Tafuta

2026.05.28 Papa na Antonio Di Iorio, Mkurugenzi mpya wa Fas 2026.05.28 Papa na Antonio Di Iorio, Mkurugenzi mpya wa Fas 

Antonio Di Iorio ni Mkurugenzi Mpya wa Mfuko wa Afya,Vatican

Afisa wa Kitengo cha Masuala ya Jumla cha Sekretarieti ya Vatican,atachukua wadhifa wake tarehe 15 Julai.

Vatican News

Antonio Di Iorio ndiye mkurugenzi mpya wa FAS, Mfuko wa Usaidizi wa Afya, taasisi ya Vatican inayotoa huduma za afya kwa wafanyakazi wa Kikanisa, Watawa  na walei (wa sasa na wastaafu) wa Curia Romana, Gavana, na vyombo vinavyosimamiwa moja kwa moja na Kiti Kitakatifu cha Kitume. Uteuzi wa Papa Leo XIV ulichapishwa alhamisi tarehe 28 Mei 2026, na ulitangazwa katika Sekretarieti ya Vatican na naibu wake, Askofu Mkuu  Paolo Rudelli. Hadi sasa yeye ni afisa katika Kitengo cha Masuala ya Jumla ya Sekretarieti ya Vatican na  mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko huo huo tangu tarehe 24 Juni 2020, ambapo atachukua wadhifa wake mnamo Julai 15. Di Iorio pia ni mthibitishaji wa saini katika Ofisi ya Camerlengo.

Wakati wa kutangazwa kwake wadhifa mpya
Wakati wa kutangazwa kwake wadhifa mpya

Maisha na Kazi

Akiwa ameoa na mtoto mmoja wa kiume, mkurugenzi mpya wa FAS aliajiriwa na Kitengo cha Kwanza cha  Sekretarieti Vatican mnamo tarehe 2 Januari 1988, na amehudumu hapo tangu wakati huo. Alishiriki katika Mkutano Mkuu wa Uchaguzi  mara mbili kama mthibitishaji wa Chumba cha Kitume, kisha Ofisi ya Camerlengo, kufuatia kujiuzulu kwa Papa Benedikto XVI na baadaye kufuatia kifo cha Papa Francisko. Katika Sekretarieti ya Vatican, alishikilia nyadhifa mbalimbali, ikiwa ni pamoja na: mjumbe kamili wa Bodi ya Wakaguzi wa OPBG kwa kipindi cha miaka mitatu 2014-2016, ambacho sasa ni naibu mkaguzi; na nafasi zingine za ukaguzi wa taasisi za Vatican (LEV, CTV). Aliteuliwa katika Bodi ya Wakurugenzi ya FAS mnamo 2020, bado ni mjumbe. Alipewa Tuzo ya shujaa wa Papa ya Mtakatifu Sylvester mnamo Desemba 1994 na Shujaa wa Mtakatifu Gregori Mkuu mnamo Agosti 2006.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

28 Mei 2026, 18:26