elimu,pamoja na Wanariadha wa Vatican,CONI na Kamati ya Olimpiki ya Walemavu ya Italia.Watatembelea Hospitali ya watoto ya Mtakatifu Marta mjini Vatican ili kukutana na baadhi ya familia katika hali dhaifu.

Vatican News

Kuanzia medali kwenye uwanja wa michezo hadi ukaribu na wale ambao hawajawahi kupanda jukwaani kwa sababu hawaonekani. Hii itakuwa uzoefu unaofurahiwa na baadhi ya wanariadha wa Italia walioshiriki katika Olimpiki ya Majira ya Baridi na Michezo ya Paralimpiki huko Milan-Cortina nchini Italia ambao wakutana na Papa Leo XIV.

Kundi hilo, likiwakilisha wenzao wote, litakuwa mjini Vatican siku ya Alhamisi  tarehe 9 Aprili 2026, baada ya Pasaka saa 5:30 asubuhi majira ya Ulaya ili kukutana na Baba Mtakatifu Leo XIV katika Ukumbi wa Clementine wa Jumba la Kitume na baadaye kushiriki wakati wa mshikamano.

Msalaba uliosindikiza wana michezo

Wakati wa Mkutano na  Papa, kama sehemu ya mpango ulioratibiwa na Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu, kwa ushiriki wa Wanariadha wa  Vatican, Kamati ya Olimpiki ya Kitaifa ya Italia (CONI) na Kamati ya Paralimpiki ya Italia (CIP), “Msalaba wa Wanamichezo,” ambao uliwekwa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Babila huko Milano kwa muda wote wa Michezo, pia utakuwepo.

Maswali kwa waandishi wa habari na kutembeleza zahati ya watoto

Mwisho wa Mkutano huo katika  taarifa kutoka ya Baraza la Kipapa, kutakuwa na sehemu ya waandishi wa habari katika ukumbi mkuu ndani ya  Jumba la Kitume, kwa wanariadha wanaotaka kutoa ushuhuda wao. Wengine watatembelea Zahanati ya Watoto ya "Santa Marta" "kukutana na familia zinazopitia umaskini na udhaifu."

Michezo na Ukaribu

Taarifa hiyo inakumbusha kwamba sanjari na ufunguzi wa Michezo ya Majira ya Baridi mnamo tarehe 6 Februari 2026, Papa Leo XIV alisaini Barua yenye mada: "Maisha tele" kuhusu thamani ya michezo, ambayo inasisitiza, miongoni mwa mambo mengine: jinsi michezo ya ushindani si tu kuhusu changamoto za kiwango cha juu bali pia kuhusu ubinadamu, kulingana na maadili yanayohamasisha uzoefu wa Wanariadha Vatican. "Hapa, michezo si tamasha, bali ni ukaribu; si uteuzi, bali ni usaidizi; si ushindani uliokasirika, bali ni safari ya pamoja,” Papa alibainisha.

WABARIADHA KUKUTANA NA PAPA

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku:Just click here.

01 Aprili 2026, 16:51