Tafuta

Fuatilia matukio ya Papa Mbashara kuupitia Wijeti Fuatilia matukio ya Papa Mbashara kuupitia Wijeti 

Ziara ya Kwanza Kimataifa ya Papa'online'katika wijeti ya Vatican News

Kwa mara ya kwanza katika historia kutakuwa na uwezekano wa kufuatilia ziara ya Papa Leo XIV barani Afrika kupitia WIJETI ya Vatican kwa kufuata video zote mbashara katika kila lugha.Kuna uwezekano wa kuweka wijeti kwenye tovuti zote bila malipo ili kupata matangazo mbashara na habari zote kuhusu ziara ya Papa inayoanza Aprili 13-23,2026.

Vatican News

Wijeti  Mpya ya video ya Vatican News ilizinduliwa mnamo Februari iliyopita na imepata kupakuliwa na mamiaelfu ya tovuti katoliki mtandaoni Ulimwenguni kote. Sasa, shukrani  kwa chombo hicho, itawezekana kupata moja kwa moja na kwa urahisi nyenzo zozote za habari zinazohusiana na hija ya Papa Leo XIV barani Afrika kuanzia tarehe 13 hadi 23 Aprili 2026.  Hii inahusiana na habari, video, tafsiri zilizoandaliwa na wahariri wa habari wa Vatican ambao hutoa maudhui ya kuaminika na yaliyothibitishwa.

Papa:Wijeti ya Habari za Vatican ni chombo cha uinjilishaji

Papa Leo XIV mwenyewe aliwaandikia Maaskofu ulimwenguni kote mnamo Februari iliyopita, akihimiza usakinishaji wa wijeti hii: "Ndugu mpendwa, mpango huu wa Habari za Vatican ni chombo cha uinjilishaji. Unatoa fursa ya kuunganisha na kubadilishana zawadi kati ya Roma na Kanisa katika nchi yako. Ni njia kwa ajili ya parokia na jumuiya zako kupata taarifa kila mara kutoka katika  chanzo kikuu."

Fuatilia Wijeti
Fuatilia Wijeti

Matangazo na ripoti katika lugha uliyochagua

Wijeti inaweza kusakinishwa kwa urahisi bila malipo hivi sasa, kama ilivyosisitizwa na Dr  Andrea Tornielli, Mkurugenzi Mkuu wa uhariri wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano. Akielekea Tovuti za Wakatoliki, parokia, jimbo, na aina nyingine za vyombo, Dk. Tornielli anaandika: "Katika mkesha wa ziara ya Papa Leo nchini mwenu, tunafurahi kuwawekea kifaa hiki kipya, ambacho kitaruhusu tovuti zote na huduma za habari zinazohusiana na Kanisa, (majimbo, parokia, na vyombo vingine vya habari ambavyo mngependa kushirikishana navyo ujumbe huu ) kupokea matangazo ya moja kwa moja ya video ya ziara ya Papa Leo XIV na masasisho yote ya Habari za Vatican katika lugha mnayoichagua."

Usakinishaji bila malipo

Unaweza kusakinisha Wijeti kwenye tovuti yako kwa kupakua kiungo hiki:

https://www.vaticannews.va/widget/embed.html

Tunakuhimiza kutumia zana hii na hivyo kufikisha maneno ya Papa kwa wapokeaji wengi iwezekanavyo.

Njia ya Hija ya Papa

Ziara ya Pili ya  Papa Leo XIV nje ya nchi itadumu siku kadhaa kuanzia tarehe 13 hadi 23 Aprili 2026. Papa atasafiri kwenda Algeria, Camerun, Angola, na Guinea ya Ikweta, akizungumza kwa lugha nne na kuzungumzia mada kama vile amani, mazingira, uhamiaji, familia, vijana, na ukoloni. Pia itakuwa fursa ya kumfuata Papa wa Kiagostino katika nyayo za Mtakatifu Agostino.

WIJETI YA PAPA AFRIKA

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku:Just click here.

10 Aprili 2026, 11:36