Tafuta

Hia ya Kitume ya Papa Francisko nchini Ireland: Mkutano wa 24 wa Familia Kimataifa Hia ya Kitume ya Papa Francisko nchini Ireland: Mkutano wa 24 wa Familia Kimataifa  (Vatican Media )

Askofu Mkuu Luis Mariano Montemayor Ang'atuka Madarakani

Askofu mkuu mstaafu Luis Mariano Montemayor, alizaliwa tarehe 16 Machi 1956 nchini Argentina. Baada ya masomo yake ya Kikasisi, tarehe 15 Novemba 1985 alipewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tarehe 19 Juni 2008, Baba Mtakatifu Benedikto XVI akamteuwa kuwa ni Balozi wa Vatican nchini: Senegal, Cape Verde na Mwakilishi wa Kitume nchini Mauritania na hivyo kumpandisha hadhi na kuwa ni Askofu mkuu na hatimaye, kuwekwa wakfu tarehe 6 Agosti 2008.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV, tarehe 11 Julai 2026 ameridhia ombi lililowasilishwa kwake na Askofu mkuu Luis Mariano Montemayor, Balozi wa Vatican nchini Ireland la kutaka kung’atuka kutoka madarakani kadiri ya Sheria, Kanuni na Taratibu za huduma za kidiplomasia, Ibara 20§2. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu mstaafu Luis Mariano Montemayor, alizaliwa tarehe 16 Machi 1956 Jimbo kuu la Buenos Aires nchini Argentina. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 15 Novemba 1985 alipewa Daraja Takatifu ya Upadre.

Maaskofu wakati wa hija ya kitume Papa Francisko nchini Ireland
Maaskofu wakati wa hija ya kitume Papa Francisko nchini Ireland   (Vatican Media)

Tarehe 19 Juni 2008, Baba Mtakatifu Benedikto XVI akamteuwa kuwa ni Balozi wa Vatican nchini: Senegal, Cape Verde na Mwakilishi wa Kitume nchini Mauritania na hivyo kumpandisha hadhi na kuwa ni Askofu mkuu na hatimaye, kuwekwa wakfu tarehe 6 Agosti 2008. Baba Mtakatifu Benedikto XVI tarehe 17 Septemba 2008 akamteuwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Guinea Bissau. Tarehe 22 Juni 2015, Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa ni Balozi wa Vatican nchini Congo DRC.

Papa Leo XVI akizungumza na jopo la Mabalozi wa Vatican
Papa Leo XVI akizungumza na jopo la Mabalozi wa Vatican   (ANSA)

Tarehe 27 Septemba 2018, Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa ni Balozi mpya wa Vatican nchini Colombia na tarehe 25 Feburari 2023 akateuliwa na Baba Mtakatifu Francisko kuwa Balozi wa Vatican nchini Ireland hadi tarehe 11 Julai 2026 alipong’atuka kutoka madarakani. Tarehe 11 Julai 2026 Baba Mtakatifu Leo XIV akaridhia ombi lake la kutaka kung’atuka kutoka madarakani. Kimsingi Askofu mkuu mstaafu Luis Mariano Montemayor amelitumikia Kanisa kama Padre kwa Miaka 40 na kama Askofu kwa munda wa miaka 17 na usheee!

Kung'atuka
14 Julai 2026, 14:32