Tafuta

2026.07.01 Askofu Mkuu Sithembele Sipuka,wa Capetown,Afrika Kusini. 2026.07.01 Askofu Mkuu Sithembele Sipuka,wa Capetown,Afrika Kusini.  (©Sr Christine Masivo)

Askofu Mkuu wa Capetown apokea Pallium kutoka kwa Papa Leo XIV

Miongoni mwa Maaskofu wakuu 35 waliopokea Pallium kutoka kwa Papa Leo XIV katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro kwenye Sherehe ya Watakatifu Petro na Paulo alikuwa Askofu Mkuu Sithembele Sipuka wa Cape Town.Sherehe ya kiliturujia iliashiria uhusiano rasmi wa Askofu Mkuu na Papa Leo XIV na kuthibitisha tena utume wake wa kichungaji wa kuwatumikia watu wa Mungu.

Na Sr. Christine Masivo, CPS – Vatican.

Akizungumza baada ya Misa Takatifu katika Basilika ya Mtakatifu Petro mjini  Vatican tarehe 29 Jumi 2026 katika  maadhimisho ya Sherehe ya Mtakatifu Petro na Paulo, Askofu Mkuu Sithembele Sipuka wa Jimbo Kuu Katoliki la Cape Town nchini Afrika Kusini  alikuwa mmoja wa Maaskofu wakuu 35 ambao Papa Leo XIV aliwapatia  Pallium, ambalo ni vasi la sufi safi inayotengenezwa kwa manyoya ya kondoo wachanga  ambapo ni ishara inayoonekana ya ushirika wake na Baba Mtakatifu na jukumu la kichungaji alilokabidhiwa kama Askofu Mkuu wa mji Mkuu (Metropolitan) wa Nchi anayoiwakilisha. Askofu Mkuu huyo alitafakari maana ya Pallium, wito wa uongozi, na wito wa Kanisa wa kukuza umoja, haki, na upatanisho nchini Afrika Kusini.

Papa aliwavalisha Pallium Maaskofu wakuu
Papa aliwavalisha Pallium Maaskofu wakuu   (@Vatican Media)

Ushirika na shukrani

Tofauti na miaka ya awali, ambapo Pallium ilivikwa kwa Maaskofu wakuu katika majimbo makuu mahalia baada ya baraka yake huko Roma, kwa mwaka huu 2026, Papa Leo XIV alitoa binafsi Pallium wakati wa sherehe ya kiliturujia katika Basilika ya Mtakatifu Petro, huku akisisitiza utamaduni wa kale ulioonesha uhusiano kati ya maaskofu wakuu wa jiji na utume wa Petro. Askofu Mkuu Sipuka alitoa shukrani zake kwa wote walimsindikiza  wakati wa tukio hili muhimu, akiwashukuru wote waliowezesha. Alimshukuru Kardinali Stephen Brislin wa Afrika Kusini kwa msaada wake wa kidugu na kwa kumtambulisha kwa jumuiya ya  Australia, mahali pa ukarimu na uchangamfu unaowakaribisha mahujaji na wale wanaotafuta makazi Roma, wajumbe wa Baraza la  Maaskofu Katoliki la Afrika Kusini (SACBC), na wote walioungana  na sherehe hiyo.  "Mnaleta kitu cha nyumbani kwenye meza hii hapa Roma," alirudia.

Jumuiya Italia ikimpongeza Askofu Mkuu Sipuka kuvaa Pallio
Jumuiya Italia ikimpongeza Askofu Mkuu Sipuka kuvaa Pallio   (©Sr Christine Masivo)

Naye  Kardinali Stephen Brislin wa Afrika Kusini alimpongeza Askofu Mkuu Sipuka kwa kupokea Pallium na akatoa shukrani kwa kukubali kwake kwa ukarimu huduma aliyokabidhiwa. "Sifa yako ndefu ya uongozi wa kichungaji kama Askofu wa Mthatha, Rais wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Afrika na Madagascar (SECAM), Rais wa Baraza la Makanisa, Afrika Kusini na sasa kama Askofu Mkuu wa Cape Town, ni mfano mwema kweli" Kardinali alibainisha. Kardinali pia alitoa udhihirisho thabiti wa Askofu Mkuu Sipuka wa huduma ya uaminifu kwa Kanisa, akimtaja kama mchungaji aliyejitolea kwa  ajili ya Injili na kwa watu aliokabidhiwa kuwaongoza. Pia alimpongeza Askofu mkuu kwa utayari wake wa kuhutubia na kuwakilisha Kanisa kitaifa na kimataifa, akizungumza dhidi ya ufisadi, umaskini, na ukosefu wa usawa; aliunga mkono mazungumzo ya imani mbalimbali, na kuhimiza upatanisho na utawala bora.

