Tafuta

2026.06.29 Askofu Mkuu Westminster, Richard Moth, alipokea pallium kutoka kwa Papa Leo XIV Juni 29, 2026. 2026.06.29 Askofu Mkuu Westminster, Richard Moth, alipokea pallium kutoka kwa Papa Leo XIV Juni 29, 2026. 

Askofu Mkuu wa Westminster apokea pallium:‘Ni ishara yenye nguvu sana’

Askofu Mkuu Richard Moth alikuwa mmoja wa Maaskofu thelathini na watano waliopokea pallium kutoka kwa Papa Leo XIV.Katika mahojiano na Vatican News,alielezea ishara muhimu ya pallium, na jukumu lake jipya kama Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki a Uingereza na Wales na matumaini yake ya kuendelea na mazungumzo na Kanisa la Uingereza.

Na Kielce Gussie – Vatican.

Maaskofu wakuu 35 walioteuliwa hivi karibuni waliingia katika Basilika ya Mtakatifu Petro asubuhi ya tarahe 29 Juni 2026, mjini  Vatican na kuondoka na vazi jipya dogo la kiliturujia wakiwa na jukumu kubwa la Kanisa.  Papa Leo XIV aliwavalisha kitambaa  cheupe, kinachoitwa pallium, mabegani mwa Maaskofu Wakuu hawa wakati wa Misa ya Sherehe ya Watakatifu Petro na Paulo, Wasimamizi wa Mji wa Roma. Miongoni mwao alikuwa Askofu Mkuu wa Westminster, Richard Moth, ambaye alielezea mwingiliano huo wa Papa kama "jambo lisilo la kawaida." Hii ilikuwa kwa mara ya kwanza katika miaka kumi na moja kwa Papa kuwapatia tena  maaskofu wapya Pallium hilo ndani ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro.

Maaskofu wakuu wa Makanisa Makuu waliopokea Pallium
Maaskofu wakuu wa Makanisa Makuu waliopokea Pallium   (@Vatican Media)

Miaka kumi na moja iliyopita, Papa Francisko alihamisha sherehe hii ya kuwekwa kwa pallium kutoka Roma hadi kwenye majimbo makuu mahalia  ya Maaskofu wakuu pamoja na mabalozi wa Kitume. Maaskofu hawa wapya walialikwa kusherehekea Misa ya pamoja na Papa na kuhudhuria baraka ya pallium. Askofu Mkuu Moth alielezea Vatican News jinsi anavyopenda utamaduni wa kupokea pallium kutoka kwa Papa kwani ni "ishara ya ukaribu wake na huduma ya Petro kutoka kwa Baba Mtakatifu mwenyewe. Ni uzoefu wenye nguvu sana, ishara yenye nguvu sana nadhani kwa kila mtu."

Mwaka Mpya, majukumu mapya

Akitokea kuwa askofu wa Jimbo la Arundel na Brighton kusini mwa Uingereza kwa miaka kumi na moja iliyopita, Askofu Mkuu Moth alishiriki kwamba kuhamia Westminster kunahusu ukubwa. "Kutoka jumuiya 85 hadi 206, kwa hivyo yote ni kuhusu ukubwa. Ni kubwa tu na kuzoea kitu kikubwa kunahitaji kujiongeza", alibainisha. Hata hivyo, hii haikuwa jukumu jipya pekee alilochukua katika miezi saba iliyopita. Baada ya Papa Leo XIV  kumteua kuwa Askofu Mkuu wa 12 wa Westminster mnamo Desemba mwaka 2025 , Askofu Mkuu Moth alichaguliwa kuwa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki la Uingereza na Wales mnamo Aprili 2026. Alitumia nafasi hiyo , alikumbuka kuwa "alibarikiwa sana kwa Uingereza na Wales" kwa sababu ni "kundi la Maaskofu lililoungana sana na kuna hisia halisi kwamba tunafanya kazi pamoja kwa ajili ya mema ya utume wa Kanisa."

