Vatican:AI itakuwa maendeleo ya kweli tu ikiwa itahudumia hadhi ya binadamu!
Vatican News
Katika taarifa ya Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Umoja wa Mataifa, akihutubia tarehe 13 Julai 2026 katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa huko New York, Marekani wa mkutano wa Baraza la Uchumi na Kijamii (ECOSOC) lililojitolea kwa mada "Kufanya vyema zaidi: Kuharakisha hatua za haraka na za mabadiliko ili kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu ifikapo 2030,” alibainisha kuwa “Kipimo halisi cha maendeleo hakitakuwa katika ustaarabu wa teknolojia zinazoibuka, bali kama zimewekwa kwa ajili ya kumtumikia binadamu na manufaa ya wote.
Uwezekano na Hatari za AI
Ujumbe wa Vatican, ukifuata waraka wa Papa Leo XIV wa Magnifica Humanitas, ulisisitiza kwamba akili unde "ina uwezo wa kuharakisha maendeleo kuelekea Malengo ya Maendeleo Endelevu, ikiwa ni pamoja na yale yanayorekebishwa mwaka huu." Hata hivyo, ikiwa teknolojia hii mpya ikiathiri hadhi ya mwanadamu, haijalishi yenye ufanisi, faida, au ubunifu, kweli haiwezi kuwa njia ya kufanya vizuri zaidi." Ingedhoofisha maono ya maendeleo endelevu yaliyoainishwa katika Ajenda ya 2030, ambayo kulingana na hadhi ya mwanadamu lazima iwe kitovu cha kila juhudi za maendeleo. Lengo la maendeleo, ni ukombozi kamili wa watu kutokana na njaa, magonjwa, kutojua kusoma na kuandika, na umaskini." Lengo hili linaweza kufikiwa, kiuchumi, tu kupitia ushiriki sawa katika michakato ya kimataifa, kijamii, kujenga jamii kulingana na mshikamano, na kisiasa, ns kuimarisha taasisi za kidemokrasia zinazohakikisha uhuru na amani."
Ukuaji wa uchumi bado haufanyi kazi vizuri
Ingawa "ukuaji wa uchumi umekuwa halisi na tayari umefikia mengi na kuwawezesha mabilioni ya watu kuepuka umaskini uliokithiri, bado unaoneshwa na matatizo makubwa, kama vile "kuongezeka kwa ukosefu wa usawa - kati na ndani ya nchi - na kuibuka kwa aina mpya za umaskini." Mwishoni mwa taarifa yake, ujumbe wa Vatican katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa kwa hivyo ulihimiza kukabiliana na matatizo haya na kutambuahadhi isioweza kuepukika wa mwanadamu," hasa ili kushikilia "ahadi zilizofanywa katika eneo la maendeleo endelevu."
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.