Tafuta

2026.05.12 Askofu Mkuu Gallagher huko Cabo Verde 2026.05.12 Askofu Mkuu Gallagher huko Cabo Verde 

Gallagher:Diplomasia ya Vatican imetumikia amani kwa karne nyingi

Katika maadhimisho ya miaka 50 ya uhusiano wa kidiplomasia ya Vatican na Cape Verde,Askofu Mkuu Gallagher,Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa,alitoa hotuba ambapo alichunguza mbinu za utendaji kazi wa diplomasia ya Kipapa.Vatican ina uhusiano na Mataifa 184 na Balozi 93 zilizoidhinishwa Roma,ambazo zinaimarisha uzoefu unaopatikana baada ya muda kwa kuhamasisha haki na ulinzi na heshima ya binadamu.

Na Sr. Christine Masivo,CPS –Vatican.

Ulinzi wa maisha, familia, uhuru wa kidini, haki za binadamu, demokrasia, ushirikiano wa pande nyingi, na sheria za kimataifa huunda "maadili ya msingi" yanayoshirikiwa na Vatican na Cape Verde. Pamoja na haya kuna "changamoto kuu za kimataifa" kama vile migogoro, mgogoro wa hali ya hewa, ukosefu wa usawa, uhamiaji, mabadiliko ya kiteknolojia, biashara ya dawa za kulevya, mgogoro wa maadili, ubinafsi, na kupoteza hisia ya ukweli.Haya yalisema na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa, katika mkutano uliofanyika Jumatatu, tarehe 11 Mei 2026, huko Cape Verde.  Askofu Mkuu amekuwa huko Jamhuri ya kisiwa cha Afrika hadi tarehe  14, katika fursa ya maadhimisho ya miaka 50 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya Vatican na nchi hiyo.

Lengo kuu la amani

Katika hotuba yake kwa lugha ya Kihispania alisema kuwa “Nusu karne ya mazungumzo, ushirikiano, na urafiki wa kweli kati ya taifa changa huru na moja ya taasisi ya zamani za kidiplomasia duniani alisisitiza kwamba diplomasia ya Papa iliimarishwa na tamaduni ndefu ya kihistoria inayolenga lengo kuu la amani na ulinzi na ukuzaji wa utu wa mwanadamu.

Katika suala hilo  alikumbuka asili ya diplomasia ya Papa katika karne ya 11, wakati wa Mageuzi ya Papa  Gregori, pamoja na kuanzishwa ndani ya Kanisa kwa "haki ya uhalali." Askofu Mkuu Gallagher  alisisitiza utulivu wa kitaasisi uliopatikana katika karne ya 15, huku mpito  baadaye ulipitishwa na Mataifa mengine pia   kutoka utume wa  mara kwa mara hadi wa kudumu, sifa kuu ya diplomasia ya sasa. Mwishowe, alilenga katika uimarishaji wa diplomasia ya Papa katika karne ya 16 na 17, ambapo alisisitiza utofauti kati ya  mabalozi, mawakili, wajumbe.


Mahusiano ya kidiplomasia ya Vatican

Kwa sasa, "Vatican inadumisha uhusiano wa kidiplomasia na Nchi 184, pamoja na Umoja wa Ulaya na Shirika la Kijeshi la Malta," na kuna Balozi  93 za kidiplomasia zilizoidhinishwa na Vatican na ziko Roma.  Askofu Mkuu Gallagher alielezea mbinu za kazi za kidiplomasia za Papa na utendaji kazi wa Sekretarieti ya Vatican katika dhamira yake ya kumtumikia Papa. Ndani ya uzoefu ulioendelezwa kwa karne nyingi "katika huduma ya amani, haki, na ulinzi na uhamasishaji wa wa utu wa binadamu," alibainisha, uhusiano na Jamhuri ya Cape Verde ulianza hata kabla ya nchi hiyo kutangaza uhuru mwaka 1975.

Askofu Mkuu Gallagher aliwakumbusha Mkutano  uliofanyika wa  Papa Paulo VI mnamo tarehe 1 Julai 1970, mjini  Vatican kwa viongozi kadhaa wa harakati za uhuru wa Afrika, wakiwemo Agostinho Neto, Marcelino dos Santos, na Amílcar Cabral. Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Nchi  alisisitiza kwamba mkutano huo "ulisababisha kukatizwa kwa muda kwa uhusiano na Ureno, lakini ulionesha kujitolea kwa ujasiri kwa Kanisa kuunga mkono sababu ya Afrika na utu wa watu."

Kanisa huko Cape Verde

Wakati huo huo, uwepo wa Kanisa umejikita katika historia ya Jamhuri ya Cape Verde na ni sehemu ya utambulisho wake. Wamisionari Wakatoliki, miongoni mwa wakazi wa kwanza wa visiwa vya Afrika mnamo 1462, walitoa matokeo mengi  sana ya utamaduni, sanaa, muziki, na desturi zake. Ilikuwa mwaka 1533 ambapo Jimbo la Santiago ya Cape Verde ilianzishwa, ya kwanza Kusini mwa Jangwa la Sahara, na kuifanya nchi hiyo kuwa "kitovu cha uinjilishaji na mpangilio wa kijamii, pamoja na shule, hospitali, na taasisi za elimu," Askofu Mkuu Gallagher alisisitiza. Badala ya kupendekeza "mifumo ya kisiasa au kiuchumi," Kanisa linaomba "kwamba utu wa binadamu uheshimiwe na kwamba uhakikishwe uhuru wa kutekeleza dhamira yake.” Katika muktadha huu, alirejea Mkataba wa 2013 kati ya Vatican na Cape Verde, uliolenga kuhakikisha usaidizi hasa katika maeneo ya afya na elimu.

Kusasisha Mkataba wa kidiplomasia kati ya Vatican na Cape Verde
Kusasisha Mkataba wa kidiplomasia kati ya Vatican na Cape Verde

Mahusiano yaliyojengwa juu ya upendo na ukweli

Askofu Mkuu Gallagher pia alihimiza kuhamasisha "diplomasia ya matumaini na maadili," akitumia wito wa Papa Leo XIV wa "amani isiyo na silaha na na inayopokonya silaha" kupitia "mahusiano yaliyojengwa juu ya upendo na ukweli." Mwishowe, aliwahimiza viongozi na watu wa Cape Verde "kudumu katika kutafuta manufaa ya pamoja, haki, umoja, na mshikamano." Siku ya Jumatatu tarehe 12 Mei 2026, Itifaki ya Utekelezaji wa Mkataba wa pande mbili wa 2013 ilisainiwa kati ya Vatican na Kanisa mahalia  mbele ya Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher.

Askofu Mkuu Gallagher huko Cape Verde

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

13 Mei 2026, 10:22