Kikundi Kazi cha Upendo:Mtandao wa Kuwasaidia Maskini wa Roma
Benedetta Capelli – Vatican.
Kutembea pamoja, kusikiliza uzoefu wa kila mtu na kuutumia vyema, kusindikizana na wale wanaoomba msaada katika mpango halisi na si tu katika kukabiliana na hitaji la haraka. Hii ndiyo maana ya mkutano wa kwanza wa Kikundi Kazi cha Upendo ulioandaliwa na Baraza la Kipapa la Huduma ya Upendo kwa ushirikiano wa karibu na Jimbo kuu la Roma, ambao ulifanyika tarehe 7 Julai 2026 katika Jumba la Mtakatifu Calisto, kwenye Makao Makuu ya Baraza la Kipapa la Kuhamasisha Maendeleo fungamani ya Binadamu. Kardinali Michael Czerny alitoa salamu kutoka Baraza la Kipapa la Kuhamasisha Maendeleo Fungamani ya Binadamu, akisisitiza uhusiano wa karibu kati ya "huduma ya upendo na kuhamasisha maendeleo fungamani ya binadamu" katika kulinda heshima ya kila mtu na "katika kujitolea kuhakikisha kwamba hakuna mtu anayeachwa."
Mkutano huo, ambao pia ulihudhuriwa na Kardinali Baldo Reina, ambaye ni Makamu wa Jimbo Kuu la Roma, ambaye alifungua kikao hicho kwa kusisitiza umuhimu wa mpango huo kwa maslahi ya walio hatarini zaidi na thamani ya ushirikiano katika huduma yao, ulihudhuriwa na mashirika mengi ya upendo yanayofanya kazi katika eneo hilo: Caritas Roma, Wahamiaji, Ofisi ya Jimbo kwa Ushirikiano wa Kimisionari kati ya Makanisa, Kituo cha Astalli, Shirika la Malta, Jumuiya ya Mtakatifu Egidio, Wamisionari wa Comboni, Wavincentiani, Wascalabriniani, Vyama vya Walei vya Kijimbo, ACLI (Kikundi Matendo cha Kikatoliki cha Italia), Wamisionari wa Upendo wa Mama Teresa wa Calcutta, na Ndugu wa Tafakari.
![]()
Meza kwa ajili ya Kazi kuhusu Upendo katika ukweli wa upendo jijini Roma
Kutenda pamoja
"Ishara halisi ya kisinodi," alielezea Askofu Mkuu Luis Marín de San Martín, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Upendo, katika hotuba yake, "ambayo alisema kuwa alihubiri miaka mitano akiwa kama Katibu Msaidizi wa Sekretarieti Kuu ya Sinodi, alisema "tumeitwa sio kuitambua tu, bali kuishi na kuifanya ionekane." Safari ya pamoja na ya kidugu ya kutoa jibu kamili kwa ajili ya changamoto za umaskini, "mabadiliko ya kijamii ya haraka na mara nyingi yanayovuruga mwelekeo," na matatizo yanayowakabili wale wanaowatunza watu wenye magonjwa ya akili. "Yote haya," alisema "yanatutaka tusonge mbele katika mwelekeo wa kuyafanya pamoja kama mwili mmoja wa kikanisa."
Uwajibikaji
Mapendekezo matatu yalitolewa: "kuhamasisha uwajibikaji wa pamoja," kwa sababu kila ukweli una wigo wake tofauti, na kwa hivyo ni muhimu kufanya kazi pamoja, sio kuingiliana. "Kutoka katika mtazamo huo," alisisitiza Askofu Mkuu Luis Marín de San Martín, "kuna hamu ya majadiliano ya moja kwa moja kuhusu jinsi kila mmoja wetu anavyoweza kuwasaidia vyema kaka na dada zetu wanaohitaji."
![]()
Askofu Mkuu Luis Marín de San Martín,Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Upendo
Ushirikiano
Pendekezo jingine ni kukuza ushirikiano. Kuanzia Kanisa linalosonga mbele, kama kawaida, kuwa "chumba cha dharura cha upendo" kulingana na ufafanuzi wa Ofisi ya Kipapa ya Misaada ya Kipapa na Kardinali Konrad Krajewski, hadi Kanisa linalotembea pamoja, likishiriki taarifa, uzoefu, na ujuzi ili kuelewa vyema mahitaji na kujenga njia zenye ufanisi zaidi. Yote haya huku likiheshimu utambulisho na karama, kwa sababu "utofauti, unapoishi katika ushirika, unakuwa utajiri wa kiroho."
Kusindikiza
Hatimaye, pendekezo la mwisho linahusu kuingizwa kwa aina mbalimbali za upendp. Kwa maana hiyo, meza ya majadiliano ni jukwaa la kufanya kazi katika kuwahudumia maskini, "bila kujali hadhi ya kichungaji au kisheria." Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Upendo, alisisitiza kuwa, Baraza hilo halikusudii kuchukua nafasi ya mashirika ya kibinafsi, bali kuhamasisha majadiliano, kuwezesha mazungumzo, na kusindikizana, kwa kujiweka "katika huduma ya chochote ambacho Roho anataka kuhamasisha kupitia mchango wa kila mtu."
Mpango wa Meza ya Kazi kuhusu Upendo
Mpango uliounganishwa na unaoendelea
Kuunganisha miongozo hii kunamaanisha kuunda "mtandao wa ndani unaoweza kusindikizana na watu kupitia mpango," ambao si jibu la haraka tu bali pia unamaanisha "kujenga njia na mtu" inayojumuisha "kukaribishwa na kusikilizwa, usaidizi wa vifaa, huduma ya afya, programu za elimu na ujumuishaji wa kazi, na mwongozo wa kiroho." Njia ya kuwekwa uhai, ambapo kukuza uaminifu, "uvumilivu wa kuelewana, nia ya kutojifunga ndani binafsi," kila wakati ukijiweka chini ya mwongozo wa Roho Mtakatifu," alihitimisha Askofu Mkuu Luis Marín de San Martín. Kundi kazi litaendelea kushiriki katika majadiliano na ubadilishanaji unaoendelea miongoni mwa washiriki, likilenga kudumisha mtandao huu wa ushirikiano kwa maslahi ya walio hatarini zaidi na kufikia malengo ya pamoja. Ili kuunga mkono mchakato, mikutano mitatu imepangwa kila mwaka, kwa mwezi Juni, Oktoba, na Februari, ambayo itatoa fursa za kutafakari na kushirikisha.
Imesasishwa tarehe 9 Julai 2026 saa 5:00 na Angella Rwezaula.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.