Tafuta

2026.05.13 Skrini kubwa na sentensi za Papa Leo XIV. 2026.05.13 Skrini kubwa na sentensi za Papa Leo XIV. 

Kiti Kitakatifu:Programu ya kila siku inazinduliwa kwenye skrini kubwa za kidijitali

Baraza la Kipapa la Mawasiliano,kwa kushirikiana na Selfiestreet,itatangaza picha na maudhui yanayohusiana na Vatican katika baadhi ya maeneo maarufu zaidi jijini Roma na Milano nchini Italia.Katika fursa ya Kipindi cha Noeli 2025,Jumbe za Papa Leo XIV zilikuwa zimetangazwa kupitia skrini kubwa.

Vatican News

Baraza la Kipapa la Mawasiliano litatangaza picha na maudhui rasmi yanayohusiana na Kiti Kitakatifu kupitia skrini kubwa za kidijitali za mtandao wa Selfiestreet. Mpango huu utaanza Dominika tarehe 17 Mei 2026, kwa programu maalum katika baadhi ya maeneo maarufu zaidi jiji la  Roma na Milano nchini Italia.

Maeneo na Nyakati za Utazamaji

Jijini  Roma, katika Njia ya Tunisi - Makumbusho ya Vatican, matangazo maalum ya moja kwa moja yataoneshwa saa 6:00 mchana na  na 10:00 jioni masaa ya Ulaya. Programu itaendelea kwenye skrini kubwa kwenye  njia ya Lungotevere delle Navi saa 3:00 usiku na kisha saa 4:00 usiku katika uwanja wa Rimembranza. Huko Milano, programu itaonekana kwenye skrini kubwa kwenye njia Garibaldi saa 12:30 jioni. Katika siku zijazo, programu itaendelea kila siku kwenye skrini zote za mtandao wa Selfiestreet zinazohusika katika mpango huo, ikiendelea kutangaza maudhui rasmi ya Kiti Kitakatifu. Mpango huo pia utapanuliwa polepole, katika miezi ijayo, hadi skrini zingine za kidijitali katika miji mbalimbali ya Italia.

Ushirikiano wa Awali

Wakati wa Kipindi cha Noeli iliyopita, Selfiestreet tayari ilikuwa imetangaza mpango maalum wa mawasiliano ya kuona unaokisi misemo na maneno kutoka kwa Papa Leo XIV. Kuanzia Desemba 23 hadi 31, 2025, uteuzi wa picha muhimu za Papa na Kanisa, zikiambatana na jumbe zilizoongozwa na Noeli, zilitangazwa kwenye skrini kubwa zilizokuwa karibu na Basilika ya Mtakatifu Petro.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

14 Mei 2026, 09:21