Pallio wito wa kuwachunga watu wa Mungu

Askofu Mkuu Sipuka alitafakari kuhusu Pallium, akiielezea kama vazi dogo la kiliturujia lenye jukumu kubwa. Alieleza kwamba katika maisha yake yote mara nyingi alikabidhiwa nafasi za uongozi, lakini kupokea pallium kutamsaidia kuelewa maana halisi ya wito huo. "Pallium(pallio)Takatifu ni kitambaa cha sufi iliyowekwa mabegani, na inanikumbusha Mchungaji Mwema anayewaelekeza na kuwabeba kondoo waliopotea nyumbani," alisema. Alitoa maoni zaidi kwamba uongozi si kuhusu hadhi au upendeleo, bali ni kuhusu kuwabeba wengine mabegani mwako katika huduma ya upendo, hakuna mchungaji anayetembea peke yake; wakati mwingine mchungaji anahitaji kubebwa. “Tunda lolote ambalo huduma hii imezaa ni kazi ya neema ya Mungu, na ninawashukuru wote walioniunga mkono katika huduma yangu yote ya kikuhani na kiaskofu,” alieleza kwa unyenyekevu.

Kubebwa kwa Pallium za Maaskofu wakuu wa Kanisa
Kubebwa kwa Pallium za Maaskofu wakuu wa Kanisa   (@VATICAN MEDIA)

Kutumwa katika ushirika

Akitafakari kauli mbiu yake ya kiaskofu, “Kwa pamoja na Kutumwa”, anapata msukumo kutoka katika ushuhuda wa Watakatifu Petro na Paulo. Alieleza kwamba Petro anawakilisha umoja wa Kanisa lililokusanyika karibu na Mrithi wa Petro huku Paulo akiwakilisha wito wa kimisionari wa Kanisa wa kutangaza injili kwa kila taifa na watu. “Pallio inaniunganisha kwa Mrithi wa Petro na kwa Kanisa la ulimwengu wote. Wakati huo huo, inanituma katika utume ili kuongozana na watu wa Mungu popote walipo.” Akielekeza mawazo yake kwenye hali nchini Afrika Kusini, Askofu Mkuu alitoa wito wa kujitolea upya kwa udugu na mshikamano huku kukiwa na mvutano unaoongezeka unaoathiri wahamiaji na wakimbizi kutoka nchi zingine za Afrika. Akitambua hali halisi ya kijamii inayowakabili Waafrika Kusini, alionya dhidi ya kuelekeza kukatishwa tamaa kwa wahamiaji walio katika mazingira magumu ambao wenyewe wanatafuta usalama, kazi na heshima.

Kuvalishwa kwa Pallium Maaskofu wakuu
Kuvalishwa kwa Pallium Maaskofu wakuu   (@Vatican Media)

Askofu Mkuu alisisitiza jamii kushughulikia chanzo kikuu cha dhuluma kupitia mazungumzo, uwajibikaji wa pamoja na sera zinazokuza manufaa ya wote badala ya mgawanyiko. "Maumivu yetu yanatutaka tusipate mtu wa kulaumu bali kitu cha kujenga," alisema.

Askofu Mkuu Sipuka na Watawa wakimpongeza
Askofu Mkuu Sipuka na Watawa wakimpongeza   (©Sr Christine Masivo)

"Ni kwa pamoja tu, ndipo tunaweza kutafuta suluhisho ya kudumu zinazodumisha heshima ya kila mtu." Kwa kuhitimisha Askofu Mkuu Sipuka alikabidhi huduma yake kwa Bwana, akiomba kwamba Pallio imkumbushe kila wakati wito wake wa kuimarisha ushirika ndani ya Kanisa na kuwatumikia watu wa Mungu kwa uaminifu, unyenyekevu, na matumaini.

ASKOFU MKUU SITHEMBELE SIPUKA NA PALLIUM NA PAPA

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

01 Julai 2026, 11:16