Mojawapo ya vipaumbele vya Mkutano wa Maaskofu ni kufanya kazi kwa ajili ya na kulinda heshima ya kila mwanadamu. Hasa, Askofu Mkuu alitoa mfano wa kufanya kazi ili "kuzuia muswada wa usaidizi wa kufa", ambao alisema, "tutakabiliana nao tena, inaonekana kama katika wakati ujao." Askofu Mkuu Moth alitania kwamba kuwa Rais wa Baraza la Maaskofu ni kazi ya ziada kidogo, lakini pia ni fursa kubwa kazi ambapo anahisi kweli "msaada wa maaskofu ndugu zake."

Kuanza alfajiri saa 11.00 kwa sala

Akitazama Jimbo lake Kuu jipya, Askofu Mkuu alisisitiza kwamba sala imekuwa na itaendelea kuwa msingi wa kazi yake. "Jambo ambalo limezidi kuwa wazi kwa miaka mingi kwamba nimekuwa Askofu ni kuanza kila kitu kutoka mahali pa sala kwa sababu tusipofanya hivyo, hatuwezi kufanya chochote," alisema. Kwa maombi, Askofu Mkuu Moth alishirikisha, kwamba "tumeandaliwa vyema kutimiza utume ambao Mungu ametuitia. Kwa sababu hiyo, malezi ni mojawapo ya mambo anayolenga katika jukumu jipya. Kutumia maombi na malezi, ili yaunganishe, na wito wetu kama Wakristo wa kutangaza Injili inawezekana" jambo ambalo Askofu Mkuu alisisitiza kwa miaka mingi kabla ya chapisho hili jipya.

“Ikiwa kuna mtu yeyote anayesikiliza haya katika Majimbo la Arundel na Brighton watakuwa wamesikia haya mara kadhaa tunazungumzia sala hii, malezi na kisha kazi ya utume.” Huu ni ujumbe ambao Askofu Mkuu Moth aliuzingatia. Anatenga muda kila siku kujitolea kwa ajili ya maombi sio mwisho na si katikati. “Ni saa kumi na moja asubuhi kila siku  anatoa  muda kabla ya siku ya mikutano na mambo mengine yanayokuja baadaye  na wakati huo wa maombi, wakati huo wa ukimya ambao kila kitu hukua,” Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki la Uingereza na Wales alisisitiza.

Maaskofu wakuu wa makanisa makuu walipokea pallium
Maaskofu wakuu wa makanisa makuu walipokea pallium   (@Vatican Media)

Maaskofu wakuu wawili, mazungumzo yao yanafanana

Mnamo Aprili mwaka huu 2026 Askofu Mkuu Moth alisafiri kuja Roma na kushiriki katika mkutano na Papa Leo XIV na Askofu Mkuu mpya wa Canterbury, Sarah Mullally. Alishirikisha kwamba,  yeye na Askofu Mkuu wa Canterbury walikuwa na jukumu siku ya kuwekwa wakfu kwa kila mmoja nchini  Uingereza.

"Nadhani wasikilizaji walitoa ishara ya hamu yetu ya kufanya kazi pamoja pale tunapoweza," Askofu Mkuu Moth alielezea. "Nadhani kutakuwa na maeneo fulani katika suala la ufikiaji wa kijamii Uingereza na Wales yote ambapo tutaweza kufanya kazi pamoja." Akitzama  mustakabali wa uhusiano kati ya Kanisa Katoliki la Roma na Kanisa la Uingereza, alisisitiza umuhimu wa kudumisha mazungumzo kati yao. Askofu Mkuu Moth na Askofu Mkuu Mullally wote ni "marais wa makanisa pamoja Uingereza pamoja na wengine, kwa hivyo kutakuwa na fursa za kufanya kazi pamoja.

ASKOFU MKUU WA WESTMISTER NA PALLIUM

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

01 Julai 2026, 10:56